Hii ya wanafunzi wa Rwanda ni fitina au vilaza

Hii ya wanafunzi wa Rwanda ni fitina au vilaza

Mkuu, hao wanyarwanda wapo sahihi kabisa. Kwanini!. Tanzania ni moja ya nchi (inaweza kushika namba moja) ambayo rate ya kufeli wanafunzi wa vyuo vikuu ni kubwa sana. Nimeenda Ulaya nimeenda Marekani nimeenda Asia. Kwangu mimi sijaona wanafunzi wakifeli namna hii. Halafu cha ajabu ni kuwa ma-graduate wa vyuo vikuu vya Tanzania sio bora kama wanaohitimu Ulaya nk. Kunani? Bado elimu yetu imejikita kwenye kukariri kukariri kukariri na kukariri. Ndio maana wengi wa wanafunzi wa vyuo hawaishi kuingia na nyenzo kwenye mitihani!
 
Waambie Tz hatuna elimu ya
kuwafaulisha wote walioko darasani kama huko kwao,hapa kufeli kupo na
kama hawaamini waambie wafanye research kidogo kwa miaka kumi iliyopita
alafu jibu watapata wenyewe ...usikubali wakusumbue kwa vitu wanavyoweza
kutafiti na kujua historia ya kufeli ya chuo kama UDSM,kingine
wakumbushe hii siyo KIU&co. tunakoambiwa kufaulu bwerere na GPA za
matawi ya juu.

Ujumbe umefika mkuu, ingawa wao wanadai ni vipanga
 
Mkuu, hao wanyarwanda
wapo sahihi kabisa. Kwanini!. Tanzania ni moja ya nchi (inaweza kushika
namba moja) ambayo rate ya kufeli wanafunzi wa vyuo vikuu ni kubwa
sana. Nimeenda Ulaya nimeenda Marekani nimeenda Asia. Kwangu mimi
sijaona wanafunzi wakifeli namna hii. Halafu cha ajabu ni kuwa
ma-graduate wa vyuo vikuu vya Tanzania sio bora kama wanaohitimu Ulaya
nk. Kunani? Bado elimu yetu imejikita kwenye kukariri kukariri kukariri
na kukariri. Ndio maana wengi wa wanafunzi wa vyuo hawaishi kuingia na
nyenzo kwenye mitihani!

na hicho walichokuwa wanakiongea kwamba wao hawawezi kukremisha ila wanaelewa zaidi, ila kukrem na kuelewa kuna uhusiano mkubwa sn.
 
Ni wazi wanaweza dhani siasa zina mkono wake kutokana na hali ilivyo sasa, lakini kiuhalisia kuna mengi yanatakiwa yaangaliwe katika kufail kwao!
Wengi wameelezea utofauti wa lugha, hilo ni moja! Lingine ni system zinazotofautiana za elimu inaweza kuwa kikwazo. Tanzania tuna Advanced Sec. School baada ya O'level. Vipi kuhusu wao?? Hili linatofauti kubwa sana. Nina mfano mzuri wa vijana toka Msumbiji na DRC (wao hawana A'level). Light courses ambazo ni introductory wao wanasema kabisa zipo "above their level"!!!!
Katika lugha kuna ndugu zako Wacongo, wao wanaona bora Kiswahili kitumike kuliko English...It's funny na nashaka kama watakuwapo this AY
 
Elimu ya Udsm ngumu sana dah. Walimu wanacomplicate sana maisha.
 
Habari za jioni wanajamvi!

Leo hii nimekutana na tukio moja la kushangaza kidogo. Tulikuwa tunajadili mambo mbalimbali ya masomo na wanyarwanda ambao nasoma nao nje ya nchi. Baada ya mazungumzo mengi wakaanza kunidodosa mambo yahusuyo elimu ya Tanzania, swali kubwa ambalo niliulizwa hivi elimu ya Tanzania ni ngumu sana, kuna tofauti gani kati ya elimu ya Tanzania na Rwanda au nchi nyingine za afrika mashariki.

