macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Waambie Tz hatuna elimu ya
kuwafaulisha wote walioko darasani kama huko kwao,hapa kufeli kupo na
kama hawaamini waambie wafanye research kidogo kwa miaka kumi iliyopita
alafu jibu watapata wenyewe ...usikubali wakusumbue kwa vitu wanavyoweza
kutafiti na kujua historia ya kufeli ya chuo kama UDSM,kingine
wakumbushe hii siyo KIU&co. tunakoambiwa kufaulu bwerere na GPA za
matawi ya juu.
Mkuu, hao wanyarwanda
wapo sahihi kabisa. Kwanini!. Tanzania ni moja ya nchi (inaweza kushika
namba moja) ambayo rate ya kufeli wanafunzi wa vyuo vikuu ni kubwa
sana. Nimeenda Ulaya nimeenda Marekani nimeenda Asia. Kwangu mimi
sijaona wanafunzi wakifeli namna hii. Halafu cha ajabu ni kuwa
ma-graduate wa vyuo vikuu vya Tanzania sio bora kama wanaohitimu Ulaya
nk. Kunani? Bado elimu yetu imejikita kwenye kukariri kukariri kukariri
na kukariri. Ndio maana wengi wa wanafunzi wa vyuo hawaishi kuingia na
nyenzo kwenye mitihani!
Habari za jioni wanajamvi!
Leo hii nimekutana na tukio moja la kushangaza kidogo. Tulikuwa tunajadili mambo mbalimbali ya masomo na wanyarwanda ambao nasoma nao nje ya nchi. Baada ya mazungumzo mengi wakaanza kunidodosa mambo yahusuyo elimu ya Tanzania, swali kubwa ambalo niliulizwa hivi elimu ya Tanzania ni ngumu sana, kuna tofauti gani kati ya elimu ya Tanzania na Rwanda au nchi nyingine za afrika mashariki.
Baada ya mazungumzo ya muda kidogo nilikuja kugundua chanzo cha maswali yote hayo ilikuwa kuna wanafunzi wapatao 35 kati ya 100 waliokuwa wanasoma Chuo kikuu wamefeli (Disco) na wanatakiwa kurudi Rwanda. Hao wanyarwanda wanasema hii ni mara ya kwanza kutokea kwao kwa kuwa wanafunzi hupelekwa sehemu mbalimbali afrika mashariki na sehemu nyingine lakini haijawahi kutokea wanafunzi wakafeli namna hii.
Kiukweli hawajasema direct kwamba kuna fitina imefanyika kwa wanafunzi wao lakini hisia zao zinaonyesha moja kwa moja kwamba wamehujumiwa. Ingawa walionyesha labda tatizo la lugha maana wanafunzi wengi wa Rwanda, elimu yao huipata kwa kifaransa na chinyarwanda lakini bado wanajiuliza kwa nini iwe mwaka huu na sio miaka mengine. Kwa sasa wizara ya elimu inawasubiri wanafunzi hao ili kuongea nao kujua chanzo cha wanafunzi wengi kufeli, kwa kuwa wanafunzi wote hao walikuwa wansomeshwa na serikali ya Rwanda.
Elimu ya Udsm ngumu sana dah. Walimu wanacomplicate sana maisha.
tatizo lugha!
kwani umeambiwa wamesoma nchi wanayozungumza lugha gani?
Ni vilaza tu hao.Wamezoea elimu za kutafuniwa ndo maana wakija kwenye nondo's
wanadisco
acha uchochezi wewe. kwani umeambiwa hao wanafunzi wamesoma UDSM au Tanzania? mleta mada amesema nje ya nchi ingawa hajabainisha ni nchi gani wala chuo wanachosoma
hivi inakuwaje mnadisco wengine enzi zetu ata tusipofanya mtihan tunafauru
Ni wazi wanaweza dhani siasa zina mkono wake kutokana na hali ilivyo sasa, lakini kiuhalisia kuna mengi yanatakiwa yaangaliwe katika kufail kwao!
