Hili la Makonda kuruhusu bodaboda kuingia katikati ya jiji la Dar es salaam linafikirisha sana kwa hawa wanasiasa wetu

Tripo9

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2009
Posts
4,357
Reaction score
3,550
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza

Makonda karuhusu boda ziingie katikati ya jiji. Zuio hili hapo mwanzoni bila shaka lilikua na maana yake pana na imekua kawaida na imekua kama sheria boda boda haziingii katikati ya jiji.

Nimezumguuka miji kadhaa mikubwa hua hiki ni kitu wenzetu wengine wanafanya.

Jamani hata kama ni hizi danganya toto za watu kutaka kura zimezidi mpaka kupindua sheria?

Mimi I'm fine mtu agawe pilau watu wale, mtu awajazie boda boda wese ili azunguke nao kwa kampeni sababu hapo hakuna sheria inayovunjwa. By the way hata mtu agawe buku saba saba kwani vepee. Sawa tu. Chukua buku saba ikifika kwenye kura mpige chini mwanasiasa aliyekupa buku zake saba. Kwani atakuona.

Kwanza hiyo buku saba itakua inabadilishwa jina rightly so kutoka kua rushwa mpaka kua takrima na maisha mbona yanaenda hakuna anaekamatwa,

Shida ni hapa tunapoamua kucheza na vitu ambavyo ni kama sheria tayari na kuvitumia kama political stunt. Jamani sheria hazipinduliwi hivyo. Huu uchaguzi utapita halafu tunavowajua hamna hata haya za uso mtarudi kwenye utaratibu wa kawaida tunawajua nyinyi.

Hii nchi hii mpaka hasira yaani.

Sio kila kitu Cha kupinga na kuweka ushabiki, kuruhusu bajaji na bodaboda ulikuwa ni uamuzi sahihi katika kipindi Cha Korona ili kurahisisha usafirishaji na kupunguza msongamano mkubwa wa watu vituoni na kupelekea kuchelewa kwenye majukumu yao.
 
Mkuu umesoma kweli mada na kuielewa au umesoma tu?? Mleta mada kasema mambo mawili

a) kulikuwa na sheria iliyopitisha katazo hilo. Sheria hiyo itenguliwe na bodaboda ziingie mjini, la sivo baada ya uchaguzi bodaboda zitazuiliwa tena.

b) ni kwa manufaa ya siasa. Makonda si chombo cha uamuzi wa jambo hili. Na wala si yeye aliyeweka zuio hilo kwanza, inakuwaje analiondoa?? Jiji likiamua kukamata watu na kuwatoza faini, watakuwa wamekosea?

Mkuu, bado unataja corona ambayo mnasema haipo? Nini ushahidi wa kuwa kuna corona na bodaboda zinahitajika??
 
Sio kila kitu Cha kupinga na kuweka ushabiki, kuruhusu bajaji na bodaboda ulikuwa ni uamuzi sahihi katika kipindi Cha Korona ili kurahisisha usafirishaji na kupunguza msongamano mkubwa wa watu vituoni na kupelekea kuchelewa kwenye majukumu yao.

Corona imeanza wiki hii? Si imepungua tayari? Bado mnafanya siasa za kipuuzi za kusaka kura kwa kuhadaa wananchi?
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza
Makonda karuhusu boda ziingie katikati ya jiji. Zuio hili hapo mwanzoni bila shaka lilikua namaana yake pana na imekua kawaida na imekua kama sheria boda boda haziingii katikati ya jiji.
Nimezumguuka miji kadhaa mikubwa hua hiki ni kitu wenzetu wengine wanafanya.
Jamani hata kama ni hizi danganya toto za watu kutaka kura zimezidi mpaka kupindua sheria?
Mimi I'm fine mtu agawe pilau watu wale, mtu awajazie boda boda wese ili azunguke nao kwa kampeni sababu hapo hakuna sheria inayovunjwa. By the way hata mtu agawe buku saba saba kwani vepee. Sawa tu. Chukua buku saba ikifika kwenye kura mpige chini mwanasiasa aliyekupa buku zake saba. Kwani atakuona.
Kwanza hiyo buku saba itakua inabadilishwa jina rightly so kutoka kua rushwa mpaka kua takrima na maisha mbona yanaenda hakuna anaekamatwa,
Shida ni hapa tunapoamua kucheza na vitu ambavyo ni kama sheria tayari na kuvitumia kama political stunt. Jamani sheria hazipinduliwi hivyo. Huu uchaguzi utapita halafu tunavowajua hamna hata haya za uso mtarudi kwenye utaratibu wa kawaida tunawajua nyinyi. Mshipa wa aibu hamna K++%##na zenu.
Hii nchi hii mpaka hasira yaani.
Siasa babu anatafuta mtaji wa watu si unajua bado kidogo?
 
Corona imeanza wiki hii? Si imepungua tayari? Bado mnafanya siasa za kipuuzi za kusaka kura kwa kuhadaa wananchi?
Siasa zitakutia stress mwanangu muda mwengine jaribu kurelax tu.
 
Mbona nimerelax sana mwana. Au unakonda nini?
Mwana kila nikiona comment yako kwenye masuala ya siasa uko vere siriaz,huwa najiuliza hivi mwana huwa anapata muda wa kufurahi kweli.
 
Sio kila kitu Cha kupinga na kuweka ushabiki, kuruhusu bajaji na bodaboda ulikuwa ni uamuzi sahihi katika kipindi Cha Korona ili kurahisisha usafirishaji na kupunguza msongamano mkubwa wa watu vituoni na kupelekea kuchelewa kwenye majukumu yao.
Tanzania hamna corona mbona inaenda kinyume na magufuli
 
Mwana kila nikiona comment yako kwenye masuala ya siasa uko vere siriaz,huwa najiuliza hivi mwana huwa anapata muda wa kufurahi kweli.

Muhuni wangu kwangu kwenye siasa ndio ninakopatia raha. Ukinitoa humu ndio nakosa raha.
 
Unauliza hirizi Tanga!
Ila nakubali,kwa sababu wakati mwengine unakuta watu muda wote wanaeleza malalamiko tu jinsi wanavyonyanyaswa yani muda wote wao hawana zuri wao. Unaweza kuona wanaeleza hayo kwa sababu wanachukizwa nayo ila nilichogundua ni kwa wamekuwa wakiyapenda hayo na yasipofanyika hawaoni raha kabisa.
 
hasira kivipi na waeznio nao wanatafuta ugali wao. wavae helmet tu muhim na wasichomekee barabaran
 
Back
Top Bottom