Hiki kitukimeniuma, japo ni kidogo! Jirani kaomba unga wa Sembe kaenda kufulia viatu

Issue sio unga ishu ni chakula. Hata kama ingekuwa punje moja ya haragwe

Push to Start
Mkuu kama alikuomba kwa ajili ya kupikia Sawa ila kama ukupewa sababu ya kuombwa unga na wewe ukatoa bila kumuliza anakoupeleka mm sijaona kosa maana ata mm natumiaga kung'arisha viatu na vinang'aa vizuri tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeumia sana mkuu

Push to Start
Ila baada ya kugundua kwamba unga uliompa aliutumia kwa kusafishia viatu muda huo huo kama ungemwambia huyo jirani yako kwa upole tu kwamba hukujua kama unga alioomba ulikuwa ni wa kusafishia viatu na ukamsikia jibu lake usingeteseka kiasi hiki. Maana kwa jinsi unavyoonekana baada ya kuamua kuanzisha uzi huu hapa leo utateseka sana siku nzima kwa sababu utalazimika kuwa unauchungulia kila mara kuona wadau wanasemaje kuhusu hii hoja yako. Sasa hayo si mateso jamani wakati ungeweza kuyaepuka kwa kutumia hiyo njia mbadala na pia kwa kuzingatia kwamba ulikuwa umetoka kanisani?
 
Viatu vyeupe vya kitambaa kama cha jeans huwa vinaoshwa na unga. Lakini naww ukishampa mtu kitu kwann utake kumpangia matumizi kama ulitoa kwa moyo mmoja basi haina haja ya kulalamika
 
Mkuu kama alikuomba kwa ajili ya kupikia Sawa ila kama ukupewa sababu ya kuombwa unga na wewe ukatoa bila kumuliza anakoupeleka mm sijaona kosa maana ata mm natumiaga kung'arisha viatu na vinang'aa vizuri tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa angekuwa wa ajabu kama angedanganya matumizi ya huo unga. Lakini hawakuwa na makubaliano yoyote ya matumizi.
 
Kuna miaka fulani vile viatu tulikua tuna viita mbwaa,vina manyoya ivi,vilikua vinauzwa kwenye maduka ya bora..na vilitoka kenya,wahenga watanitetea kwa hili, ilikua ni fasheni ukashivifua unapaka unga vikikauka unafuta ule unga na brush...af kama una petrol unavipaka..na mara nyingi hii shughuli hufanyika jmos kwa ajili ya kanisani j2,au j2 kwa ajili ya kazini au chuoni j3...na lazima ukute marafiki zaidi ya wawili chuoni,kitaa au kazini wana mbwa zao,wamezivaa na wakihadithiana jinsi ya kuvitunza ikiwemo uoshaji huo mkuu,na mtu anaweza akawa na pear hata mbili za aina moja na mara nyingi vilikua vya khaki,kwa hiyo msamehe buree[emoji28]Mwisho kabisa unaweza ukachagua rafiki lakini sio jirani...

Sent using by using Nokia ya tochi
 
Sio naongea kiushabiki ila kiukweli unga sio chakula juu hauwezi kuula mkavu! So sijaona kosa la jamaa hapo angekuwa amekuomba ugali hapo sawa ila kwa unga sioni kosa mbona ngano inatengenezewa pombe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimaliza kufua viatu kabla ya kuvianika unapaka unga kwa juu, ndipo unaanika, hii inasaidia kuzuia viatu kuwa na ramani au kufubaa vikikauka,,
Na hii haijalishi kama rangi ya viatu ni kahawia, nyeusi, blue n.k. utatumia tu huo unga ambao wenyewe kwa rangi ni mweupe?
 
Umeshindwa kwenda kumueleza huko? Siyo kila kitu ni cha kuandika
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…