Hiki ni Kiswahili cha kisasa au?

Mathethamathetha

Senior Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
152
Reaction score
148
Huwa najiuliza kama mtu amesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba na labda akaenda sekondari pia, inawezekanaje anaandika hivi:

Neno Hakuna anaandika akuna, Usipite anaandika husipite, Ibada anaandika Hibada, hifadhi anaandika ifadhi, akiba anaandika hakiba, usitupe anaandika husitupe, mahindi anaandika maindi, hayupo anaandika ayupo. n.k.

Yani nimebaki najiuliza hiki ni kiswahili cha kisasa au?
 
Sio walio zaliwa mjin mkuu!!watu wameathiriwa na lugha mama
 
Hiyo ndiyo lugha ya Kiswahili ya watu wa sasa (kizazi kipya). Lugha ya Kiswahili kwa sasa haina tofauti na Lugha ya Kiingereza kwa sasa. Kiswahili kimepoteza hadhi.
 
Wananikera sana
 
Hiyo ni athari ya lugha mama, na hao ni watani wangu wa kutokea mkoa wa Kagera wanaojisifu sana kwa usomi,na maarufu sana kwa ulaji wa panzi wa kijani.
 
Ukiniandikia msg yenye maneno hayo sikujibu milele.
Mi mwenyewe kama mtu anafundisha au ameleta hoja kwenye mitandao akaandika hivyo huwa napita tu sisomi kwa sababu inachosha kusoma vitu visivyoeleweka. Unakuta hata baadhi ya waandishi wa habari wanaoandika hivyo.
 
Hiyo ndiyo lugha ya Kiswahili ya watu wa sasa (kizazi kipya). Lugha ya Kiswahili kwa sasa haina tofauti na Lugha ya Kiingereza kwa sasa. Kiswahili kimepoteza hadhi.
Unaposema haina tofauti na lugha ya Kiingereza una maana gani mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…