Vimekuwepo vingi kuanzia January mpaka tunapokaribia kuumaliza mwaka 2023
Vilikuwepo vya kufurahisha
Vilikuwepo vya kushangaza
Vilikuwepo vya kuchanganya
Vilikuwepo vya kuhuzunisha
Vilikuwepo vya kuumiza nknk
Najua ni vingi na kuna kimoja ama viwili utakuwa unavikumbuka.. Please share..[emoji23]
Changu ni hiki hapa
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Ruvuma linawasaka popote walipo mhandisi wa Wilaya ya Halmashauri ya Mbinga Mji pamoja na daktari aliyehusika kuweka plasta ngumu (POP) kwenye mkono wa mhandisi huyo, kuonesha kwamba anaumwa ili kukwepa tuhuma za ubadhirifu wa fedha pamoja na wizi wa vifaa vya shule.