Hiki ni kielelezo cha jamii yetu ya Kitanzania, tabia na hulka zetu

Hiki ni kielelezo cha jamii yetu ya Kitanzania, tabia na hulka zetu

Wasalaam,

Niseme nimesikitishwa mno, tena kupita maelezo, mtu tuliyekuwa tunaheshimiana sanaa, tunaitana "wakuu", kila tunapokutana kwenye nyuzi hapa JF, "mkuu" ni nyingi, mkuu wangu akanipa mchongo wa kuwekeza mahali fulani huku akijinasibu kuwa yeye anakula mafao (millions) ya uwekezaji wake huku akinihusia na mimi niwekeze huko, "mkuu" tukabadilishana mawasiliano na kuanza kunimentor kwa ajili ya uwekezaji.

Mkuu akani-inspire sanaa cha kushangaza jana napita mitaa fulani humu JF namkuta mkuu kajawa na jazba kwa kukosa vocha ya bure zilizokuwa zikigaiwa huko kwenye huo uzi, mkuu anatokwa na maneno ya kulaani kabisa kwa kukosa vocha ya bure, niseme nimesikitishwa sana na wewe "mkuu", hivi najiuliza hata zile nondo za uwekezaji ulizokuwa unanipa ni za kweli mkuu?

Watanzania ni watu waongo waongo mno, kuanzia viongozi mpaka raia wake, sisi ni watu njaa njaaa sanaa kuanzia raia wa kawaida mpaka viongozi waandamizi na ndio maana watu wananunuliwa na kuhongwa kwenye chaguzi, viongozi wanasaliti na kuhama vyama vyao kwa ajili ya maslahi ya tumbo, masikini hazaminiki.

Na huu ndio uhalisia wa jamii zetu tunazoishi nazo huku mitaani.
Nisiwachoshe "wakuu"

Wasalaam,

Mla Bata.
Umesomeka MJIVUNI.
 
Tunaenda wapi kama taifa, tunadhalilika hivi kisa vocha, tukiletewa kilo moja moja za mchele na maharage kipindi cha kampeni tutaweza kukataa kweli?

Ebu tuseme na shida zetu basi.
 
Tunaenda wapi kama taifa, tunadhalilika hivi kisa vocha, tukiletewa kilo moja moja za mchele na maharage kipindi cha kampeni tutaweza kukataa kweli?

Ebu tuseme na shida zetu basi.
Mkuu umenikumbisha sadaka za mchele na nyama kwenye taasisi Fulani hivi aisee ufisadi hautakuja kuisha kamwe wakubwa Wana hungry fire
 
Mungu atulindie matajiri na donors wetu wote wa JF kwa kurudisha kwa jamii #bringsbacktocommunity
 
Mkuu mbona hii issue ya VOCHA mmeichukulia too personal sometimes mgetoa pongezi inge -make sense Sana kuliko hivi.
 
Back
Top Bottom