Uchaguzi 2020 Hili la Dkt. Magufuli kutumia kisukuma kwenye kampeni siafiki

Uchaguzi 2020 Hili la Dkt. Magufuli kutumia kisukuma kwenye kampeni siafiki

Mpucha

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2012
Posts
1,232
Reaction score
1,592
Nimemsikia mgombea urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli, kwenye kampeni zake zinazoendelea huku kanda ya ziwa, amekua akitumia kisukuma mara kwa mara.

Hatukuwahi kusikia Rais yoyote waliotangulia wajifanya kama anavyofanya magu.

Najiuliza tu, wagombea wengine wa vyama CHADEMA, ACT Wazalendo, CUF nk wafanye kama anavyofanya Magufuli?
 
Aende Hai aone Mbowe ambavyo humwaga kichaga kwenye kampeni yake ya ubunge
 
Nyani haoni kundule. Mfatilie Ezikiel Wenje mgombea wa Ubunge kupitia chadema mkoa wa mara jimbo la Rorya. Hakuna siku ametumia lugha ya Taifa adi mwisho wa kampeni. Anatumia kiluo kila sehemu yeye tumweke kundi gani?

Lisu alivyoenda singida alitumia kinyaturu mara kibao mbona hukusema?
 
Unamshauri au unasemelea?

kwa maana yeye anamwaga sera zake, so kama huzielewi tafta ya Hashimu Rungwe utazielewa tu Mkuu. Mbona hailazimishwi kuelewa sera fulan
 
Magufuli ni Icon ya Taifa, hao kina wenje, tundu lisu nk nk hao ni wao kama wao, magu yupo level ya kina mkapa, Jk, mwinyi na nyerere, yeye ndiye anaongoza njia hao wengine wanaiga tu, taifa likiingia kwenye ukabila au udini hataulizwa wenje wala lisu naomba uelewe hivyo. Anaetakiwa kukemea hayo ni yeye, sasa hebu niambie wabunge wote zaidi ya 300 kila mtu afanye kampeni kwa lugha yake nini hatma yake ?
 
"Ukiona kiongozi anatumia ukabila au udini kutafuta legitimacy ya kisiasa, huyo amefilisika" Mwalimu JK Nyerere.
 
Wabongo bana kukosoa tu kila kitu... kuna shida gani kutumia kisukuma? sasa kama kautana na watu wa kwao unataka aongee kiswahili?
 
Nimemsikia mgombea urais kupitia ccm, mh Magufuli, kwenye kampeni zake zinazoendelea huku kanda ya ziwa, amekua akitumia kisukuma mara kwa mara. Hatukuwahi kusikia rais yoyote waliotangulia wajifanya kama anavyofanya magu. Najiuliza tu, wagombea wengine wa vyama chadema, act, cuf nk wafanye kama anavyo fanya Magu ?
Ni mara yangu ya kwanza kumsikia rais akitumia lugha ya wenyeji katika matukio kama haya. Wasaidizi wake wamsaidie kwa ushauri wasikae kimya.
 
Kabisa Mkuu mtu hatari sana huyo na ni mbaguzi sana.

Magu angekuwa rais wa kwanza Tanzania nahakika tungekuwa wakabila wabaya zaidi kuliko Rwanda na tungekuwa tupo vitani saizi, jamaa ni mkabila vibaya sana.
 
Nimemsikia mgombea urais kupitia ccm, mh Magufuli, kwenye kampeni zake zinazoendelea huku kanda ya ziwa, amekua akitumia kisukuma mara kwa mara. Hatukuwahi kusikia rais yoyote waliotangulia wajifanya kama anavyofanya magu. Najiuliza tu, wagombea wengine wa vyama chadema, act, cuf nk wafanye kama anavyo fanya Magu ?
Ulitaka aongee kichaga mkuu wakat huko yupo kwao hawezi kuongea kisukuma kama yupo kanda ya kazkazin
 
Anaongea kisukuma ili atimize ndoto yake ya kuifanya TZ iwe kama ulaya😀😀
 
Magufuli ni Icon ya Taifa, hao kina wenje, tundu lisu nk nk hao ni wao kama wao, magu yupo level ya kina mkapa, Jk, mwinyi na nyerere, yeye ndiye anaongoza njia hao wengine wanaiga tu, taifa likiingia kwenye ukabila au udini hataulizwa wenje wala lisu naomba uelewe hivyo. Anaetakiwa kukemea hayo ni yeye, sasa hebu niambie wabunge wote zaidi ya 300 kila mtu afanye kampeni kwa lugha yake nini hatma yake ?

Una point katika hili, lakini jee umewahi kuskiiliza lugha zinazo tumika na wabunge kwenye kampeni pembezoni wa nchi ?
 
Back
Top Bottom