Hili kwa wanachuo; ni janga zaidi ya tulijuavyo na kulisikia

mkandi

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
281
Reaction score
121
Leo saa 2 usiku, redio one imetangaza kua mwanachuo wa mwaka wa 3 shahada ya uuguzi, St. Johns university, amebakwa na mwili wake umeokotwa asubuhi. Hivi karibuni, wanachuo wa IFM na J.K Nyerere waliandama kupinga vitendo vya wizi, ubakaji na ulawiti dhidi yao.
Haya yamenikumbusha takribani miezi 6 nilipokua Dodoma. Wanachuo wa off-campus, hasa wa St. Johns, CBE na UDOM walikua wakiingiliwa kwa zamu na kufanyiwa matendo hayahaya. Nilibahatika kukutana na victims kadhaa pale dodoma hosp.

Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa na polisi walitambuliwa kua ni walewale waliofanya vitendo hivyo katika chuo cha SAUT-Mwanza miezi kadhaa iliyopita, na kwamba vitendo vilipungua baada ya baadhi yao kuuawa huko.
Nilichojifunza na kujiuliza katika hili:
1)hawa jamaa wanafanya kazi kama mtandao (ndo maana dodoma walikamatwa gesti kama kundi)
2)wanapata wapi ujasiri wa kunajisi bila hata kinga, chumba kwa chumba, mwanachuo baada ya mwingine? Wana ajenda gani?
3)Je tatizo ni visasi juu ya wanachuo, zaidi ya tatizo la wizi?( so far ziibiwazo zaidi ni laptop baada ya kunajisi-kunani na hizi laptop?)
4)Je tofauti ya maisha ya jamii na wanachuo mitaani ni bomu jingine?

Ubakaji, ulawiti na wezi kwa wanachuo ni zaidi ya tatizo la kihalifu na kwangu mie; hili suala NI ZAIDI YA NILISIKIAVYO NA KULIJUA!


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wengine taarifa imetukuta njiani, amebakwa akiwa chuoni au nje ya chuo?
 
Kweli nchi hii haina mwenyewe na wengi wameshajua ndiyo maana wanatawala wanavyotaka wao. Tanzania utawala wa nchi na usalama wa raia uko wapi? Yaani hadi umekuwa ni mtindo kuwabaka, kuwalawiti, na kuwaua wanavyuo? Kwani the so called serikali iko wapi? Rais mzima na mvi zake kichwani anaenda kubembea huko kwa wenyewe kila kukicha wakati nchi inateketea mikononi mwake? Wanavyuo wakiandamana mabomu ya machozi. Raia wakiandamana kudai haki yao ya ulinzi na usalama wanapigwa mabomu ya machozi. Ni nani atusemee kuhusu ulinzi na usala hapa Tanzania? Tunahitaji usalama vyuoni na katika mashule yetu. Tunahitaji usalama uraiani na matika mazingira yote ya nchi yetu. Polisi wanabaka, wanaua, wanababikizia watu makesi yaani nchi inaondoka polepole na hakuna kiongozi yeyote wa kutusaidia hapa. Kweli inasikitisha sana.
 

Wewe ndugu huna akili kabisa sasa rais ulitaka awepo ili akamate wabakaji au wabakaji wana uhusiano gani na rais
 
Hili si suala la uharifu wa kawaida ni la mfumo hatarishi. Mfumo wa kuacha wanachuo kama kuku wa kienyeji bila chuo kuwajibika kuwatafutia makazi ndiyo chanzo cha matatizo haya. Maisha ya wanachuo wengi wanaoishi uraiani ni hatari tupu. TCU lazima wawapige stop watu wanaojenga madarasa bila mabweni na kuyaita vyuo kikuu. Vyuo visiruhusiwe kudahiri wanafunzi zaidi ya wale vinavyoweza kuaccomodate. Mfano, udsm first year tu ndo wanaopata vyumba the rest shauri yao (msewe au jesus village). Kuna chuo kikuu kimoja Tanga wanafunzi wake wanalazimika kupanga kwenye nyumba za nyasi. Stella Maris Mtwara wenye nyumba hawaruhusu wanachuo waliopanga kutembelewa na wenzao vinginevyo wawalipie pango (pango linalipwa kwa kichwa), ukikaidi unafukuzwa na chenji hairudi.
 
Wewe ndugu huna akili kabisa sasa rais ulitaka awepo ili akamate wabakaji au wabakaji wana uhusiano gani na rais
Nimejaribu kutafakari juu ya ulichokiandika nikalinganisha na jina lako, naona kama vinafanana vilee.... Hivi unapoambiwa kuwa wafungwa kadhaa wameachiwa kwa msamaha wa raisi, unadhani raisi ndo physically anayafungua makomeo ya milango ya magereza?
 
Wengine taarifa imetukuta njiani, amebakwa akiwa chuoni au nje ya chuo?

Mkuu, alikua mama mtu mzima kidogo; akitokea Library mida ya saa tatu usiku. Akaokotwa asubuhi yake (jana).

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
. Mfumo wa kuacha wanachuo kama kuku wa kienyeji bila chuo kuwajibika kuwatafutia makazi ndiyo chanzo cha matatizo haya..
ulichosema Isotope, nakubaliana nacho sana. Hata taaluma inashuka vyuoni. Muda mwingi unatumika katika usafiri na kuteka maji. Usiku hawataenda Library tena wale.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Vyuo vifanye hima kushirikiana na wananchi na jeshi la polisi ili kuimarisha ulinzi.Pia madereva wa bodaboda wasajiliwe ili wajulikane na wachungane wenyewe ili kudhibiti uhalifu.Nadhani ndivyo ilivyofanyika SAUT-Mwanza hadi usalama ukarudi katika hali ya kawaida.
 
liweke akilini hili kwenye nyekundu,wakati nyie mnaandamana kudai mikopo(wenyewe mnaita kudai pesa zenu)kuna mfanyakazi,achia mbali watu wa mtaani,wanaolipwa pungufu ya shs 5000 kwa siku...kumbuka hiyo 5000 ndiyo inatumika kulipia nyumba,chakula,ada za wadogo zenu,nauli......etc.ukimaliza chuo wewe,kama unasoma shahada,tegemea kupata pungufu ya sh 15,000 kwa siku KAMA UTAFANYA KAZI SERIKALINI..najua sasa hivi mnakopeshwa sh 7000 kwa siku............nafurahi angalau umeliona tatizo.
 
Usalama wa taifa mkataba wa kazi ni 24hrs ila wao wanakunywa tu pombe, kila kitu polisi,polisi hawawezi peke yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…