Kwani halmashauri safari hii na wenyewe watatakiwa wapeleke gawio, maana sasa serikali badala ya kutunga sera, kukusanya kodi na kutoa hudumu inajikuta inafanya hadi biashara ndogo ndogo za mama ntilie. Juzi juzi watu walikuwa wanauliza kwa nini kampuni za serikali kama TPDC na STAMICO kwa miaka mingi zimeshindwa kuvumbua na kuendesha uchimbaji wa madini, gesi na mafuta hadi mabeberu ndo waje wafanye na kutuachia mashimo na ile asilimia 4...