Hili halikubaliki ni kama ubaguzi kwenye timu kama Simba

Hili halikubaliki ni kama ubaguzi kwenye timu kama Simba

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2018
Posts
830
Reaction score
898
Habari Wana JF najua mpo poa samahani kama nitakuwa nimewakwanza Kwa fikra hizi mnisamehe ila Wengi Wanaumia sana

Serikali hii inapesa za kulipia mashabiki pamoja na kuwapa pesa ya kujikimu huko South Africa, lakini mbona SIMBA SC walishawahi Kwenda South lakini hakuna mtu aliyejitokeza kuwalipia mashabiki kwenda huko??? Au tuseme yanga ndio imetawaliwa na serikali peke yake?

Hii serikali yetu pendwa Kama haijui Imeenda kutengeneza Tabaka la hatari sana katika wapenda soka nchini TANZANIA.

Je, Waliisubiria Yanga iwe robo ndio iaze kusaport? Kama ni hivyo iweje sasa hivi Inajitokeza kusema inawalipia mashabiki wa yanga kwenda South Africa Je simba sc wanaoenda misri mashabiki vipi haiitaji mashabiki??

Imeshindwa kuboresha huduma za Umeme , Serikali iliyotangaza Elimu Bure ya uongo hadi leo Walimu wa Tz wanadai michango ya walimu wakujitolea,michango ya mlinzi wa shule.. Lakini serikali inayowalipia pesa watu waende kwenye starehe zao huko South hadi leo imeshindwa kuboresha na kushusha bei za Nauli za mabasi yaani nauli ya Dar Es Salaam Morogoro Kama nchi zingine unaweza kwenda umbali wa km zaid ya elfu 1

Halafu linatokea Dude na Kitambi chake linasema Mama anaupiga mwingi[emoji23][emoji119]

Yaani ukipita kariakoo makundi maalumu ya wanaomba msaada kwa wapita njia, huwa najiuliza hivi serikali imeshindwa kuwasadia hawa watu au hawastahili kupata misaada?

Hawa watu hata kwa mwezi ukawapa laki ya kula ni thawabu kuliko kuwalipia nauli na kuwapa pesa ya kujikimu hawa watu wanayoipa hasara serikali mara kwa mara kwa kuvunja mageti pale Taifa.

Haya ni matumizi mabaya ya Pesa za wananchi ,kumbukeni hizi ni kodi na wananchi wa Tanzania[emoji24]

Mngetumia pesa kutangaza utalii kama anavyofanya nchi za Jirani mfano Kagame pengine mgeongeza Utalii na kupata pesa nyingi za kigeni,kuliko kuwapa pesa watu wakatumie kwenye starehe South Africa baadae serikali inakuja kutangaza Deni la Taifa limepanda Hadi Tilioni 100.

Uchumi wa Nchi upo Stagnant kwasababu ya mambo kama hayo.yaani kodi za wananchi wanalipiwa naurl na pesa ya kujikimu mashabiki wa Yanga kwenda hadi South.Yaani wakifika Zambia wanashuka wanakula pesa ya serikali,wakifika Zimbabwe wanashuka wanakula wanakula pesa ya Serikali bila kusahau na kunywa [emoji23][emoji119][emoji119]

Aya kwakuwa basi acha tunaseme mama anaupiga mwingi Si ndiyo mnataka tusifie ,basi mama anaupiga mwingi[emoji119]

Okay Good evining [emoji274] Tanzania.

Mungu atusaidie sana soka la Tanzania lisiendelee kuwepo Kwenye Siasa.

Pia soma: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF
 
Mbona simba nao wameomba na wamekubaliwa? Alafu kama una uchungu na pesa za serikali gombea urais uje ubane bajeti.
 
Mbona simba nao wameomba na wamekubaliwa? Alafu kama una uchungu na pesa za serikali gombea urais uje ubane bajeti.
Nilishasema 2030 mungu akitujalia raisi wangu anakuwa poul makonda
 
Investment unaofanya sehemu inayolipa boss.

🔹 Moja wapo ya kazi ya serikali ni kuwaletea wananchi wake furaha.

🔹 Hii ni principle halali kabisa iliyotungwa na MWANA Filosophia na Jurisprudence JEREMY BENTHAM katika principle yake ya UTILITARIANISM.

