Hiki Kingereza cha Wasanii wetu kwenye Instagram accounts zao ni cha wapi?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Wakuu, mi nauliza tu!

Hawa ni mastaa wetu, ‘vioo’ vya jamii. Basi wengi wao hupenda ku-name akaunti zao ‘official’.

Yaani kila msanii ana prefix- au suffix- official, hata wale uchwara atajiita ‘officialuchwara’ au ‘utopoloofficial’.

Napata tabu huenda mimi sielewi, na wala siioni huko kwa mabeberu tunakojifunza. Wajuvi nijuzeni, nami nipate kujua.

Nini maana ya kuwa ‘official’ kwenye hizi kurasa zetu?

Asanteni.
 
Wabongo wanapenda kufungua akaunti kwa kutumia majina yao...parody kibao. Wakaona kuweka neno official ndio dawa.
 
Kwa wasanii wakubwa let's say Nasibu Abdul (diamond) , Juma Jux na wengineo ukiingia Kwenye mitandao kama IG, FB n.k utakutana na Accounts nyingi zenye majina hayo ambazo nyingi ni "fan pages" ndio maana wakaamua kuweka official ili kutofautisha ama kuonyesha kuwa hizo ni rasmi.

kidogo utakuwa umepata mwanga sio?
 
Mbona diamond anatumia diamond platinumz na sio official...?
 
Hata Giroud na Lacazatte wanatumia ile ya kifaransa officiele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…