Apitakujilamba
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 205
- 82
Habari za jioni wanajamvi!
Leo hii nimekutana na tukio moja la kushangaza kidogo. Tulikuwa tunajadili mambo mbalimbali ya masomo na wanyarwanda ambao nasoma nao nje ya nchi. Baada ya mazungumzo mengi wakaanza kunidodosa mambo yahusuyo elimu ya Tanzania, swali kubwa ambalo niliulizwa hivi elimu ya Tanzania ni ngumu sana, kuna tofauti gani kati ya elimu ya Tanzania na Rwanda au nchi nyingine za afrika mashariki.
Baada ya mazungumzo ya muda kidogo nilikuja kugundua chanzo cha maswali yote hayo ilikuwa kuna wanafunzi wapatao 35 kati ya 100 waliokuwa wanasoma Chuo kikuu wamefeli (Disco) na wanatakiwa kurudi Rwanda. Hao wanyarwanda wanasema hii ni mara ya kwanza kutokea kwao kwa kuwa wanafunzi hupelekwa sehemu mbalimbali afrika mashariki na sehemu nyingine lakini haijawahi kutokea wanafunzi wakafeli namna hii.
Kiukweli hawajasema direct kwamba kuna fitina imefanyika kwa wanafunzi wao lakini hisia zao zinaonyesha moja kwa moja kwamba wamehujumiwa. Ingawa walionyesha labda tatizo la lugha maana wanafunzi wengi wa Rwanda, elimu yao huipata kwa kifaransa na chinyarwanda lakini bado wanajiuliza kwa nini iwe mwaka huu na sio miaka mengine. Kwa sasa wizara ya elimu inawasubiri wanafunzi hao ili kuongea nao kujua chanzo cha wanafunzi wengi kufeli, kwa kuwa wanafunzi wote hao walikuwa wansomeshwa na serikali ya Rwanda.