Uchaguzi 2020 Hili la Dkt. Magufuli kutumia kisukuma kwenye kampeni siafiki



Hujui Yeye ni Rais wa wasukuma ???.
au wasukuma sio watu??
 
WAKIFANYA HIVYO WATAKATWA MARA MOJA KWA KUENDEKEZA UBAGUZI WA UKABILA
 
Wagombea wengine ni wastaarabu kwa hiyo waelewa kuwa nchi hii ina makabila 120 kila kabila na lughà yake. Rais wetu mpendwa ni Musukuma asiyejua lughà nyingine yeyote hata alipokuwa mwalimu alipangiwa afundishe hukohuko Usukumani. Hii imempa shida sana katika uteuzi wa watumishi wa Serikali ikambidi ateue na kutengua mara kwa mara akiwazungusha Wasukuma haohao kama Temi wa huko.
 
JPM tangu mwaka 2015 amekuwa akitumia lugha za makabila mbalimbali kusalimia hadhara anayo hutubia. Shinyanga ni Wasukuma asilimia kubwa hivyo kuchomekea Kisukuma inaruhusuwa. Sijui kwamba unaelewa neno kung'atuka lilikuwaje neno la kitaifa.

JPM mtamuelewa tu, si mtu wakuboresha kingereza chake kwa kuangalia movies za Kinaigeria ana mambo mengine muhimu zaidi ya utumishi wake kwa Watanzania Ana karama ya kujiamini kwa kile anachofanya.
 
Huu ni upuuzi ambao umeanza kurejea kwa kasi ktk awamu hii, badala ya kwenda mbele, tunajirudisha nyuma kwa kasi.

Vv
 
La kutumia kisukuma liko Sawa ,lengo massage ifike barabara kwa wahusika ,kuna baadhi huwa hata kiswahili hawajui
 
Unapinga Jambo gumu mno mkuu, ni Sawa na mha akutane na mha mweziwe halafu eti wasiongee kiha??

Wapi na wapi?
 
Ni kwao na ana Uhuru wa kuongea na wakwao Cha mhimu tusifanye makosa NI YEYE2020
 
Kwani Singida ameshafanya kampeni tayari nijuavyo alianzia Dar....Arusha...Mwanza..shinyanga na leo Tabora
Ubaya wa kuongea kilugha ni pale mtu anapofanya Kampeni pekee siyo?

Huna ukijuacho kuhusu unachokikemea
 
Hahaha mwacheni aongee tu, watoto wa primary school anaojaziwa kwenye kampeni wengi kiswahili hawakijui vile vile.
 
Ulimuuliza tundu lisu alipokuwa kwao wakati, kusaka wadhamini
 
wabongo bana kukosoa tu kila kitu... kuna shida gani kutumia kisukuma? sasa kama kautana na watu wa kwao unataka aongee kiswahili?
Una uwezo finyu wa kufikiri, la, una ushabiki wa kupitiliza. Katika Tanzania ya leo hakuna mahala kukuta kabila moja tu, tumechanganyikana sana. Matangazo hayo huoneshwa kwa watanzania wengi. Penye uhitaji wa ukabila ni vizuri isioneshwe live.
 
Ulimsikiliza Msaliti Lissu akitafuta wadhamini pale Ikungi?? Acha kubwabwaja!
 
Una uwezo finyu wa kufikiri, la, una ushabiki wa kupitiliza. Katika Tanzania ya leo hakuna mahala kukuta kabila moja tu, tumechanganyikana sana. Matangazo hayo huoneshwa kwa watanzania wengi. Penye uhitaji wa ukabila ni vizuri isioneshwe live.
Wewe inaonekana hujui lugha ya kwenu.
 
Huyu bwana huwa anatumia kisukuma ili kiwahadaa watu kuwa yeye ni msukuma wakati kila mtu hapo chato analijua kabila lake halisi ila wanamsifu kwa jinsi alivyoweza kuishi vizuri na baba yake wa kambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…