🔹Alisema " jambo lolote linaloleta furaha liungwe mkono na liendelezwe na jambo linaloleta huzuni lifutiliwe mbali.

🔹 Ukifuatlilia wiki nzima ya mechi ya YANGA nchi nzima ilikuwa na furaha, kile kitendo Cha watu kusafiri kutoka Kila Kona ya Tanzania na nje ya nchi kilileta maximum pleasure kwa wananchi na serikali ilifikia malengo yake. Utaona kuwa japo kuwa walivunja mageti lakini hakuna kilichotokea kwa sababu walikuwa wanaofuata furaha ilipo. Hapo serikali iliona kama mtoto kafurahi na kuvunja chupa kwa bahati mbaya. Mama atanunua nyingine

🔹. Sasa Simba inaleta huzuni, kwa mashabiki na wananchi serikali itawasapoti kweli? Sasa timu inachafua Hali ya hewa Kila wakati halafu inalialia kuomba usafiri wa ndege wakati wazee wa UTILITY wanasafiri kwa mabasi?
 
Investment unaofanya sehemu inayolipa boss.

🔹 Moja wapo ya kazi ya serikali ni kuwaletea wananchi wake furaha.

🔹 Hii ni principle halali kabisa iliyotungwa na MWANA Philadelphia JEREMY BENTHAM katika principle yake ya UTILITARIANISM.

🔹Alisema " jambo lolote linaloleta furaha liungwe mkono na liendelezwe na jambo linaloleta huzuni lifutiliwe mbali.

🔹 Ukifuatlilia wiki nzima ya mechi ya YANGA nchi nzima ilikuwa na furaha, kile kitendo Cha watu kusafiri kutoka Kila Kona ya Tanzania na nje ya nchi kilileta maximum pleasure kwa wananchi na serikali ilifikia malengo yake. Utaona kuwa japo kuwa walivunja mageti lakini hakuna kilichotokea kwa sababu walikuwa wanaofuata furaha ilipo. Hapo serikali iliona kama mtoto kafurahi na kuvunja chupa kwa bahati mbaya. Mama atanunua nyingine

🔹. Sasa Simba inaleta huzuni, kwa mashabiki na wananchi serikali
Pale unapopewa pepa la mtihani na unapopangilia kazi yako vzr unasema leo napata mia ya mia kumbe pointi zingine umeandika ushubwada...unarudi na 10... 😀 😀 😀 😀
 
Mbona mafisadi wakila mabilioni huongei kwa uchungu si kodi zetu pia .
..
 
Acha watu wale hela ya serikali wewe! Nchi yenyewe ilishauzwa kitambo. Au unataka watu wachache pekee ndiyo waendelee kufaidi?
 
YANGA inaonesha matumaini MWAKAROBO ashajifia pesa zitapotea bure.
 
Kabla ya mechi ya raundi ya kwanza serikali il8shasema tunasubiri maoni ya hizi club kuona serikali itawasaidiaje kuelekea mechi za robo fainali Yanga ilikua ishaamza kampeni yake kwa mashabiki kuchangia kiasi cha Tsh 600k ivyo baada ya kuona ser8kali inaweza saidia ikapeleka ombi. Hivyo lilikua ni jukumu la viongozi wa club ya Simba na wao kupeleka maombi yao.

Kuhusu matumizi ya hizi pesa naomba muwe waelewa kuna fungu limetengwa kwa ajili ya shughuli kama hizi kwa kila wizara na ndio maana taarifa inasema serikali kupitia wazara ya michezo imefanya jambo fulani, sio kila mara muwe mnakuja kulia lia sijui kuna omba omba ukiwaisaidia utapata thawabu ningekushauri nenda kawasadie wewe hizo thawabu zinakusubiri.

Punguzeni makasiriko mjitume zaidi itawasaidia sana.
 
Kama kuna pesa zimetengwa Kwa ajili ya haya maswala ebu tukumbushane ni timu ngapi zilikosa nauli ya kwenda kucheza nje huu ni ujinga ambao selkali inafanya
 
Usishindane na uvccm. Acha malalamiko boss. Hizo ni tabia za wale wenye jezi zenye rangi ya chama.
 
Back
Top Bottom