Hili la kuwatoza wageni Dola 100 ili kuwasajili lina ukakasi.

Hili la kuwatoza wageni Dola 100 ili kuwasajili lina ukakasi.

gmosha48

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
2,399
Reaction score
1,481
Nimeona kwenye gazeti tangazo kutoka NIDA, linalotaka wageni wakaazi halali kwenda kusajiliwa. Sina uhakika sana na nia ya usajili huu, lakini kuna jambo moja lipo wazi. NIDA wanataka kukusanya hela kupitia mchakato huu. Cha kujiuliza, kama wageni walifuata taratibu zote halali za kuingia nchini, ikiwepo kulipia viza na vibali vya kufanya kazi, hizi fedha wanazotaka NIDA ni za nini? Kwa nini gharama zote zisijumuishwe kwenye mchakato mmoja?

Naunga mkono jitahada zote za kuzuia wahamiaji haramu, ila kwa wale wanaoingia kwa kufuata taratibu sii sahihi kuwatisha mizigo na kuwapitisha katika longo longo zisizokuwa na maana. Uwepo wa wageni Tanzania kihalali una manufaa makubwa kiuchumi. Tusijidanganye, nchi nyingine wanafanya jitihada za makusudi kuvutia wageni wengi nchini mwao. Taratibu zinarahisishwa na zinatabirika. Sisi kila uchwao tunaibuka na vitu ambavyo ni kama vinawakataza wageni kuishi au kutembelea Tanzania.
 
Back
Top Bottom