Hilda Newton: Nimepokea taarifa kuwa Mohamed Issa amefikishwa Mahakama ya Uhujumu Uchumi

Hilda Newton: Nimepokea taarifa kuwa Mohamed Issa amefikishwa Mahakama ya Uhujumu Uchumi

Kutoka account ya X ya Hilda Newton:

Nimepokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Wakili Advocate Mahinyula

Anasema kwamba leo Mohamed Issa amefikishwa Mahakama ya Uhujumu Uchumi upande wa Jamhuri wakasema kwamba hawana nia ya kuelendele kesi hivyo Mohamed akaachiwa lakini cha kusikitisha akakamatwa tena na Polisi na sasa wanampeleka Mahakama ya Kisutu

NB: Enzi za Magufuli Mwaka 2019 Mohamed Issa akiwa kaimu Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Pwani alikamatwa na Polisi wakambambika kesi ya Uhujumu Uchumi. Kwasababu kesi yake haikuwa na dhamana so akapelekwa gereza la Segerea ambako amekuwa akiishi kama Mahabusu mpaka leo.Katika kipindi chote iko cha miaka 7 leo ni mara ya tatu upande ya Jamhuri wanasema hawana nia ya kuendelea na kesi wanamwachia halafu wanamkamata tena na kumshtaki kwa kosa hilo hilo
😭
Huu uonevu lazima ufike mwisho, mwachieni kijana wa watu kama ni kumtesa basi mmeshamtesa vya kutosha.
Huo ni uonevu
 
Zaidi ya ile ya king'ang'anizi kulamba asali?
Yule hakuwa na madhara!! Tunawataka muingie barabarani maana hamna mlamba asali sasa!! Nitafurahi kukuona kula kwa tindo ukikinukisha barabarani.
 
Yule hakuwa na madhara!! Tunawataka muingie barabarani maana hamna mlamba asali sasa!! Nitafurahi kukuona kula kwa tindo ukikinukisha barabarani.
Hapana, hatutakinukisha tutasubiri Mbowe atushauri tuingie kwenye maridhiano.
 
Huyo Mahinyila na Lissu si walionesha uwezo wa kufanya fujo Za kitoto kwenye chaguzi Za CHADEMA?? Vipi hawajaingiza tu watu barabarani kumkomboa Kijana??? Acheni kulia lia tupo tayari kwa mshikemshike mliotuahidi
We jamaa bado hujakubali Mbowe alishindwa uchaguzi.
 
Mtu akiwa mwizi, halafu mwanachadema, hairuhusiwi kumkamata?
Huo wizi ataufanyia wapi akiwa upinzani ndugu? Juke kuna very elites ambao wqnawajibishana kwa haki tofauti na hii ishu iliyoanza leo kisa tu aendelee kukaa mahabusu. Embu jiongeze bhasi, ifikie kipindi tuwe binadamu bila kuangalia hali za familia zetu bali taifa zima
 
Huyo Mahinyila na Lissu si walionesha uwezo wa kufanya fujo Za kitoto kwenye chaguzi Za CHADEMA?? Vipi hawajaingiza tu watu barabarani kumkomboa Kijana??? Acheni kulia lia tupo tayari kwa mshikemshike mliotuahidi
Alipowekwa ndani kwa miaka yote hiyo Mbowe alikuwa wapi?! Mbona hamkumlilia Mbowe amsadie? Leo mnaleta maneno maneno ya nongwa?!
 
Back
Top Bottom