Msitari wa pambizo
JF-Expert Member
- Sep 25, 2014
- 3,098
- 5,451
Katika harakati za kudai na kukumbusha katiba mpya suala la mgombea binafsi haliungumzwi kabisa. Si CHADEMA, ACT, CCM au chama chochote cha siasa wa kulisemea hili.
Hii ni kwa sababu wote wanaangalia maslahi yao hivyo hawawez kulipigania hili. Sisi ambao tungetamani sura halisi ya uwakilishi ambao si lazima uwe na mwavuli wa chama cha siasa ndio pekee tunaweza kulisemea hili.
Tunaomba tena jambo hili lipewe uzito mkubwa katika katiba mpya kwa sababu dhana ya uwakilishi ni makubalino ya wananchi na mwakilishi wao wala sioni sababu ya kuwepo ulazima wa chama cha siasa kusimama katikati hapo.
Tupaze sauti tunataka haki ya kuwakilishwa na mtu na sio chama cha siasa.
Wananchi tunataka mgombea binafsi ili kutoa fursa kwa watu wenye uwezo kujisimamia na kuendesha siasa ktk nchi yao kwa uhuru bila kufungwa na chama cha siasa.