Hii Yanga ya Zahera imeanza kunipa wasiwasi

....kingine yule beki namba mbili (Mustafa) alikuwa anachelewesha mashambulizi kwa tabia yake ya kurudisha mipira nyuma...
Kama sijakosea.. Mustafa ni beki wa kati ila anacheza pembeni kama mbadala tu wa Boxer
Kama Juma Abdul yuko fit sioni sababu ya kukaa benchi na kucheza mtu ambae ni mzito kusukuma timu mbele.
X100 ampange yule dogo rasta ni mwepesi sana
 
Kuna umuimu wakupata beki namba mbili mbadala wa Gadiel uyu Ally Mtoni awezi kabisa ziba pengo la Gadiel.
 
Kama sijakosea.. Mustafa ni beki wa kati ila anacheza pembeni kama mbadala tu wa Boxer
Kama Juma Abdul yuko fit sioni sababu ya kukaa benchi na kucheza mtu ambae ni mzito kusukuma timu mbele.
X100 ampange yule dogo rasta ni mwepesi sana

sawa kabisa...mimi binafsi ni mshabiki wa Zahera na napenda aendelee kuifundisha Yanga...ilanaomba asaidiwe kwa ushauri...haikuwa sahihi kwa Yanga kuanza na wacchezaji watatu tu wa msimu uliopita....ni kosa kubwa ambalo limei-cost Yanga....lile goli limefungwa kizembe sana...kulikuwa hakuna covering defender baada ya Yondani kupitwa...na halafu Shikalo alitoka mapema...ningekuwa mimi ni kocha jana kikosi changu kingekuwa kama ifuatavyo: Shikalo, Boxer/Juma Abdul, Sonso, Yondani, Moro, Tshishimbi, Balama, Feisal, Molinga/Balinya, Raphael Daudi/Ngasa, Sibomana.
 
Sawa mkuu, wageni waliopo ni wa kawaida sana.tunataka wawe ni viwango vya juu ya wazawa.
Kwa vipi sasa? Timu imesajili ilivyoweza, pia muda utaongea. Hata kwa Chirwa ilikuwa hivi hivi, baadaye mkabadilika. Nashauri tuwape robo ya kwanza ya mzunguko mpaka dirisha dogo tutakuwa tumejua mbivu na mbichi. Malalamiko ya wakati huu hayaleti afya kwa klabu wala hayatendi haki. Uwezo wa Mwinyi sote tunaujua, isipokuwa baadhi ya mashabiki mmeanza kucheza mziki wa mikia, wakiponda mnaunga bendi bila kutafakari. Muda ni jibu la kila jambo, tusiwe kikwazo kwa timu yetu wenyewe, tuwe wenye hekima.
 
Huyu zahera bana !!!! haeleweki anachezesha mfumo gani yeye kila siku ni kulalamika tuu timu inaposhindwa na aikshinda kwa ugumu kagoli cha kuanzia dakika ya 70 utasikia anasema " SISI TULIWAACHIA POSENSIO" sasa POSENSIO kila siku mpaka lini ni lini timu itacheza kwa hari na uchu wa magoli mengi ili kuwaponyesha mashabiki kutokana na hiyo formula yake ya possensioo?
 
Nilidhani mnajua kuwa msimu huu ndiotunajenga timu baada ya kuwaacha baadhi ya wachezaji kufuatia viwango vyao. Tuwe wakweli, Tambwe alishafika mwisho kwa umri ule. Makambo mpira ni biashara pia, timu haikuwa na fedha kipindi anauzwa. Kamusoko pia tayari pancha za uzeeni zishaanza. Timu ilihitaji vijana wenye kasi. Tatizo tunasahau upesi mno, mnataka kushinda tu, kwa timu gano hasa mliyokuwa nayo msimu uliopita? Ajibu hakuachwa, aliwapiga chenga viongozi akapewa mkataba wa awali na mikia. Swali kwenu enyi walalamikaji, mlikuwa na pesa ya kumwongezea mkataba Ajibu kabla haujaisha? Vipi kwa Gadiel ilikuwaje kwani?

Nawasihitusiwe wajuaji wengi, tutavuruga timu kwa kusikiliza maneno ya mbumbumbu fc. Zahera tunamjua tangu msimu uliopita, no ujinga kumtilia shaka kwa mechi za awali kwenye timu changa. Huo sio mpira hata kidogo, ni ushabiki wa vijiweni.
 
Umetisha mkuu, ndio kwanza mwanzo huu.
 
Wana Yanga wanatoa maoni yao kuhusu timu yao... We hutaki
 
Kwani kocha anapanga timu kwa kuangalia vigezo gani? Pia unaweza kutuambia hali ya wachezaji na perfomanceyao kwenye mazoezi? Kupanga kikosi huk umtaani kila mtu anaweza, lakini kwanza tupate majibu hayo
 
Wana Yanga wanatoa maoni yao kuhusu timu yao... We hutaki
Kuna tofauti kati ya lawama na maoni. Ona mdau aliyetoa maoni hapo juu 3llyEmma: kwa kuchambua mechi za awali. Hayo ni maoni, lakini mtu anayembeza kocha na wachezaji hatoi maoni. Pia unalalamika kwa mechi moja tu,unajua mpira? Unasema timu ni mpya halafu unalalamika, unasema timu iliachawachezaji wakati mpaka msimu unaisha timu ina madeni tupu, huoni haya si maoni tena bali ni mtazamo hasi? Tunasahau tulipotoka
 

Mmmmh ok...nilidhani kuwa tunatoa maoni ya kujenga kwa ajili ya timu kumbe wengine mnaona ni ushabiki wa mmnachoita vijiweni...kwa hiyo wote tuwe na mawazo yanayofanana kwa ajili ya timu...kwa hiyo maoni yako tofauti na mimi (sisi) siyo ya kijiweni ila sisi ndiyo ya kijiweni...wewe ndiye unayejua lililo jema na baya kwa timu ..very interesting...unaweza ukawa na hoja lakini uwasilsishaji wako wa hoja ulioambatana na dharau na kejeli kwa wengine wenye mawazo tofauti na wewe una walakini sana...anyway niishie hapa maana mwelekeo wake nadhani itakuwa ni kurushiwa matusi....sioni hata na haja kuendelea kutoa maelezo ya kilicho nyuma ya sualala Ajib, Gadiel, Tambwe na Makambo...
 
Mmh mkuu, labda nalo neno.
 
Safi sana kwa analysis yako murua. Vizuri kuwaza kivingine pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…