Hili halikubaliki ni kama ubaguzi kwenye timu kama Simba

Mkuu sisi hatuhitaji huo msaada wa kinafiki na wa kisiasa,, sisi twende kimyakimya kama underdogs mana tunajua tunaenda kukamilisha ratiba tu ya mechi ili turudi tuendelee na ligi kuu.
 
Hii principle haipo hivi, wapo ambao pia walipata furaha Kwa mpira wa Simba ilihali walifungwa goal 1 halafu utambue kua Simba hajatolewa kwenye Mashindano ule ni mpira na bado haujaisha angekuwa amefungwa goal 2 sawa ila 1 bado nafasi anayo kubwa tu...
 
Yanga wenyewe wameomba shida iko wapi?
Ndiyo maana sijawahi kuwadharau Simba kwa ujumla sababu najua wenye akili mpo wengi tu.
Binafsi sina shida na Yanga kuomba msaada serikalini. Shida Yangu ni huo msaada wa hadi kulipa posho mashabiki. Ingekuwa ni wachezaji hapo sawa. Ila kwa jinsi baadhi ya wanasimba wanavyolipinga, hapo ndiyo sikubaliani nao.
 
Simba wataitia Serikali hasara mara mbili, kwenye kurudi Simba Wengi watasafirishwa kwa ushirikiano wa Serikali ya SA na TZ.
If you know what I mean.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…