Hili apa wazo la biashara kwa wenye mtaji

MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2013
Posts
623
Reaction score
606
Natumai mu wazima tena siku hii ya leo mkiendelea na mapambano dhidi ya umaskini niwape pole sana na niwatie moyo tu mapambano ni magumu ila tutashinda pamoja.


Bila kupoteza muda nianze moja kwa moja nipo mkoani Mara na nimepitia baadhi ya wilaya kama serengeti,tarime n.k lakini nimefika eneo la Isenyi nikaona kuna fursa ya biashara pale kwa mtu mwenye mtaji akifungua kiwanda kidogo cha mikate atapata faida na kurudisha hela yake kwa muda mfupi sana kutokana na kwamba hakuna kitu kama hicho kule na kuna mahitaji ya kutosha kufungua kiwanda pale watu wanategemea mikate inayotoka Bunda,Arusha,Mugumu kwa mtu au kikundi ambao wanaweza kujipanga wachangamkie fursa hiyo ningekuwa na uwezo ningeifanya hii biashara lakini tatizo ni mtaji kwa hiyo wenye hela zenu jamani msifurahie tu kuziona bank ila zungusheni ziongezeke kwa kuwekeza hapo. Nawasilisha
 
1.5m inatosha kama mtaji??

kwa kweli kwenye suala la mtaji sio rahisi nijue nafikiri mngetafuta kwanza bei ya ovena ya kuokea hiyo mikate alafu ndo mnaweza kujua ni kiasi gani kitatosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…