Baada ya mazungumzo ya muda kidogo nilikuja kugundua chanzo cha maswali yote hayo ilikuwa kuna wanafunzi wapatao 35 kati ya 100 waliokuwa wanasoma Chuo kikuu wamefeli (Disco) na wanatakiwa kurudi Rwanda. Hao wanyarwanda wanasema hii ni mara ya kwanza kutokea kwao kwa kuwa wanafunzi hupelekwa sehemu mbalimbali afrika mashariki na sehemu nyingine lakini haijawahi kutokea wanafunzi wakafeli namna hii.

Kiukweli hawajasema direct kwamba kuna fitina imefanyika kwa wanafunzi wao lakini hisia zao zinaonyesha moja kwa moja kwamba wamehujumiwa. Ingawa walionyesha labda tatizo la lugha maana wanafunzi wengi wa Rwanda, elimu yao huipata kwa kifaransa na chinyarwanda lakini bado wanajiuliza kwa nini iwe mwaka huu na sio miaka mengine. Kwa sasa wizara ya elimu inawasubiri wanafunzi hao ili kuongea nao kujua chanzo cha wanafunzi wengi kufeli, kwa kuwa wanafunzi wote hao walikuwa wansomeshwa na serikali ya Rwanda.

Please tuache ku-associate vitukio vinavyoweza kuleta uchochezi. Sisi wabongo tunaweza kuwavumilia wenzetu, taarifa hii isije ikapokelewa na RWANDA tofauti wakaamua kulipiza visasi ovyo! Tuwe makini na posts zetu.
 
Elimu ya Udsm ngumu sana dah. Walimu wanacomplicate sana maisha.

acha uchochezi wewe. kwani umeambiwa hao wanafunzi wamesoma UDSM au Tanzania? mleta mada amesema nje ya nchi ingawa hajabainisha ni nchi gani wala chuo wanachosoma
 
hivi inakuwaje mnadisco wengine enzi zetu ata tusipofanya mtihan tunafauru
 
acha uchochezi wewe. kwani umeambiwa hao wanafunzi wamesoma UDSM au Tanzania? mleta mada amesema nje ya nchi ingawa hajabainisha ni nchi gani wala chuo wanachosoma

Ndio wanafunzi hao ni wanyarwanda ambao wanasoma pale UDSM, kila mwaka Rwanda inaleta wanafunzi wao Tanzania kama vile Tanzania inavyopeleka wanafunzi wake pale Uganda Makerere.
 
Ni wazi wanaweza dhani siasa zina mkono wake kutokana na hali ilivyo sasa, lakini kiuhalisia kuna mengi yanatakiwa yaangaliwe katika kufail kwao!
Wengi wameelezea utofauti wa lugha, hilo ni moja! Lingine ni system zinazotofautiana za elimu inaweza kuwa kikwazo. Tanzania tuna Advanced Sec. School baada ya O'level. Vipi kuhusu wao?? Hili linatofauti kubwa sana. Nina mfano mzuri wa vijana toka Msumbiji na DRC (wao hawana A'level). Light courses ambazo ni introductory wao wanasema kabisa zipo "above their level"!!!!
Katika lugha kuna ndugu zako Wacongo, wao wanaona bora Kiswahili kitumike kuliko English...It's funny na nashaka kama watakuwapo this AY

System ya elimu ni kama ya kwetu tu sema wanatumia majina tofauti, o level wanaiita junior sekondari school na a level wanaiita senior sekondari school. Kikubwa ni lugha maana ni miaka ya karibuni nafikiri kuanzia mwaka 2009 wameanza kujifunza kwa kingereza kuanzia sekondari school. Ila kama unavyojua jinsi tunavyojifunza mfano watanzania tunafundishwa kwa kingereza lakini tukiwa kwenye discussion tunaongea lugha ya kiswahili na kwao ni hivyo hivyo wanjifunza kwa kingereza wakiwa kwenye discussion zao wanadiscuss kwa kinyarwanda au kifaransa.
 
Wakuu labda na mim nitoe mchango wangu hapo juu.binafsi mim ni mmoja wa watu ambao tupo nao course moja hao warwanda...ao warwanda wanaolalamika kudsco weng wao hawajitumi na wanajitenga.yani mkipangwa kweny group moja la practical ni mzigo kwa kweli.wengi wao nadirik kusema uwezo wao ni mdogo na course wanazotaka kusoma wao kiuhalisia ni ngumu.
Kwa mfano ukienda pale coet utawakuta,wengi wao wapo civil engineering na hyo ndo course inayoongoza kwa wanafunzi kufeli...na hilo swala la kufeli sio wao tu hata sisi wazawa tunafeli vile vile..
Kiufupi ni kwmba wengi wao hawajitumi labda na lugha pia kwa mbali inachangia....
 
