Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
Hili CECAFA wamelifanya kwa bahati mbaya au ni ile ile ya kutembea na matokeo mkononi? Eti mshindi wa kwanza wa kundi alimo Azam atacheza kwenye hatua ya kwanza ya mtoano (robo fainali) na mshindi wa pili wa kundi alilomo Yanga.
Hivi CECAFA haijui kwamba kisoka sasa Azam iko level moja na Yanga na Simba? Kwa nini CECAFA inataka timu moja ya Tanzania ife mapema? Kama kungekuwa na Yanga na Simba, zingepangwa zitoane mapema? Si tunakumbuka mwaka 2011 jinsi Yanga na Simba walivyopitishwa kwa nguvu ili wacheze fainali? Si mnakumbuka jinsi kila penalti walizokosa wakati wa penalti tano tano zilivyorudiwa eti kulikuwa na makosa lakini kusiwe na hata penalti moja iliyokoswa na wapinzani iliyorudiwa kwa sababu hiyo au moja ambayo watanzania hao walipata iliyorudiwa kwa kupigwa kwa makosa?
Ingependeza kwa mashindano mafupi kama haya kwa timu kubwa za nchi moja kuwekewa uwezekano wa kukutana fainali tu. Nina hakika Yanga itakuwa nyuma ya Gor Mahia kwenye kundi lake na Azam itaongoza kundi lake na hivyo mtoano ni Azam na Yanga. YEYOTE KATI YAO ANAKUFA KWANI ZOTE NI TIMU KUBWA ZENYE WACHEZAJI WAKUBWA ZINAZOTAKA KUFANYA MAKUBWA. Cecafa wameniudhi sana.