Hili jukwaa limepunguza sana mvuto tofauti na kipindi cha nyuma nini tatizo?

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Kipindi cha nyuma kulikuwaga na mijadala migumu sana humu,
Kulikuwa na hamasa sana, watu nakumbuka walikuwa hadi wanakutana kwa Chai day na wana discus Biashara hasa kilimo,

Idea ya Jamii Saccos ilianzishwa na wadau wa humu na Saccos ikaanzishwa,Wadau humu nakumbuka wakina Chasa, Liverpool, Madinimadini na wengineo wali fanya hadi mkutano mkubwa pale Rombo green view hotel.

Kulikuwa na wadau kama Malila, sijui wako wapi siku hizi wanachungulia tu na kusepa.

Jukwaa limevamiwa na watoto, limevamiwa na watu ambao humu ni sehemu ya kujipumzisha, humu huja kana kwamba wamepotea njia.

Jukwaa halina kash kash kama za enzi zile ambapo kulijjwa na mijadala migumu sana na pia watu walikuwa wanakutana kufanya mikutano na pia watu walilima pamoja,

Ile nguvu sidhanii kama itarudigi make now day wengi wanao ingia humu kuchangia na kupost utaona kabisa uwezo wao ni mdogo sana na wengi wanakuja kupumzika tu,

Nawakumbuka sana watu kama Malila, ELININO na wengineo Watu kama Liverpol watu kama chasa

Humu lazima watu wabadilike watu wawe kweli na nia.
 
Sahihi kabisa, ht mm nilijiunga JF kwa hamu kubwa kutokana na mijadala iliyokuwa ikijadiliwa humu, Kwanza nilikuwa msomaji tu kwa kipindi kirefu ndo bdae nikajiunga, nimeona jinsi kulivyo ss Ni doro sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imekuwa jambo gumu kwani watu wameona huu ni uwanja wa kuweka uzushi na kashfa kwa maslahi yao pasipo tena kujali ukweli manufaa ama atharibya wanachoandika
 
Jukwaa limevamiwa na wanapropaganda

Wanazusha, wanadanganya, wanapotosha waziwazi bila woga wala aibu.

Lakini pia moderators kuibeba dhana ya where we dare to talk openly vibaya..... Kutoa mwanya kwa niliyoyataja hapo juu kufanyika bila hatua kali kuchukuliwa.

Ukweli tumepoteza dira.
 
kiukweli kabisa hili jukwaa na lile la tech ndiyo yaliyonifanya nijiunge jf lakini siku hizi naona watu wamekimbilia kwenye ssias wakitupiana kashfa tu
 
Habari zinachujwa sana. Kuna siku nilijiuliza. Hiv ckuiz CCM inatoa dau ili baadhi ya post zifutwe? Unakuta Uzi upo zaidi ya masaa 12 na comments zaidi ya 100. Ila mods wanafuta
 
TATIZO NI KWAMBA HUMU WAMEJAA WAPUUZI WATUPU NI BORA MUONGEE NA MOD AWATENGENEZEE SUB JUKWAA KWA AJIL YA WATU SIRIASI TU

MOD ANAWEZA TENGENEZA SUB
 
kama ulikwemo akilini mwangu. ila makuzi mengi sana humu kwa sasa sizioni zile nondo au zimepitiwa na wasiojulikana
 
Humu kuna UMOJA WA VIJANA wanaopiga wazee wao huwezi pata hoja na mijadala ya maana. Hata ikianzishwa inavurugwavurugwa na UMOJA WA VIJANA.
 
Siasa ndo tatizo, watu wanaona bora wakatoane mapovu kule kwenye siasa kuliko kuja hapa kujadili namna ya kupambana na hali zao
 
Mnashangaza mno mnaolazimisha mambo ya zamani kuwa ya leo. Zamani kulikuwa na Leyland bus, leo kuna Zhengzhou Yutong bus. Hata hivyo hizo mada za kilimo mbona zipo?

Kuna thread inaendelea kuhusu Kuporomoka kwa zao la Mbaazi. Ndo maana kuna member akasema hakuna aliyekatazwa kuleta mada hizo. Acheni lawama haisadii kitu
 
Acheni tuseme ukweli.

Tutasemea wapi ukweli ilihali mtu anasema ni bora malaika washuke kwa japo dakika 1 ili waizime mitandao ya kijamii.

Facebook hapaliki ukisema ukweli unakamatwa.

Hapa ni jukwaa huru japo mnaifanyia fitina zisizokuwa na mashiko.

Mtu anatoa taarifa jinsi wizi unavyofanyika badala ya kufanya uchunguzi kwa wanaotuhumiwa nyie mnakimbilia kwingine.

Hapa JF majukwaa mbalimbali yamewekwa ambayo yanakidhi kila haja za watu, ni chaguo lako sasa kuangalia jukwaa linalokufaa na kushughulika nalo acha mengine yasiyokuhusu.

JF Live Long.
 
Badala ya kulalama ni vyema ungebadilika na kuchukua maamuzi ya kurudisha kile ulichokuwa unakitaka..

Halafu siku hizi sio kama zamani tena, mambo yamebadilika, teknolojia imebadilika, sheria zimebadilika, watu wamebadilika.. Kwa hiyo usishangae kukosa baadhi ya vitu..

Cha kufanya kama unaweza Anza kubadilika wewe ili uhamasishe nao wabadilike...JF ina majukwaa mengi sana.. Chagua ulipendalo weka nia vitu visivyo na maana vipotezee chukua vya maana
 
Kila jambo na wakati wake. Ukweli ni huu..

1/Kiujumla kwa sasa shughuli nyingi za biashara zimedorora sana karibu kila mahali, hivyo msisimko wa kujadiri mambo ya biashara umepungua na unaelekea kupotea kabisa. Hivyo tusishangae sana, maana Jamii forums ndio kioo ya yale yanayoendelea kwenye jamii zetu.

2/Kwa sasa kila kitu ni siasa, kila mtu analazimika kufuatilia siasa kwa sababu siasa imeathiri maisha ya watu moja kwa moja. Na kila mtu anajaribu kuchukua upande wa kisiasa wa kusimamia. Hakuna ujanja na hatuwezi kukwepa.

3/Kila jukwaa lina wahenga wake(Senior participants) na hao ndio wana mchango mkubwa katika kuchochea mijadala. Hao wakilala, na jukwaa lina lala na kupoteza mwelekeo. Sasa tujiulize humu ndani, wahenga wa jukwaa hili wanafanya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…