Hili la kuhusu usalama wa pesa za pensheni za Wastaafu limekaaje?

Hili la kuhusu usalama wa pesa za pensheni za Wastaafu limekaaje?

Aladeen04

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2016
Posts
3,524
Reaction score
5,731
Heri ya nanenane kwenu nyote mtakaopitia uzi huu.

Ndugu zangu kwa sasa wazee wetu wastaafu wanapitia suala gumu sana linalohusiana na kikokotoo malalamiko yapo kila pahala.

Nina imani Serikali yetu sikivu inasikia na inafanyia kazi jambo hilo ili wazee wetu wapate stahiki zao zote bila kutunziwa tena.

Tatizo kubwa ni kuhusu wastaafu wetu hawa kupigiwa simu ambazo zina viashiria vya utapeli wakiambiwa kuwa wenzao wamepata pesa zaidi na mhusika ambaye kapigiwa simu inaonekana kapewa pesa kidogo na kabaki yeye tu miongoni mwa waliopata pesa za kustaafu (Pension).

Ni kwanini wapigiwe wao kwa namba zao na si watu ambao siyo wastaafu?

Uaminifu uko wapi kwa mamlaka zinazohusika juu ya usalama wa pesa kidogo wanazopata wazee wetu?

Hii imekaaje?
 
Proposal imepelekwa wanataka iwe 50-50 na sio 33-67
 
Hiki kikokoto ni Wiz Tuu , Mtu apew chake[emoji39]

Age of 60 unapew robo baada ya miak 10 mbele upew TENA [emoji3526][emoji613][emoji880]
 
Back
Top Bottom