Ndugu wanajamvi JF, wizara ya elimu imetoa maagizo ufanywe mtihani kuwatahini waanafunzi wa kidato chaa kwanza 2013 ili watakaofeli wachujwe. Pia tumeambiwa kuwa mitihani na marking schemes italetwa mashuleni. Pia mitihani ifanywe Jumatatu 11 na kusahihishwa mashuleni. Cha kushangaza tunatumiwa habarii kuwa mtihani na marking scheme vipo website ya wizara, hivyo tudownload na kuzalisha nakala za kututosha. Sasa je kuna umuhimu wa huo mtihani? Na kama ndio, je lengo la huo mtihani ni nini? Nawasilisha.