Hili jambo linanitafuna sana.

Hili jambo linanitafuna sana.

Joined
Oct 27, 2024
Posts
33
Reaction score
277
Toka nakuwa na ufahamu nimeona wazazi wangu wakipambana sana, lakini bahati haijawa upande wetu, mama kavunja sana kokoto, baba nae kapambana sana lakini wapi.

Wazazi wangu wamenisomesha kwa shida sana, hadi chuo kikuu ambapo serikali ilinipa mkopo, wazazi walitegemea sana niwe mkombozi wa familia Baada ya masomo. LAKINI imekuwa tofauti Sana.

Toka mwezi wa Saba nimemaliza, nimejaribu kupambana kutafuta kazi ya fani yangu ya ualimu lakini pote napokwenda nakosa, application zaidi ya kumi na sita lakini wapi.

Nimejichanganya mitaani, wakuu Kila kazi napiga lakini malipo ni madogo sana , kazi takutumia nguvu hazina malipo mazuri kabisa. Pesa inaishia nyumbani, na mahitaji ya wadogo wangu, wazazi wamechoka sana na umri wao umeenda Sana

Kwa wiki napata kazi mara mbili tena hapo Kwa kutafuta na hungaika sana, malipo ya saidia fundi huku kwetu ni elfu Saba siku nzima.
Napesa yenyewe haikai, natoa sapoti nyumbani ( maisha yetu ni kama msumari na nyundo ).

Sina mtu, Wala ndugu anaweza nishika mkono au kunipa mtaji , ikifika jioni najikunja nakuwaza sana. Hii kitu inaniuma sana Sana.

Nawaza hivi kwa maisha haya kweli tatoboa, Kweli takuwa na mafanikio. Bahati Mbaya ajira zenyewe ngumu I feel too bad 😓😓😓
 
Pole haya ni mapito tu wala hayadunu miaka yote.

Mmezaliwa wangapi nyumbani?
 
Utatoboa tu mkuu,endelea kujichanganya. Kwanza ulifanya kosa kubwa sana kusoma ualimu. Hiyo hata ukiajiriwa kwa hiyo kazi bado utakua masikini kama ulivyo sasa. Kwa ustawi wako,zingatia yafuatayo;

1.Unamudu vizuri kuendesha gari,pikipiki,bajaji na Guta
2. Uwe mchapakazi kwelikweli. Ishi kama hukuwahi kwenda shule ila ktk michongo yako ipige kisomi kiwango cha Phd
3. Kuwa na nidhamu isiyotia mashaka ktk kazi zako. Weka nidhamu ya kiseminari
4. Kuwa muaminifu 100%. Usijaribu wala kuwaza kuiba,kudhukumu na kuhujumu cha mtu

5. Jijengee uwezo wa kujichanganya nq matajiri au watu waliofanikiwa kukuzidi. Kama una tabia tajwa hapo juu hutokosa majukumu na kipato cha kusurvive kisha mdogo mdogo utaaminika kwenye michongo

6. Ukianza kupata michongo tumia akili na uwezo wako wote kuanzisha kitu chako! Kaa mbali kabisa na kampani za ulevi na umalaya

7. Muombe sana Mungu na kutoa sadaka kwa mujibu wa imani yako ktk hatua zako zote kuanzia sasa

Nakutakia kila la heri mkuu. Ni wewe wa kuikomboa familia yako kiuchumi na sio mtu mwingine. Ukishindwa tutakulaumu wewe. Hilo sitaki kukuficha mkuu! Kila kitu kinawezekana ukiamua na kukubali kulipa gharama hitajika
 
Nyakati ngumu huwa zipo kwenye maisha ya kila mwanadamu ili kutufunza mambo mbalimbali. Endelea kupambana huku ukimtumainia Mungu wako. Tayari una pakuanzia, elimu uliyoipata ni mtaji, usikate tamaa.

Huwezi kujilinganisha na vilema au watu ambao hawakupata fursa ya elimu kama yako. Jichanganye na makundi ya wapambanaji, elimu yako itakukomboa katika wakati usiotarajia. Pia pitia vizuri mchango #6
 
Utatoboa tu mkuu,endelea kujichanganya. Kwanza ulifanya kosa kubwa sana kusoma ualimu. Hiyo hata ukiajiriwa kwa hiyo kazi bado utakua masikini kama ulivyo sasa. Kwa ustawi wako,zingatia yafuatayo;

1.Unamudu vizuri kuendesha gari,pikipiki,bajaji na Guta
2. Uwe mchapakazi kwelikweli. Ishi kama hukuwahi kwenda shule ila ktk michongo yako ipige kisomi kiwango cha Phd
3. Kuwa na nidhamu isiyotia mashaka ktk kazi zako. Weka nidhamu ya kiseminari
4. Kuwa muaminifu 100%. Usijaribu wala kuwaza kuiba,kudhukumu na kuhujumu cha mtu

