Hili bunge limejaa washenzi na wahuni sijapata kuliona toka tupate uhuru, Rev. Mtikila

ndo mwenyewe unasemaje wewe mgonjwa wa akili
 
Wewe ndio Mtikila?????? Jitoe basi kwenye hilo bunge la kihuni.

Tiba

Kukimbia tatizo sio kuzuia tatizo, kamwe mwanajeshi huwa haukimbii msitu.
 
Mh. Wewe ulikuwa bosi wangu na leo unaomba kura..Nkikupa kura yangu utafurahi weye? Hili lilikuwa swali la mmoja wa wazenji akimuuliza Pandu Ameir Kificho! Ndio hawa anawasema Mtikila?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Pu*mba*vu zao. Yaana eti wameanza kudai nyongeza ya posho mapeemaaa. Eti laki 3 haziwatoshi.
 
Mkuu, nina maana asilimia 61 kwa mujibu wa tume inataka serikali tatu lakini cha ajabu tokea tume imkabidhi Rais rasimu hiyo hawasikiki kutetea maamuzi hayo kwenye media kama Tv na radio, utasoma tu kwenye gazeti. Zile asilimia chache ndizo zimejikita mno kwenye Tv na radio kusisitiza misimamo yao na kushinikiza kupuuza maoni ya wengi. Mfano wale wanaojiita wasomi waliokutana hivi juzi wakisema eti muundo wa serikali moja ndio unaofaa, hawa jamaa ni ajabu kweli maana najiuliza kama wasomi hawajaisoma rasimu ya katiba ilivotoa majibu? Kwa nini wamejikita kwenye muundo tu wa muungano na kuacha kutetea elimu bora kwenye katiba?.
 

Njaa inatusumbua huenda ukapata hata ukuu wa wilaya! Maana kote nchini hali ni ngumu kwanin wasijipendekeze? Lazima wajipendekeze walau waonekane kwa wanamuunga mkuu wa kaya mkono lakini nyoyoni mwao naamini hawaamini wanayoyatoa katika media mbalimbali!
 
Yeye ni kiongozi katika chama chake badala ya kupendekeza wengine akajipendekeza yeye, leo anaibuka na kutudanganya kua hakuitaji nafasi hiyo swali la kujiuliza ni nani aliyempendekeza?

Mtikila mwenyewe mhuni!
 
Mchungaji Mtikila leo amekandia bunge lote la katiba na kusema anasikitka soon atalicha bunge hilo mana limechaguliwa kihuni. Nasema hivi wambieni kabisa nimesema hili ni bunge la kihuni limechaguliwa kihuni ndio maana unakutana na mambo ya kishenzi mnayoendelea kuyaona. Nasema tangia uhuru sijapata kuona bunge la kihuni kama hili. Sitoshangaa maamuzi ya kihuni na kishenzi kutokea siku tunaagana pale nje. Huyo ni rev. Christopher Mtikila
 

Kama ameshatambua ni wahuni anafanya nini huko? Au na yeye anajifunza uhuni maana hata naye kachaguliwa kihuni!!!
 
Mbona toka jana amesema hayo lakini bado tu yuko Dodoma haondoki?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kweli kabisa wote ni wahuni hâta huyo chairman wa muda muhuni tuuuu
 
Inategemea sana nani aligharamia hicho kikao cha wanaoitwa wasomi na alitaka kitoe msimamo gani! Ajabu ni kuwa kwa nini hawakupendekeza na kutetea kwa nguvu Serikali moja wakati tume inakusanya maoni na kuandika rasimu?
 
Mch. Mtikila katumia maneno makali, mazito na machafu lakini kwa upande wa pili unaweza kumtetea kwa maana hata angelikuwa mtaalamu gani wa lugha hapa duniani ni ngumu kupata majina sahihi ya kuwaita hawa watu mbali na haya aliyotumia!
Atakuwa wa kwanza kwa kauli na lugha ya namna hii kufungiwa vikao ndani ya Bunge hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…