Hili la Kutaka Ma Bus yote yaingie MAGUFULI BUS TERMINAL , ningekupongeza bwana Chalamila

Hili la Kutaka Ma Bus yote yaingie MAGUFULI BUS TERMINAL , ningekupongeza bwana Chalamila

Nilitarajia ungeanza na ushauri wa kuondoa malori ambapo Dar yote imekuwa ICD sababu bi hatari mno yale malori yanapopita na kontena na kusababisha pia foleni. Mimi niombe sana Serikali ilitazame hili la mabasi maana abiria tunateseka mfano mtu kwa sasa ambaye anaishi sinza au Tabata au Magomeni anaposhuka Ubungu ,Shekilango moja anakuwa amepata msaada mkubwa mno wa kumuwezehsa kufika kwake . Fikiria Mbezi kulivyo mbali mtu anakwenda pengine Kigamboni ni kumuongezea garama ya nauli.Mimi niombe serikali iangalie hizi ICDs na changamoto ya malori. Mabasi sioni tatizo kwani asilimia kubwa yanafanya kazi usiku na pia hata yatoke wapi huwa yanaingia hapo mbezi.
Watu tulikua tunatoka mbagala kwenda ubungo kupanda bus za mikoani na hapakua na bus za mwendokasi,mbezi kuna bus za mwendokasi hadi kivukoni/gerezani,acheni kudeka,hizo kampuni ziwe na huduma za shuttle
 
Usijilinganishe na watu masikini, utabaki na umakini wako hadi kufa.
Kama Morocco
Screenshot_20260818-104744~2.jpg
 
Hili la mabus yote kuanzia mbezi ni shida nyingine.
Kuna siku nikasema ngoja nipande bus kwenda moro nikapandia shekilango tukapelekwa mbezi. Nikaenda chooni, mpokea hela anasema maji hamna. Kwahiyo ukitaka kujisaidia ununue maji dukani halafu ulipe tena kuingia chooni. Vyoo ni vichafu havina mfano. Nikajuta ningejua ningejisaidia palepale shekilango.
Viongozi waache usumbufu.
Jiji la dar ni kubwa kulazimisha watu wote kwenda mbezi ni unyanyasaji kwa abiria. Mara 100000 stand ilivyokuaga ubungo.
 
Lengo la huduma ni kurahisisha maisha ya watu. Hilo weka akilini.

Kutumia gharama kujenga huduma fulani sio kigezo cha kuwatesa watu.

Elimu na Akili zipo kwaajili ya kusaidia kurahisisha maisha ya mwanadamu. Hiyo ndio akili na elimu.

Mtu yupo Bunju akapande gari Mbezi Magufuli kisa ilijengwa kwa gharama?

Kama ishu ni Watu wapande kwenye stendi rasmi. Hilo ni muhimu.
Utaratibu unaweza kuwekwa.
Kuna stendi ya Mwenge Pale. Inaweza kukava watu wanaotokea Sinza na Bagamoyo road. Ingawaje Tegeta pangetakiwa pawe na stendi hata kama ni ndogo kama ya Mwenge.
Kisha Mbagala,

Ukitoa tuu matamko na amri bila kuangalia shida na mahitaji ya wananchi unakosa sifa ya uongozi
💯
 
Back
Top Bottom