Hiki kitanda kinaweza kutengenezwa hapa Tanzania?

Nimepigwa hahaa

Mzee kama unazungumzia vya kutengenezwa hapa sawa lakini sio cha ubora huo, unaweza kuwa hujui vitu vilivyo kwenye hicho kitanda kikiwa complete
 
Kwa hiyo laki nne, mbao aina gani itatumika,ngozi au pvc ya ubora gani na bei gani kwa meter? Mfumo wa umeme na radio etc gharama zikoje?
 
Nimepigwa hahaa

Mzee kama unazungumzia vya kutengenezwa hapa sawa lakini sio cha ubora huo, unaweza hujui vitu vilivyo kwenye hicho kitanda kikiwa complete
Mfano hicho picha kachukua alliexpress kama si alibaba. Ukinunua kwenye maduka yenu ya kishua kufidia gharama kubwa ya shipping lazima ifike hiyo hela uliyotaja.

Hapo sana sana kuna soft wood. Mdf, pvc.(ambazo nyie mnaziita lether) Usb extension na godoro nyembamba.

Ingia keko hapo watu wanatoa vitu vikali tu. Mafundi siku hizi YouTube zipo kila kitu kiko wazi wanajifunza vitu vipya.
 
Made in Tanzania.. kinatengenezwa tatzo watz na kasumba ya kupenda vya nje
 
Wewe hujui vitanda. Kitanda cha laki 4 ni mbao tupu, sofa bed zenyewe ndio zinachezea hapo. Hiki kitanda ukinunua chini ya 2M basi ungeachana nacho tu.
 
Wewe hujui vitanda. Kitanda cha laki 4 ni mbao tupu, sofa bed zenyewe ndio zinachezea hapo. Hiki kitanda ukinunua chini ya 2M basi ungeachana nacho tu.
Sijasema bei ya kuuza mkuuβ˜οΈπŸ˜€. Nimesema gharama ya material kwa mtengenezaji. Kwa fundi wa keko hapo lak 8 - 1.2 unachukua vinginevyo amekuchapa ukija vibaya.

Ila ukitaka vya kutoka nje hata hiyo mil 2 ni ndogo.
 
ngoja nijipange,nataka kuoa mke alale pazuri mtoto wa watu;
nampenda sana huyu mwanamke wangu 😁😁😁😁;
 
Kinaweza kutengenezwa sema wanunuaji ndio itakuwa shida...
 
My wife to be financial services njoo uone mambo huku. Kama vipi tujichange tununue hiki kitanda. Kile cha elfu 70 cha Shamba boy kitatusababishia tu ulemavu wa migongo tutakapo zeeka.
Jamani Hubby, hiki ni kizuri mno na i can imagine kitakachokua kinaendelea kila muda tukitumia hicho kitanda haina kuchokaa na kinaongeza sweetness hikiπŸ˜€πŸ˜€. Ila kama kile cha 70,000 hadi leo hii umesave 15,000 tu hicho si tutasave milele na isifikeπŸ˜€πŸ˜€
 
Kwa mtanzania hakuna kinachoshindikana
 
Hata ndege mbona nasikia kuna mzee anaunda?
Achana na mzee. Tuna kiwanda cha kuuza ndege au magari au hata pikipiki? Manake kitu chenye engine kinatengenezwa halafu kiuzwe na kiingizie mtu au kampuni? Hichi kitanda kinatengezwa na kinaingizia mtu hela. Achana na story za mitandaoni au za mtu kama yule dogo wa Bukoba alitengeneza kapikipiki kadogo kenye engine. Akaishia tu juu juu. Akili tunazo. Uwezo tunao. Lakini hayo mambo yanahitaji uwekezaji wa hela mkubwa. Kwa hio hata huyo wa ndege hakuishia popote. Alijaribu, akashindwa kuendeleza fani imwingizie $$$.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…