Hiki kipindi kimetisha sana

Hiki kipindi kimetisha sana

Habari zenu wandugu,
Wakati nasubiri chai leo home nikasema nisikilize radio,nikaweka Choice FM,basi nikasikia kuna session inaitwa mahabara ya mapenzi,yaani unawatumia message kwenye kipindi kuwa unataka kupimiwa mapenzi yako nao wanakupigia simu wanakuuliza maswali.
Ilikuwa kama hivi;
Mtangazaji:hello?
Mpimiwa mapenzi:hello
Mtangazaji:Naongea na VERO?
Mpimiwa mapenzi:Ndiyo
Mtangazaji:Umetuma message kuomba maabara ya mapenzi ikupimie mapenzi yako si ndiyo.
Mpimiwa mapenzi:Ndiyo
Mtangazaji:Mpenzi wako anaitwa nani?
Mpimiwa:Anaitwa Mika.
Mtangazaji:Anaishi wapi Mika.
Mpimiwa:Anaishi Tegeta.
Mtangazaji:Anafanya kazi gani?
Mpimiwa:anafanya kazi TANESCO.
Mtangazaji:Mahusiano yenu yana muda gani.
Mpimiwa :Yana kama miezi MITATU hivi au MINNE.
Mtangazaji:Mna mtoto na bwana Mika?
Mpimiwa:Hapana.

Mtangazaji:Kwanini unataka kupimiwa mapenzi,humuamini mpenzi wako au unadhani kuwa hakupendi,au ana mtu mwingne?
Mpimiwa:Hapana nataka kujua ananipenda kiasi gani.
Mtangazaji:Sawa subiri kidogo usikikie majibu kutoka kwa Mika.

Basi bwana Mika wa Tegeta kapigiwa simu (nadhani mpenzi mpimiwaji alitoa namba ya Mika kwa Mtangazaji back stage) Mambo yakawa hivi.

Mtangazaji:Halooo naongea na Mika?
Mika:Ndiyo.
Mtangazaji:Napiga simu kutoka kampuni ya blaaa blaaa blaaa,nimepewa namba na mtu anayedai mna mahusiano naye,amenambia umewahi fanya kazi shirika la umeme ni kweli?
Mika:Ndiyo ndiyo.
Mtangazaji:Kwa sasa unafanya kazi wapi.
Mika:aaaaah kwa sasa nafanya kazi hizo hizo ila nafanya mtaani zaidi,baada ya muda wangu kuisha TANESCO.
Mtangazaji:Ok basi kampuni yetu inatafuta mtu wa kufanya kazi za umeme,sijui upo tayari.
Mika (huku akitabasamu):Ndiyo nipo tayari.
Mtangazaji😱k una familia,yaani mke,mchumba au mtoto?
Mika:nina MCHUMBA na MTOTO.
Mtangazaji:una muda gani na mchumba wako?
Mika:Kama MIAKA MITATU hivi.
Mtangazaji: anaitwa nani mchumba wako.
Mika:anaitwa PENDO.
Mtangazaji:Sawa ngoja niongee na wenzangu halafu nitakupigia ili nikupe taarifa zaidi.
Mika: sawa nashukuru.
Mtangazaji wa kiume Mbeaa:basi dadaangu Vero naamini umemsikia Mika kwa maskio yako mwenyewe.......
Nadhani Vero atakua alizimia,akasindikizwa na kibao kinaitwa I'm cheating on you.
JAMANI HUU NI UUNGWANA KWELI?
YAANI TUMEANZA KUUMBUANA MCHANA KWEUPE?
NDUGU WATANGAZAJI,HATA KAMA NI UBUNIFU WA VIPINDI,MTAKUJA KUTUUA KWA UBANIFU WENU SIKU MOJA.
Sasa mnadhani Mika atajibu nini Kwa VERO na PENDO leo?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hatariii
 
Kuna watu wapumbavu sana,yaani mtu anakupigia simu kisha anakuuliza maswali yasiyo ya msingi na wewe unatiririka tu kisa umesikia habari za kazi,kusema una mke na mtoto inatosha ila mara anaitwa nani sijui bla bla ni upuuzi.
 
Back
Top Bottom