Hili joto kupikia jiko la gas kwenye chumba na sebule ni mateso

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Siku hizi zile foleni za kungojea mafiga kwenye nyumba za kupanga zimepungua sana. Siku hizi wengi wana majiko ya gas chumbani. Kwa kweli yanasaidia sana kuokoa misitu, kurahisisha maisha. Hata hivyo joto unalopambana nalo kwenye chumba wakati unapika ni kadhia nyingine.

Unaishi kwenye chumba na sebule. Sebule usiku ni chumba cha dada cha kulala na mchana ni sitting room, dining na jiko. Hapa una wageni na nyumba haina ceiling board. Lile jua la saa saba-nane mchana ni kama mko kwenye tanuri.
 
Dada na watoto wanalala sebuleni, ukiwa unaliwa usiku wanasikia makelele yote. Sebule linanukilia ugali na dagaa kutwa nzima. Maisha ya bongo shida sana.
 


Pole sana madam ila kwa sasa pambana na hali yako kwani SULUHU (sio Freeman) ni katiba mpya. 🤣
 
Kwa upande mwingine hali hii inatia hamasa kubwa ya kupambana ili mtu ahamie kwenye makazi bora zaidi.
 

Ukweli ni kwamba chumba na sebule kinamfaa asiye na familia yaani anayeanza maisha! Lakini ikitokea mkeo akapata mimba basi unaanza kujipanga kivingine!

Ukiacha swala la maisha lakini ni mateso makubwa sana kuwa na familia halafu uko kwenye chumba na sebule aisee
 
Unafikiri mke akiwa mjamzito mshahara huwa automatically unaongezeka wapi. Na mama mkubwa wa mke wako ndiye anaejua kumhudumia mzazi. Anaishi na nyinyi kwa miezi sita akimfundisha wife ulezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…