Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
atajulia wapi yeye hata kinyesi chake kikinuka anaitaja chademaUnajua madhara ya wakulima kukosa mbolea kwa wakati?
unajua maana ya kuwajibika lakini?Chadema imepoteza wabunge kutoka 100 hadi 1 lakini Mbowe hajawajibika alafu unakuja kuhangaika na waziri mchapakazi Bashe?
Kwa maoni yako wewe unataka Bashe awajibike kwa lipi? Maana kwa mwaka huu Wakulima wengi wamenufaika na mbolea ya ruzuku kuliko miaka iliopita kinachotakiwa ni maboresho madogomadogo ya hapa na pale
Unayajua yanayoendelea kwenye Mbolea ya Ruzuku au unataka kuzungumza mambo usiyafahamu kwa sababu unanufaika na uwaziri wa Bashe?Kwa maoni yako wewe unataka Bashe awajibike kwa lipi? Maana kwa mwaka huu Wakulima wengi wamenufaika na mbolea ya ruzuku kuliko miaka iliopita kinachotakiwa ni maboresho madogomadogo ya hapa na pale...
Usionge kijumla jumla izo mbolea zilizofichwa zipo wapi na wewe uliezigundua kwa nini usizifichue?Unayajua yanayoendelea kwenye Mbolea ya Ruzuku au unataka kuzungumza mambo usiyafahamu kwa sababu unanufaika na uwaziri wa Bashe?
Hivi unajua kuna wakulima hadi leo wamejisajili majina yao kwenye Serikali za Vijiji na Kata tangu Agosti mwaka jana na hadi leo msimu unakaribia kuisha wa kilimo hawajapata mbolea?
Hivi unajua kuna mbolea za ruzuku zililengwa kupelekwa kwa wakulima lakini zimefichwa na kutoroshwa kwenda kuuzwa nje ya nchi na kuwatajirisha wakubwa na sio kuwanufaisha wakulima wa Tanzania?
Labda nikwambie kitu kimoja ndugu yangu usifikiri labda nabisha kuwa akuna changamoto changamoto ndogondogo zipo nyingine zinashughulikiwe na nyingine ndio tunataka Serikali izishughulikie
Ili mbona nikwambia toka mwanzo kuwa ni usumbufu Mawakala kuwa mbali na vijiji na kumzidishia gharama Mkulima ila baada ya hizo nenda rudi Wakulima wote wanapata mbolea na ndio maana tunataka hiyo changamoto iondolewe kila mwenye uwezo wa kuuza mbolea auze yasiwe maduka ya pembejeo peke yake
Hii ni hulka ya Watanzania wengi sio waaminifu hawa wametenda kosa wamekamatwa hapa Bashe kosa lake nini?
Unajua sababu ya kuwepo mbolea ys ruzuku?Usionge kijumla jumla izo mbolea zilizofichwa zipo wapi na wewe uliezigundua kwa nini usizifichue?
Kuhusu baadhi ya Wakulima kukosa mbolea kwa wakati ni kweli maana mpaka sasa mbolea bado zinauzwa kwenye maduka ya pembejeo na hao waliokosa wakienda watapata
Changamoto kubwa ninayoiona Mawakala ni wachache mwakani waboreshe Mawakala wawepo mpaka vijijini yoyote mwenye uwezo wa kuuza mbolea apewe kibali isiwe lazima mpaka liwe duka la pembejeo
Tunapoongea umu sio lazima uwe mnufaika au muathirika muhimu uongee kitu cha ukweli na ambacho una uhakika nacho usiongee kwa ajili ya chuki,fitna,majingu nk
Wewe kama Mkulima sema haki mwaka huu na miaka iliopita ni wakati gani Mkulima ananufaika na mbolea ya rukuzu? Mwaka huu ukiitaji mifuko 20,30 nakuendelea unapata yote tofauti na kipindi kilichopita unataka mifuko 10 unapewa2 au unaambiwa imeisha kabisa
Mwaka huu changamoto kubwa nilioina ni kuchelewa kwa baadhi ya Wakulima kupata mbolea na Umbali wa maduka ya Mawakala yalipo na vijiji mambo hayo kwa maoni yangu ndio tuitake Serikali iyashughulikie kwa wakati ili mwakani yasijitokeze
Ila mnyonge mnyongeni haki yake mpeni kwa kiasi kikubwa tumeyaona mabadilko makubwa katika upatikanaji wa mbolea na kama hizi changamoto chache zilizojitokeza zikishughulikiwa itapatikana nafuu kubwa kwa Mkulima
Mbolea hii ya ruzuku imewekwa msimu huu kwa kuwa bei ilipanda Sana. Hiyo miaka mingine hakukua na hili la ruzuku. Sasa unaposema miaka iliyopita unamaanisha nn?Labda nikwambie kitu kimoja ndugu yangu usifikiri labda nabisha kuwa akuna changamoto changamoto ndogondogo zipo nyingine zinashughulikiwe na nyingine ndio tunataka Serikali izishughulikie
Swala hilo la nenda rudi na tatizo nimeshakuambia Mawakala kuwa mbali na vijiji ila baada ya nenda rudi mwisho wa siku mbolea unapata
Kuhusu wizi sijui Bashe ndio kaiba!!! Baadhi ya Mawakala wasiowaaminifu wamefanya hayo na Serikali imewakamata na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao sasa sijui hapo wewe unalaumu nini na unataka Serikali ifanyeje?
Nimekwambia toka mwanzo kuwa changamoto ndogondogo zipo na inabidi zitatuliwe na nimekwambia kuwa uuzwaji wa Mbolea mwaka huu ni mzuri kuliko miaka iliopita maana ukiachilia hizo kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza ila Mkulima akipata mbolea anapata yote anayoihitaji hata kama kwa siku hiyo itakuwa aijatimia ataambiwe aje siku nyingine aimalizie
Sasa wewe unaetaka Bashe awajibike sijui unataka Bashe awajibike kwa lipi? Na kwa maoni yako unaona Bashe anafaya vibaya kuliko Mawaziri watatu wa Kilimo waliopita?