Hili chapuo analopigiwa Lugumi ili kumsafisha linatia shaka. Mamlaka zisichukulie kama jambo la kawaida!

Hili chapuo analopigiwa Lugumi ili kumsafisha linatia shaka. Mamlaka zisichukulie kama jambo la kawaida!

TOKA MAKTABA 2021
CEO wa Kampuni ya Lugumi enterprises limited na business partners wake wakipitia matayarosho ya Mzigo kwa nchi rafiki ulivyokuwa umekamilika na ukikaguliwa tayari kwa delivery kwa mteja

1735308973772.jpeg

Mr. Saidi Lugumi with his partner in Bulgaria checking on weapons to be delivered to a friendly country, the cargo included 40mm bombs ... RPG7 and FZU UTU, Mp1 bombs, together with bullets from 556x45mm. 556x51mm sniper bullet
 
Mnaandaliwa kisaikolojia. Huyu.wakati.wa.magufuli alikimbilia canada sijui usa.

Hakusupply baadhi.ya.mitambo ya kielectronic alikotakiwa kusupply na hela alikuwa kashalipwa.

Alikuwa na clearance top level ya kuingia bandarini kuchukua mizigo yake. Swahiba wake JK huyu. Inshort JK ndie alimbeba kiswahiba.
 
Wakuu,

Kama mmeona sasa hivi karibu kila siku Lugumi yuko kwenye media, mara katoa msaada kwa watoto yatima, mara anajengea yatima nyumba, mara kaalika watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kufanya dua, mara sijui kaenda kulisha wapi, yaani ni heka heka mtindo mmoja.

Na Millard kama kawa kwenye ishu hizi hakosi. Siyo siri kuwa anatumika na watu mbalimbali mashuhuri kuwasafisha kutokana na uozo wanaofanya kwa maslahi binafsi.

Mitume na manabii wenye rekodi za ajabu wanamtumia Millard awasafishe, wanasiasa wapuuzi wakitaka mambo yao yapaishwe kuonekana wema na wanawatumikia watanzania kama mama Teresa Millard ndio kimbilio lao, GSM (Home Shopping Center) wamemtumia vizuri kuwanfanya raia wawaone wema wakati ni wachafu zaidi ya uchafu wenyewe (kupata picha ya ufirauni wa kina GSM soma hapa - .

Millard kafuta habari zote za ufisadi kuhusu Lugumi unafikiri amefanya hivyo bila kuachiwa mzigo? Kwa hili chapuo anafanya kuhakikisha yupo machoni petu kila wakati atakuwa kamegewa mzigo mchafu wa kutosha.

Ninavyofahamu Lugumi ako na skendo za ufisadi wa kutosha, na nasikia ni mafia kwelikweli.

Hili chapuo si bahati mbaya, limekuja ghafla na kwa kasi ya ajabu, inadaiwa anaenda kuingizwa Jeshini (kama bado halijafanyika tayari) na hii ni hatari kwa usalama wa nchi.

Tunaenda kupigwa na kitu kizito jamani, amkeni tukatae mafisadi, hili bomu linalokuja tutabaki mdomo wazi!

Ni kwanini haya yanatokea chini ya Utawala wa Rais Samia?
Labella
 
Back
Top Bottom