Hili la mchujo kidato cha kwanza limekaaje.?

Hili la mchujo kidato cha kwanza limekaaje.?

Njangula

Senior Member
Joined
Oct 20, 2011
Posts
179
Reaction score
18
Ndugu wanajamvi JF, wizara ya elimu imetoa maagizo ufanywe mtihani kuwatahini waanafunzi wa kidato chaa kwanza 2013 ili watakaofeli wachujwe. Pia tumeambiwa kuwa mitihani na marking schemes italetwa mashuleni. Pia mitihani ifanywe Jumatatu 11 na kusahihishwa mashuleni. Cha kushangaza tunatumiwa habarii kuwa mtihani na marking scheme vipo website ya wizara, hivyo tudownload na kuzalisha nakala za kututosha. Sasa je kuna umuhimu wa huo mtihani? Na kama ndio, je lengo la huo mtihani ni nini? Nawasilisha.
 
Whaat? Kwani si wanafanya mtihani wa darasa la saba au?
 
Nilitarajia ya kwamba kutakuwa na kurudia mtihani wa taifa kwa wanafunzi wote waliofaulu.
Ila juu wa sasa una utata.........utafanyika Jumatau.....kusahihishwa mashuleni....mtihani na marking scheme vipo kwenye website ya Wizara.....tudownload na kuzalisha nakala za kutosha.
Hii ni kali kuliko, naona kanuni za mitihani ya taifa zimebadilishwa kabisa kwa Tanzania pekee. Hii itakuwa kila mwaka, tusubiri mengi zaidi
 
Mkuu wao bado ana stress,
Unadhani ile hoja binafsi mchezo?
 
teh unajua jamani kuna matukio yanayotokea hapa tz nadhani hakuna pengine popote utakaa usikie, yaani kabila la wakwere nadhani hawafai hata kuwa mamonita wa darasa. Ni mtazamo wangu.
 
haaa hii sasa kali marking scheme kwenye website na watoto wa siku hizi wanavyojua facebook kama wamesikia watazama kwenye mtandao wadownload nao hiyo marking scheme halafu wafaulu saaaana
 
Mbona mwaka jana walifanya huo mtihani na ambao walibainika hawajui kusoma wala kuandika wanadunda bado wameingia form 2
 
Ndugu wanajamvi JF, wizara ya elimu imetoa maagizo ufanywe mtihani kuwatahini waanafunzi wa kidato chaa kwanza 2013 ili watakaofeli wachujwe. Pia tumeambiwa kuwa mitihani na marking schemes italetwa mashuleni. Pia mitihani ifanywe Jumatatu 11 na kusahihishwa mashuleni. Cha kushangaza tunatumiwa habarii kuwa mtihani na marking scheme vipo website ya wizara, hivyo tudownload na kuzalisha nakala za kututosha. Sasa je kuna umuhimu wa huo mtihani? Na kama ndio, je lengo la huo mtihani ni nini? Nawasilisha.

kama hakuna posho mtakayolipwa usisimamie mkuu huo mtihani ni feaki kwani haupo popote katika taratibu!!jiulize bilioni ngapi zimetumika kwa ajili ya mtihani wa darasa la saba uliopita?huu tena ni nini?tulisema hapa hali mbaya watoto wamefeli sana matokeo yake akaja waziri na kujitapa ufaulu umeongezeka,Mbona la kurudia asiite waandish iwa habari?
 
teh unajua jamani kuna matukio yanayotokea hapa tz nadhani hakuna pengine popote utakaa usikie, yaani kabila la wakwere nadhani hawafai hata kuwa mamonita wa darasa. Ni mtazamo wangu.

kabla lako ndo hamkupaswa kuwepo hata duniani acha hao wa umonita darasani
 
K3 ambazo zilikuwa zikipimwa drs la4 leo zinapimwa drs la9 ..ama kweli hiki ndo ccm wanachojivunia miaka 50 ya uhuru
 
tetesi, wasimamizi ni mkuu na mwingine atakaye mteuwa yeye na malipo ni 45 elfu @ ,
 
Mkuu unasema mtihani na marking scheme viko website ya wizara???
dah kaazi kweli kweli.....
 
kaka wizara yako haina wataalamu, kitendo cha kusema watoto washedi jibu sahihi ni kusababisha watoto kufaulu bila kujua kusoma na kuandika. sasa huo mtihani wanini kama NECTA wmeshindwa kazi kwanini wawaletee huo mzigo? ooo Tanzania ipo siku tutabadili lugha ili tuelewane maana watoto wao wanosoma nje na kwenye shule zinazoanza na St. ambazo mtoto wa mkulima si rahisi kusoma.
 
Da? inamaana wameshindwa kabisa kutoa wanafunzi wenye sifa darasa la saba mpaka waweke mtihani mwingine form one. ni matumizi mabaya ya raslimali watu, pesa pamoja na muda
 
Back
Top Bottom