Hii ya wanafunzi wa Rwanda ni fitina au vilaza

Hii ya wanafunzi wa Rwanda ni fitina au vilaza

Apitakujilamba

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2013
Posts
205
Reaction score
82
Habari za jioni wanajamvi!

Leo hii nimekutana na tukio moja la kushangaza kidogo. Tulikuwa tunajadili mambo mbalimbali ya masomo na wanyarwanda ambao nasoma nao nje ya nchi. Baada ya mazungumzo mengi wakaanza kunidodosa mambo yahusuyo elimu ya Tanzania, swali kubwa ambalo niliulizwa hivi elimu ya Tanzania ni ngumu sana, kuna tofauti gani kati ya elimu ya Tanzania na Rwanda au nchi nyingine za afrika mashariki.

Baada ya mazungumzo ya muda kidogo nilikuja kugundua chanzo cha maswali yote hayo ilikuwa kuna wanafunzi wapatao 35 kati ya 100 waliokuwa wanasoma Chuo kikuu wamefeli (Disco) na wanatakiwa kurudi Rwanda. Hao wanyarwanda wanasema hii ni mara ya kwanza kutokea kwao kwa kuwa wanafunzi hupelekwa sehemu mbalimbali afrika mashariki na sehemu nyingine lakini haijawahi kutokea wanafunzi wakafeli namna hii.

Kiukweli hawajasema direct kwamba kuna fitina imefanyika kwa wanafunzi wao lakini hisia zao zinaonyesha moja kwa moja kwamba wamehujumiwa. Ingawa walionyesha labda tatizo la lugha maana wanafunzi wengi wa Rwanda, elimu yao huipata kwa kifaransa na chinyarwanda lakini bado wanajiuliza kwa nini iwe mwaka huu na sio miaka mengine. Kwa sasa wizara ya elimu inawasubiri wanafunzi hao ili kuongea nao kujua chanzo cha wanafunzi wengi kufeli, kwa kuwa wanafunzi wote hao walikuwa wansomeshwa na serikali ya Rwanda.
 
Hii mbona inawezekana, hasahasa kama wengi wao walikuwa College of Engineering UDSM. Nakumbuka kuna kipindi kulikuwa na wanafunzi kutoka Mozambique, Zambia etc wengi wao walidisco. Sasa sijui ilikuwa ni ugumu wa kitabu au walikuwa wanapenda kujirusha.
Ila kwa ufupi, kwa utaratibu uliopo kwenye vyuo vyetu ni vigumu sana kumfanyia hujuma mwanafunzi yeyote maana kila kila lecturer anasahihisha na kutoa marks kwenye course yake.
 
Anapaswa kujiuliza kama kwenye hichi chuo ni wanyararwanda peke yao waliofeli. Nina uhakika kuna watanzania wengi sana watakuwemo.
 
Majungu na fitina za kisiasa vikianza kuhusishwa na taaluma, basi Hata mwanafunzi huyo atiliwe Shaka uwezo wake wa kiakili. Ku-disco Ni kawaida sana na hakubagui dini, Kabila, Taifa wala rangi.
 
Sijui sijaelewa uzi au vipi? Wewe pamoja na hao Wanyarwanda mnasoma nje ya nchi sio? Sasa kama ni nje ya nchi, hizo fitina zinatoka wapi? Tunaouwezo wa kufanya fitina sisi hadi kwenye mipaka ya nchi nyingine kuwafitini Wanyarwanda? Kwani tunaugomvi nao? All in all, Kitabu cha Tanzania ni kweli kigumu, tunasoma masomo mengi sana this is why tukiendaga nje ya nchi kufanya course yoyote, Mtanzania hua ngumu sana kufeli, labda iwe ni zile nchi ambazo sio English speaking countries. Huo ndio ukweli
 
Bora hao wamefeli katika level ya Chuo Kikuu kule Liberia ilishindikana hata kuwapata wanafunzi wa kujiunga na vyuo. Kuna sababu nyingi sana lakini moja wapo ya sababu kuu ni athari za utandawazi. Utandawazi una wigo mpana sana tusikurupuke kudhani ni internet.
 
Wanaofeli wengi tatizo ni lugha!!!!!!

Mtu kasoma french tangu chekechea halafu elimu ya juu akutane na english? ??!!!!!
Kuna waliosoma english nadhani kama option hawa hawapati taabu wakiwa higherlearning

Hebu waulize huko kwao wanatumia lugha gani????!!!!!
 
Mleta mada umenikumbusha wakati flani nikiwa nasoma chuo kikuu. Kuna wabotswana kama nane walidisco wote na kurudishwa kwao. Utasema nayo ilikuwa siasa! Nijuavyo mimi kudisco ni combination na mambo mengi na isichukuliwe kuwa mtu anakuwa hana uwezo. Labda kwavile imetokea wakati huu ambapo tumekuwa na uhusiano wa mashaka ndo maana hisia nyingi zinaeleza kuwa pengine ni hujuma. Ninaamini hakuna hujuma.
 
