Hii ya kubadilisha KM za gari hivi ni kweli ipo? Kuna gari namba BAC ina KM 38900 TOYOTA KLUGER jamaa anaiuza

Si utahisiwa ni mwizi kwa kufatilia mambo yote hayo
 
Ulipigwa na Yeye alipigwa
 
Upo uzi fulani unatangaza magari hapa JF, gari zote hazina km 100,000.
 
Chief wewe ni fundi gari..

Maelezo haya nimeona kwenye mtandao wa kijamii, yanafanana asilimia 100 hadi hicho kisa cha jamaa yako ni 100%
 
Achana na hiyo gari tafuta pesa uagize yakwako...... Watu wana mambo ya kishenzi sana. Siajabu hata engine itakuwa haipo sawa.
 
Kwa total mileage ya 38,000 kms gari hiyo ni mpya kabisa..... Sasa ndio mtu akuuzie mkononi kwa bei ya kawaida?!
 
Hii hatari sana sasa wapi kuna usalama maana YARD nako nasikia ujanja ujanja tu , mkononi nako ujanja ujanja tu labda sasa niagize mwenyewe japan
Sio yard zote. Kuna yards zinareputation nzuri. Wanaingiza gari mpya kila baada ya miezi michache. Hawa kukubambikia ni ngumu.

Ila hizi yard za wadau wanaojaribu biashara ndio kuna upuuzi mwingi.
 
Yupo mwamba pia ana gari D Km 50.000km ila imechoka kweli
 
Zinashushwa hizo tena dakika chache tu.. mara nyingi wanacheza na namba za mwanzo! hiyo lazima ilikua 138900 au pengine hata 238900
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…