Wengi wameelezea utofauti wa lugha, hilo ni moja! Lingine ni system zinazotofautiana za elimu inaweza kuwa kikwazo. Tanzania tuna Advanced Sec. School baada ya O'level. Vipi kuhusu wao?? Hili linatofauti kubwa sana. Nina mfano mzuri wa vijana toka Msumbiji na DRC (wao hawana A'level). Light courses ambazo ni introductory wao wanasema kabisa zipo "above their level"!!!!
Katika lugha kuna ndugu zako Wacongo, wao wanaona bora Kiswahili kitumike kuliko English...It's funny na nashaka kama watakuwapo this AY
That is just natural akili hainunuliwi. unajua hao vijana si ajabu walikuwa na uwezo mdogo KAMA KAWAIDA YA VIONGOZI WA AFRIKA KUPENNDELEA WATOTO WAO. NAKUMBUKA KUNA MWAKA PROF. SARUNGI ALIWAHI KUKIRI KUWA ALIMPELEKA MTOTO WAKE ALIYEPATA DIV. IV F6 ULAYA MASHARIKI KUSOMEA UDAKATARI. MFANO HUU UNAWEZA KUWEPO HATA HUKO RWANDA, WATAWALA WAKAWAPELEKA WATOTO WAO BADALA YA WATOTO AMBAO NI VICHWA KTOKA FAMILIA MASKINI. HAYA YANATOKEA SANA AFRICA. KWAHIYO HIYO NI HAKI YAO KUFELI HASWABEBEKIHabari za jioni wanajamvi!
Leo hii nimekutana na tukio moja la kushangaza kidogo. Tulikuwa tunajadili mambo mbalimbali ya masomo na wanyarwanda ambao nasoma nao nje ya nchi. Baada ya mazungumzo mengi wakaanza kunidodosa mambo yahusuyo elimu ya Tanzania, swali kubwa ambalo niliulizwa hivi elimu ya Tanzania ni ngumu sana, kuna tofauti gani kati ya elimu ya Tanzania na Rwanda au nchi nyingine za afrika mashariki.
Baada ya mazungumzo ya muda kidogo nilikuja kugundua chanzo cha maswali yote hayo ilikuwa kuna wanafunzi wapatao 35 kati ya 100 waliokuwa wanasoma Chuo kikuu wamefeli (Disco) na wanatakiwa kurudi Rwanda. Hao wanyarwanda wanasema hii ni mara ya kwanza kutokea kwao kwa kuwa wanafunzi hupelekwa sehemu mbalimbali afrika mashariki na sehemu nyingine lakini haijawahi kutokea wanafunzi wakafeli namna hii.
Kiukweli hawajasema direct kwamba kuna fitina imefanyika kwa wanafunzi wao lakini hisia zao zinaonyesha moja kwa moja kwamba wamehujumiwa. Ingawa walionyesha labda tatizo la lugha maana wanafunzi wengi wa Rwanda, elimu yao huipata kwa kifaransa na chinyarwanda lakini bado wanajiuliza kwa nini iwe mwaka huu na sio miaka mengine. Kwa sasa wizara ya elimu inawasubiri wanafunzi hao ili kuongea nao kujua chanzo cha wanafunzi wengi kufeli, kwa kuwa wanafunzi wote hao walikuwa wansomeshwa na serikali ya Rwanda.
Mkuu mnafeli kwa vile hamfikii viwango kwenda Ulaya na Marekani si hoja hata sisi tumepita huko.Mkuu, hao wanyarwanda wapo sahihi kabisa. Kwanini!. Tanzania ni moja ya nchi (inaweza kushika namba moja) ambayo rate ya kufeli wanafunzi wa vyuo vikuu ni kubwa sana. Nimeenda Ulaya nimeenda Marekani nimeenda Asia. Kwangu mimi sijaona wanafunzi wakifeli namna hii. Halafu cha ajabu ni kuwa ma-graduate wa vyuo vikuu vya Tanzania sio bora kama wanaohitimu Ulaya nk. Kunani? Bado elimu yetu imejikita kwenye kukariri kukariri kukariri na kukariri. Ndio maana wengi wa wanafunzi wa vyuo hawaishi kuingia na nyenzo kwenye mitihani!