Hili jukwaa limepunguza sana mvuto tofauti na kipindi cha nyuma nini tatizo?


Mkuu kuna wakati wa kujadili mada then wale walio BOLD huwa wanamove forward na kufanya action, labda nikuulize wewe ulitaka watu wawe wanajadili stori tu kila siku? Labda nikujulishe tu: Huyo Chasha Poultry Farm unayemtaja next month tutakuwa naye kwenye safari to Nairobi kucheki maonyesho ya kilimo; Mkuu Malila unayemtaja mimi binafsi ninashiriki naye pamoja na wadau wengine kwenye miradi mikubwa zaidi ya mitatu ambayo ilijadiliwa humu humu toka mwaka 2010; Mkuu ONTARIO ana project inarun sasaivi na watu wanapiga shule; Mkuu Zainab Tamim saccos yetu inarun sasaivi na watu tushaanza kununua hisa. SASA LABDA NIKUULIZE KWA HERUFI KUBWA; UNATAKA WATU WAWE WANAJADILI TU KWA MANENO? TAKE ACTION.

NB: Wakuu nilowataja hapo juu mniwie radhi nimeshindwa kujizuia kuwataja coz you guys can break mountains with your courage.....salute to you all.
 
Hili jukwaa limenifunza mengi yahusio ujasiri Mali.
Ukweli zamani jukaaa lilikuwa bora zaidi.
Lakini nashukuru bado Chasha Poultry Farm tuko nae bila kumsahau The Consult hao wengine wamekuwa wakichungulia.
 
Asante kwa kututaja, tumefurahi sana na kuona kumbe tumo.

Sasa hivi tuna mradi mpya na mzuri sana kwa ataependa kujiunga nasi. Usomeni hapa: Sasa tumewaletea uwekezaji mpya unaolipa kihalali
 
Watu hawangaiki tena na mambo ya biashara, hawasaidiani imebaki mambo ya kupuzi tu
 
Hamasa Haziendani na Hali halisi ya Biashara.. Kuna Watu wanazungumza like if Hela ni rahisi sana kuipata... But in reality una Haso sanaa
 
Uko sahihi. Pia ikumbukwe,biashara nyingi ziko taabani ukianza na ya mazao. Kwa hali hiyo,hata mawazo nayo yanakuwa down.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…