Hili CECAFA wamelifanya kwa bahati mbaya au ni ile ile ya kutembea na matokeo mkononi?

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Hili CECAFA wamelifanya kwa bahati mbaya au ni ile ile ya kutembea na matokeo mkononi? Eti mshindi wa kwanza wa kundi alimo Azam atacheza kwenye hatua ya kwanza ya mtoano (robo fainali) na mshindi wa pili wa kundi alilomo Yanga.
Hivi CECAFA haijui kwamba kisoka sasa Azam iko level moja na Yanga na Simba? Kwa nini CECAFA inataka timu moja ya Tanzania ife mapema? Kama kungekuwa na Yanga na Simba, zingepangwa zitoane mapema? Si tunakumbuka mwaka 2011 jinsi Yanga na Simba walivyopitishwa kwa nguvu ili wacheze fainali? Si mnakumbuka jinsi kila penalti walizokosa wakati wa penalti tano tano zilivyorudiwa eti kulikuwa na makosa lakini kusiwe na hata penalti moja iliyokoswa na wapinzani iliyorudiwa kwa sababu hiyo au moja ambayo watanzania hao walipata iliyorudiwa kwa kupigwa kwa makosa?
Ingependeza kwa mashindano mafupi kama haya kwa timu kubwa za nchi moja kuwekewa uwezekano wa kukutana fainali tu. Nina hakika Yanga itakuwa nyuma ya Gor Mahia kwenye kundi lake na Azam itaongoza kundi lake na hivyo mtoano ni Azam na Yanga. YEYOTE KATI YAO ANAKUFA KWANI ZOTE NI TIMU KUBWA ZENYE WACHEZAJI WAKUBWA ZINAZOTAKA KUFANYA MAKUBWA. Cecafa wameniudhi sana.
 
Wakati wa kupanga makundi /ratiba hawakujua kuwa Yanga atakuwa namba 2 kwenye kundi lake
 
Tatizo CECAFA hawakuwaza kwamba Gor mahia wangeifunga yanga kwa hiyo walitegemea kabisa kwamba Yanga itaongoza kundi lake na Azam nao wangeongoza kundi lao... kwa hiyo walitegemea azam na gor mahia wangekutana kwenye robo fainali
 
Cecafa kwao muhimu..Fainali wacheze wenyeji kwa wenyeji...au mwenyeji na mgeni...
 
Hili CECAFA wamelifanya kwa bahati mbaya au ni ile ile ya kutembea na matokeo mkononi? Eti mshindi wa kwanza wa kundi alimo Azam atacheza kwenye hatua ya kwanza ya mtoano (robo fainali) na mshindi wa pili wa kundi alilomo Yanga.
Hivi CECAFA haijui kwamba kisoka sasa Azam iko level moja na Yanga na Simba? Kwa nini CECAFA inataka timu moja ya Tanzania ife mapema? Kama kungekuwa na Yanga na Simba, zingepangwa zitoane mapema? Si tunakumbuka mwaka 2011 jinsi Yanga na Simba walivyopitishwa kwa nguvu ili wacheze fainali? Si mnakumbuka jinsi kila penalti walizokosa wakati wa penalti tano tano zilivyorudiwa eti kulikuwa na makosa lakini kusiwe na hata penalti moja iliyokoswa na wapinzani iliyorudiwa kwa sababu hiyo au moja ambayo watanzania hao walipata iliyorudiwa kwa kupigwa kwa makosa?
Ingependeza kwa mashindano mafupi kama haya kwa timu kubwa za nchi moja kuwekewa uwezekano wa kukutana fainali tu. Nina hakika Yanga itakuwa nyuma ya Gor Mahia kwenye kundi lake na Azam itaongoza kundi lake na hivyo mtoano ni Azam na Yanga. YEYOTE KATI YAO ANAKUFA KWANI ZOTE NI TIMU KUBWA ZENYE WACHEZAJI WAKUBWA ZINAZOTAKA KUFANYA MAKUBWA. Cecafa wameniudhi sana.
hivi wewe unajua mpira au? kote duniani ndio wanafanya hivyo wa kwanza kucheza na wa pili wa kundi jingine
 
Tatizo CECAFA hawakuwaza kwamba Gor mahia wangeifunga yanga kwa hiyo walitegemea kabisa kwamba Yanga itaongoza kundi lake na Azam nao wangeongoza kundi lao... kwa hiyo walitegemea azam na gor mahia wangekutana kwenye robo fainali

Hakuna anayejua matokeo kabla ya mechi kuchezwa hivyo kama Azam atakutana na Yanga sio kwa sababu ya ratiba bali ni matokeo yao waliyoyapata.
 
Mimi nilishangaa zile penati za yanga tu. Wakati canavaro alikula zote refa akapeta tu.
Ndio maana mpira wa tanzania hauwezi kusonga mbele kabisa. Panapo stahili adhabu inatolewa upande m1 tu.
 
Back
Top Bottom