Hii ya mchele wa Mbeya ni kali

Nakusoma sana mkuu
Ujue sisi ndio tulio badilisha makao makuu ya mkoa wa songwe badala ya kwenda chunya ambako ni pembeni ya mji wakaleta vwawa ambambapo ni sehemu ya katikati

Maana tulisema kama watapeleka chunya sisi tunahamia malawi
 
Aisee haya mambo ya mpunga, yamenikumbusha mbali sana, enzi hizo za kufukuza ndege kwenye mpunga, kupanda na kunyeshea mpunga wenyewe, mwisho wa siku hayo mashamba kwa sasa ndipo kilipo chuo kimoja maarufu hapa nchini, mashamba hayapo tena, kuna madarasa tu watu wanapiga shule.
 
Mchele wa Kyela mzuri sana. nakumbuka zamani baba yetu alienda Kyela akaja nao! aiseee yaani ilikuwa mama akipika hadi mitaa ya mbali kabisa wanasikia harufu. Ila sasa isije ikawa hizi mbolea zimeharibu ardhi ya asili na huo mchele haupo tena.
Kyela na Magugu manyara ilikua ni balaa mtaa mzima.una harufu tatizo mbegu wamechakachua
 
Hivi hapo Kyela sasa hivi mchele bei ya kilo, debe na gunia ni shilingi ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…