Hiki kisa cha huyu mwanaume aliyetembea na shemeji yake kimenifunza.

Hiki kisa cha huyu mwanaume aliyetembea na shemeji yake kimenifunza.

Write your reply...
Aendelee kumla tu kwan shida iko wapi kama jamaa anajua toka way back kua mke ana mpenda b
 
Jana katika leo tena nimesikia kisa cha kusikitisha kiko hivi,
Kuna jamaa marafiki sana toka chuo wanasoma wote marafiki kiasi kwamba hadi wamekuwa kama ndugu na familia zao zimekuwa kitu kimoja.
Walipomaliza chuo wakapanga sehemu moja. A akafanikiwa kupata kazi nzuri kuliko B, akatangulia kununua gari kabla ya B na kumsaidia B kumpush naye apate usafiri.
Wakanunua eneo kwa pamoja mlandizi na kujenga nyumba kila mtu yake ambazo zimetenganishwa kwa ukuta.
A kaoa B ana mchumba lakini wanakuwa wana hang out kila sehemu pamoja. Sasa kwa maelezo ya B siku moja A kasafiri, yeye na shemeji yake wakatoka na kurudi usiku eti shetani akawapitia akamtafuna shemeji na usingizi ukawapatia wakalala, wanashtuka asubuhi A anaingia chumbani kumbe alirudi kimya kimya. A anawambia samahani mke wangu ela ya matumizi ya leo naweka mezani akaweka 20,000 halafu akatoka akaenda kazini.
B akatoka ndani akakimbilia kwake akijua jioni jamaa akirudi itakuwa mgogoro mkubwa sana lakini ajabu jamaa alirudi hajaongelea hilo swala akawa anacheka na anaonyesha kumjali na kumpenda mkewe kama kawaida.
Hapo hapo namwita mshikaji wale na kuchill kama kawaida. B akawa anatamani jamaa aseme neno jamaa hasemi neno hiyo hali ikawa inamtesa akaamua aende kujishtaki kwa mjumbe na kumueleza kisa chote. Mjumbe akamwita A na kumwambia kilichotokea, A akabisha kuwa yeye hajamfumania rafiki yake na mkewe na kama angemfumani na kungekuwa na tatizo wangelimaliza mbona maana yule ni zaidi ya ndugu kwake. kisha akatoka na kumfuata rafiki yake na kumwambia mbona umemwambia mjumbe mambo ya ajabu mimi sina tatizo na wewe.
Jamaa akazidi mshangaa A jinsi alivyokuwa ana behave yani kama hakuna kilichotokea. Siku ya Fiesta akawambia waende Fiesta dar jamaa anadai alikubari maana alikuwa anamuogopa A anashindwa mkatalia wakaenda pamoja na shemeji aliyemtafuna. Anasema yani ile show nzima hakuwa na raha hata kidogo.
Jamaa akaona hapa huyu jamaa au anapanga kuniua ikabidi aende BAKWATA aeleze kisa chote, Masheikh wakamuita A nako akakana kuwa hajawafumania. B akazidi changanyikiwa siku ya mwaka mpya pia akawatoa akaenda nao Bagamoyo anaonyesha ana furaha zote tu.
B anadai kazi hazaiendi chakula hakishuki anazidi kukonda, akaona bora amwambie dadake A hapo ilikuwa imepita week 3, dadake mshikaji akaongea na babake A. So kikaitishwa kikao cha familia, bado A akabisha kuwa yeye hajawafumania. B akampigia magoti asemehewe amemkosea jamaa msimamo wake ni kwamba hajamkosea na wala hajawafumania wala hakumbuki kitu ka hicho.
Jamaa kuona hivyo ikabidi akatoe taarifa polisi wakampa na RB kabisa kisha akamtafuta Gea Habibu ili watu wampe ushauri maana anasema jamaa anawatesa Kisaikolojia walau aseme chochote.
Sasa a alipohojiwa na Gea anadai kwamba yeye alikuwa ashamuona mkewe kuwa anampenda rafiki yake na alikuwa ashahisi kuna jambo linaendela. So hata siku ile ni sawa aliwatega kuwa kasafiri. Ila anadai kwamba yeye hana tatizo na rafiki yake anasema amuombe mungu tu amsamehe yeye hana tatizo na wala hapangi kumfanyia ubaya wowote.
Na akadai jana aliposikia redioni akajua ni rafiki yake na akadai rafiki yake ana mchumba mwaka huu anaoa. Mchumba wa rafiki yake alipojua akataka vunja mahusiano ila yeye mwenyewe jana kawakutanisha B na mchumba wake kawaweka sawa.
Aisee kuna watu wana mioyo aisee jamaa ana moyo ila sidhani kama everything gonna be the same again.
Mara A mara B mara Gea!!

NB: Hiyo inaitwa adhabu ya kisaikolojia. Ni mbaya mno!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu B snitch..sio rafiki wa kweli...nahic jamaa hataki agombane na B kisa mwanamke ndo maana kawa kimya...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa mkuu kwa urafiki wao angemkataa na siku walipofumaniwa japo B anasema ilikuwa ndo mara ya kwanza itakuwa walikuwa wanakulana siyo mara ya kwanza
 
Ila A cyo muongeaji kabisaaa ,mpole adi nimempenda buree
Nimemsikia wakati anaongea na Gea nikama hataki ata kuongelea iyo ishu ,yuko poa tu
alafu inaelekea anampenda sana rafiki ake
 
Adi mauki kaingilia kati usifanye mchezo na physiological tougher ila wanaume mkomage na nyie mjifunze kukaa mbali na shemeji zenu mtaja kufa mdomo wazi kisa k japo mwanamke ndo alie muwekea mazingira ya kumtafuna
 
Kipindi nafanya kazi za kuajiriwa kuna mtu alinifanyia majungu nikafukuzwa kazi.

Wala sikujua kama ni yeye ila baada ya kutoka pale niliendelea kumpa support ya kazi ukizingatia Mimi ndiye niliyempokea na kumfundisha kazi.

So siku moja ananipigia ananiambia nasikia unanitangazia kuwa Mimi ndiye niliyekufukuzisha kazi. Nikashangaa sana kwanza sijawahi kuhisi baadae nikapeleleza ndio nikajua kuwa kumbe ni kweli yeye ndiye aliyepeleka zile taarifa kwa wakuu wa department.

Nikajua kuwa kumbe psychologically alikuwa anaumia kwa sababu Mimi nilikuwa nampa ushirikiano kama kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila A cyo muongeaji kabisaaa ,mpole adi nimempenda buree
Nimemsikia wakati anaongea na Gea nikama hataki ata kuongelea iyo ishu ,yuko poa tu
alafu inaelekea anampenda sana rafiki ake
Umenipenda kweli? Au ukishajua mimi ndio A hutataka hata nije pm
 
Mfano halisi wa mwanaume wa Dar ni huo hapo
 
Back
Top Bottom