Habari za jioni wanajamvi!

Leo hii nimekutana na tukio moja la kushangaza kidogo. Tulikuwa tunajadili mambo mbalimbali ya masomo na wanyarwanda ambao nasoma nao nje ya nchi. Baada ya mazungumzo mengi wakaanza kunidodosa mambo yahusuyo elimu ya Tanzania, swali kubwa ambalo niliulizwa hivi elimu ya Tanzania ni ngumu sana, kuna tofauti gani kati ya elimu ya Tanzania na Rwanda au nchi nyingine za afrika mashariki.

Baada ya mazungumzo ya muda kidogo nilikuja kugundua chanzo cha maswali yote hayo ilikuwa kuna wanafunzi wapatao 35 kati ya 100 waliokuwa wanasoma Chuo kikuu wamefeli (Disco) na wanatakiwa kurudi Rwanda. Hao wanyarwanda wanasema hii ni mara ya kwanza kutokea kwao kwa kuwa wanafunzi hupelekwa sehemu mbalimbali afrika mashariki na sehemu nyingine lakini haijawahi kutokea wanafunzi wakafeli namna hii.

Kiukweli hawajasema direct kwamba kuna fitina imefanyika kwa wanafunzi wao lakini hisia zao zinaonyesha moja kwa moja kwamba wamehujumiwa. Ingawa walionyesha labda tatizo la lugha maana wanafunzi wengi wa Rwanda, elimu yao huipata kwa kifaransa na chinyarwanda lakini bado wanajiuliza kwa nini iwe mwaka huu na sio miaka mengine. Kwa sasa wizara ya elimu inawasubiri wanafunzi hao ili kuongea nao kujua chanzo cha wanafunzi wengi kufeli, kwa kuwa wanafunzi wote hao walikuwa wansomeshwa na serikali ya Rwanda.
That is just natural akili hainunuliwi. unajua hao vijana si ajabu walikuwa na uwezo mdogo KAMA KAWAIDA YA VIONGOZI WA AFRIKA KUPENNDELEA WATOTO WAO. NAKUMBUKA KUNA MWAKA PROF. SARUNGI ALIWAHI KUKIRI KUWA ALIMPELEKA MTOTO WAKE ALIYEPATA DIV. IV F6 ULAYA MASHARIKI KUSOMEA UDAKATARI. MFANO HUU UNAWEZA KUWEPO HATA HUKO RWANDA, WATAWALA WAKAWAPELEKA WATOTO WAO BADALA YA WATOTO AMBAO NI VICHWA KTOKA FAMILIA MASKINI. HAYA YANATOKEA SANA AFRICA. KWAHIYO HIYO NI HAKI YAO KUFELI HASWABEBEKI
 
Mkuu, hao wanyarwanda wapo sahihi kabisa. Kwanini!. Tanzania ni moja ya nchi (inaweza kushika namba moja) ambayo rate ya kufeli wanafunzi wa vyuo vikuu ni kubwa sana. Nimeenda Ulaya nimeenda Marekani nimeenda Asia. Kwangu mimi sijaona wanafunzi wakifeli namna hii. Halafu cha ajabu ni kuwa ma-graduate wa vyuo vikuu vya Tanzania sio bora kama wanaohitimu Ulaya nk. Kunani? Bado elimu yetu imejikita kwenye kukariri kukariri kukariri na kukariri. Ndio maana wengi wa wanafunzi wa vyuo hawaishi kuingia na nyenzo kwenye mitihani!
Mkuu mnafeli kwa vile hamfikii viwango kwenda Ulaya na Marekani si hoja hata sisi tumepita huko.

Ulaya na Marekani ukienda vyuo vya ovyo ovyo utapasi tu lakini unarudi mbumbumbu.

Viwango vilivyoachwa na wajerumani wakati huo FoE sasa CoeT ni vya elimu ya uhandisi vya kimataifa.

Disco zilikuwepo, zipo na zitendelea kuwepo mwanafunzi asipofikia viwango.
 
Back
Top Bottom