una uhakika gani kama anamtega, we are too judgemental kwama anamtega, what if atamrudishia pesa yake, Michael mwenyewe anasema siku bado hazijesha, na pia hana hiyana kufanya ya 'kumsaidia' dada mwenye duka isipokuwa anaogopea fedha zake.
Ndugu Michael ni mwoga, tena ni mwanaume mwenye kuendekeza umbea, na zaidi ya yote ni mbahili na anapenda vya bure.
Kwanza utamkopeshaje mke wa mtu pesa bila mumewe kujua? kiasi cha mwenye mke kutambua kuwa Michael alimkopesha bint pesa ni vurumai tosha achia mbali ku do nae.
Pili ndugu Michael ameshasema dada mwenye duka ni kifaa kinachoita, ina maana ameshamwanagalia kwa jicho la tatu na la nne na mimacho imeshaanza kumtoka kabla hata hayakopwa. Alijilengesha dada akamshtukia na akachukua hatua moja mbele ya kutafuta ukaribu kwa njia ya deni. Mteja akaingia line, dada akaona yes,, mambo iko huku akajilipua kwa kumwaga shida yake.
Hebu fikiria, ameshawaambia washkaji kuhusu huyu demu, halafu akauleta uzi huu duniani ili tumpe hongera kwa kukopesha mke wa mtu au kutamaniwa na mke wa mtu? Huu ni umbea kama si nataka sitaki.
Michael aseme anamtaka dada au hamtaki, hizo longo longo nyingine ni za kitoto.