5. Jijengee uwezo wa kujichanganya nq matajiri au watu waliofanikiwa kukuzidi. Kama una tabia tajwa hapo juu hutokosa majukumu na kipato cha kusurvive kisha mdogo mdogo utaaminika kwenye michongo

6. Ukianza kupata michongo tumia akili na uwezo wako wote kuanzisha kitu chako! Kaa mbali kabisa na kampani za ulevi na umalaya

7. Muombe sana Mungu na kutoa sadaka kwa mujibu wa imani yako ktk hatua zako zote kuanzia sasa

Nakutakia kila la heri mkuu. Ni wewe wa kuikomboa familia yako kiuchumi na sio mtu mwingine. Ukishindwa tutakulaumu wewe. Hilo sitaki kukuficha mkuu! Kila kitu kinawezekana ukiamua na kukubali kulipa gharama hitajika
Ushauri mzuri sana
 
Toka nakuwa na ufahamu nimeona wazazi wangu wakipambana sana, lakini bahati haijawa upande wetu, mama kavunja sana kokoto, baba nae kapambana sana lakini wapi.

Wazazi wangu wamenisomesha kwa shida sana, hadi chuo kikuu ambapo serikali ilinipa mkopo, wazazi walitegemea sana niwe mkombozi wa familia Baada ya masomo. LAKINI imekuwa tofauti Sana.

Toka mwezi wa Saba nimemaliza, nimejaribu kupambana kutafuta kazi ya fani yangu ya ualimu lakini pote napokwenda nakosa, application zaidi ya kumi na sita lakini wapi.

Nimejichanganya mitaani, wakuu Kila kazi napiga lakini malipo ni madogo sana , kazi takutumia nguvu hazina malipo mazuri kabisa. Pesa inaishia nyumbani, na mahitaji ya wadogo wangu, wazazi wamechoka sana na umri wao umeenda Sana

Kwa wiki napata kazi mara mbili tena hapo Kwa kutafuta na hungaika sana, malipo ya saidia fundi huku kwetu ni elfu Saba siku nzima.
Napesa yenyewe haikai, natoa sapoti nyumbani ( maisha yetu ni kama msumari na nyundo ).

Sina mtu, Wala ndugu anaweza nishika mkono au kunipa mtaji , ikifika jioni najikunja nakuwaza sana. Hii kitu inaniuma sana Sana.

Nawaza hivi kwa maisha haya kweli tatoboa, Kweli takuwa na mafanikio. Bahati Mbaya ajira zenyewe ngumu I feel too bad 😓😓😓
Umaskini huzaa umaskini. Wazazi wako walijua hawana uwezo na wakajiona wao ni mabingwa wa kutotoa watoto kama kuku anavyototoa vifaranga. Matokeo yake ni kuwa wamekubebesha mzigo wa kulea wadogo zako. Ushauri wangu ni kwamba kwenye maisha, kukata tamaa ni adui namba wani kuliko umaskini wenyewe. Soma vitabu ujifunza watu wenye ulemavu na matatizo mengine walivyoweza kupambana na kuwa matajiri.
 
Jaribu kuhama huo mkoa Ila ukitaka kutoboa Kwa haraka tafuta energy ilimradi iwe haina madhara hasi.

Naona ukiendelea kukaa hapo utachelewa kufanikiwa .

Energy itafute ikufanye kukubalika kila unapoenda .

Muda mwingine jitahidi ufungue code maisha sio magumu kiasi hicho
 
mkuu hali kama yako ni nzuri sana, mimi napenda nyakati km hizo maaana kupitia hali hyo ndipo ubongo wako unapofikiria sana..na nikueleze tuu ukweli hapo ulipo haupo mbali na utajiri..........omba mungu sana usipate kwanza hyo kazi ya ualimu kwa haraka ,maana utafell.
 
Nyongeza ya ushauri mzuri wa wengi ni kuwa:hizo application letters nazo ni chimbuko la umasikini kwani akili yako haitulii sehemu moja na hivyo kutojitambua wewe ni nani.Hili litakufanya ukose uamuzi wa nini cha kufanya kama nani na kuishia kvangatanga.
 
Umeelezea lakini ungesema umesoma ualimu wa science au wa arts astashahada, stashada, shahada kwasababu kuna watu wengi humu pengine ungepata msaada.
 
kama umesomea biology kuna avarage ya miaka 4 kukaa mtaani bila ajira rasmi unless uajiriwe private .
 
Back
Top Bottom