Mkuu hacha hizo hisia, mwaka huu UDSM wamedisco watu wengi.

*Chuo kizima upande wa main campus wamedisco jumla ya wanafunzi 500. (KABLA YA MATOKEO YA SUPPLIMENTARY)

* Waliofanya supplimentary walikuwa wanafunzi 1000.
 
Duh, haya ndo matatizo ya kupeleka kila mtu Chuo Kikuu hata kama ana marks za shida shida, TCU imeleta balaa sana, inatuaribia UDSM yetu!
 
Sijui sijaelewa
uzi au vipi? Wewe pamoja na hao Wanyarwanda mnasoma nje ya nchi sio?
Sasa kama ni nje ya nchi, hizo fitina zinatoka wapi? Tunaouwezo wa
kufanya fitina sisi hadi kwenye mipaka ya nchi nyingine kuwafitini
Wanyarwanda? Kwani tunaugomvi nao? All in all, Kitabu cha Tanzania ni
kweli kigumu, tunasoma masomo mengi sana this is why tukiendaga nje ya
nchi kufanya course yoyote, Mtanzania hua ngumu sana kufeli, labda iwe
ni zile nchi ambazo sio English speaking countries. Huo ndio
ukweli

Nadhani hujanielewa, ni kwamba rwanda inautaratibu wa kuleta wanafunzi UDSM, lakini mwaka huu wanafunzi 35 kati ya 100 wamedisco na kurudishwa rwanda.
 
Ni sababu za ki-academics zaidi,haina uhusiano wowote na uhusiano wa kidiplomasia ulioyumba kwa sasa....
 
Wanaofeli wengi tatizo ni lugha!!!!!!

Mtu kasoma french tangu chekechea halafu elimu ya juu akutane na english? ??!!!!!
Kuna waliosoma english nadhani kama option hawa hawapati taabu wakiwa higherlearning

Hebu waulize huko kwao wanatumia lugha gani????!!!!!

miaka ya karibuni wameanza kufundisha kwa kingereza vyuoni, lakini si unajua mfano hapa tz mwalimu atafundisha kwa kingereza akiona hamuelewi anawaelewesha kwa kiswahili vivyo hivyo kwao wakiona hawaelewi wanamix na french au kinyarwanda
 
Nadhani hujanielewa, ni kwamba rwanda inautaratibu wa kuleta wanafunzi UDSM, lakini mwaka huu wanafunzi 35 kati ya 100 wamedisco na kurudishwa rwanda.

Sasa hivi hata mimi nimekuelewa. Unajua ukisema chuo kikuu inakuwa siyo rahisi kujua kuwa una maanisha UDSM pekee kwani kuna vyuo VIKUU vingi ndani na nje ya nchi ya TZ.
 
Hii mbona inawezekana, hasahasa kama wengi wao walikuwa College of Engineering UDSM. Nakumbuka kuna kipindi kulikuwa na wanafunzi kutoka Mozambique, Zambia etc wengi wao walidisco. Sasa sijui ilikuwa ni ugumu wa kitabu au walikuwa wanapenda kujirusha.
Ila kwa ufupi, kwa utaratibu uliopo kwenye vyuo vyetu ni vigumu sana kumfanyia hujuma mwanafunzi yeyote maana kila kila lecturer anasahihisha na kutoa marks kwenye course yake.

Nakubaliana na wewe hata mie kuna wanafunz wa nyaruanda nlisima nao UDSL wao walikua wanajitenga na hawakua wana assosiate na wabongo materials walikua nazo ila hawakua wanafanya discussion na hawaku share madesa at the end of the day wali disco sasa utasema wameonewa??
 
Ni vilaza tu hao.Wamezoea elimu za kutafuniwa ndo maana wakija kwenye nondo's
wanadisco
 
Mkuu hacha hizo hisia, mwaka huu UDSM wamedisco watu wengi.

*Chuo kizima upande wa main campus wamedisco jumla ya wanafunzi 500. (KABLA YA MATOKEO YA SUPPLIMENTARY)

* Waliofanya supplimentary walikuwa wanafunzi 1000.

kila mtu anavuna alichokipanda, kama walikuwa vilaza wasigeuze suala hili likawa la KIDIPLOMASIA
 
Waambie Tz hatuna elimu ya kuwafaulisha wote walioko darasani kama huko kwao,hapa kufeli kupo na kama hawaamini waambie wafanye research kidogo kwa miaka kumi iliyopita alafu jibu watapata wenyewe ...usikubali wakusumbue kwa vitu wanavyoweza kutafiti na kujua historia ya kufeli ya chuo kama UDSM,kingine wakumbushe hii siyo KIU&co. tunakoambiwa kufaulu bwerere na GPA za matawi ya juu.
 
Back
Top Bottom