Hiki ndio kipimo cha Uswahili. Jipime, je wewe ni Mswahili?

Hiki ndio kipimo cha Uswahili. Jipime, je wewe ni Mswahili?

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
TAFSIRI YA MANENO YANAYOTOKA NA “KISWAHILI” KWA MUJIBU WA WASWAHILI WENYEWE.

“Saa ya Kiswahili”: Saa isiyozingatia muda wa miadi (ni kinyume cha, “saa ya kizungu” ambayo humaanisha, “Juu ya alama”)


“Uswahili”: Tabia ya ubabaishaji, iliyopungukiwa weledi na ustaarabu!


“Uswahilini (au uswazi)”: Kwenye makazi holela na mpangilio hafifu, chochoro nyingi na msongamano watu.


“Mtu mswahili”: Mtu asiyeaminika, mjanja-mjanja asiye na mipango.
“Ahadi ya Kiswahili”: Ahadi hewa!


“Kupigwa Kiswahili”: kupigwa chenga kwa kutumia maneno matupu!


“Kiswahili kingi”: Porojo tupu zisizo na mashiko!
 
Back
Top Bottom