Hii ya Wamasai ni testing ground ya kuhamisha Watanzania wengine maeneo yao

Hii ya Wamasai ni testing ground ya kuhamisha Watanzania wengine maeneo yao

Kuhamishwa wao sio wa kwanza wala hawatakuwa wa mwisho.....

Ujenzi wa mji wa serikali Dom, watu si wamelipwa?

Standard gauge vipi watu hawakuamishwa?

Waliokuwa wanakaa mabondeni hapo dar hawakuamishwa?

Watu wanajitoa ufahamu wakati haya mambo yapo Kila siku na yataendelea kuwepo.

Mleta uzi asichojua ardhi ni Mali ya serikali na Rais ni custodian mkuu wa ardhi.

Kama jambo lina manufaa mapana watu hamna budi kuhama na hawa wamasai watahama tu.
 
Unaonekana kabisa wewe sio mtanzania! Kwa watanzania tunajua kabisa kuwa kuhamishwa ni jambo la kawaida maana hata mwaka 1974 tulihamishwa kuanzisha vijiji vya ujamaa

Wasalimie hapo Nyeri Kenya
 
Manufaaa ya kupisha wenye pesa? Kwa hio hata nchi ikizuwa unaona ni sawa kwa sababu ni kwa masilahi ya nchi?
 
Unaonekana kabisa wewe sio mtanzania! Kwa watanzania tunajua kabisa kuwa kuhamishwa ni jambo la kawaida maana hata mwaka 1974 tulihamishwa kuanzisha vijiji vya ujamaa

Wasalimie hapo Nyeri Kenya
Walihamishwa kupisha watu wengine?
 
Kwa akili zako fupi, ukiambia rudisha nyumba yako nyuma kidogo unaelewa nini??
Wewe ndo una akili kama piliton, Tofautisha kuhamisha watu kupisha watu wenye pesa na kuhamisha watu kupisha project ya Serijali ambapo ni nyumba chache huhamishwa, Kule North Mara hadi leo watu wamebakia masikini kisa kupisha Mgodi,
 
Hakuna kitu mtafanya nakuhakikishia
Hahaha kwa wachaga mkuu.
Mtachezea jamii zote lakini ardhi ya mchaga huwa haiguswi kabisa hata kwa kuuza mchaga hauzagi ardhi kamwe labda abadilishane na ndugu yake.
 
Manufaaa ya kupisha wenye pesa? Kwa hio hata nchi ikizuwa unaona ni sawa kwa sababu ni kwa masilahi ya nchi?

Nchi inauzwa kwa nani? Hizo story zenu za vijiweni zinaaminiwa na watu mazwazwa tu kama wewe.

Hata nyumbani kwako serikali ikiona Hilo eneo Linafaa kwa shughuli zingine litachukuliwa na wewe utaondoka kwa hiari au shurti. Hii nchi Haina watu special kuliko wengine.

Wamasai wa Ngorongoro wasepe au watasepeshwa.
 
Wamasai sio jamii ya kwanza kuhamishwa ili kupisha shughuli zingine. Watu kila siku wanahamishwa kupisha ujenzi wa barabara, majengo, viwanja vya ndege na maendeleo mengine.

Tena hawa wamasai wamepewa eneo jipya, usafiri na fidia kabisa wahame tu kwa amani. Prof Jay na watanzania wengi wamevunjiwa nyumba zao bila fidia yeyote.

Hawa mayeroo wakiendelea kujazwa kwamba wao ni special sana hawapaswi kuhama watakipata wanachokitafuta.
Mleta mada anaweza kuwa ni mdogo kiumri wakati mengine yanafanyika hapa nchini alikuwa aidha hajazaliwa au hajapata akili ya kujua nini kinaendelea.
 
Mikono imekuwa mirefu, kama sio kamba ya mbuzi imekatika.
 
Back
Top Bottom