Hili la Mugalu kutolipwa fedha zake za tuzo lina ukweli gani wadau? Bodi ya Ligi ina cha kujibu

Hili la Mugalu kutolipwa fedha zake za tuzo lina ukweli gani wadau? Bodi ya Ligi ina cha kujibu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Asubuhi ya leo nimeamka na taarifa niliyoikuta mitandaoni kuwa Bodi ya Ligi inayosimamia Ligi Kuu kwamba haijamlipa mshambuliaji wa Simba, Chriss Mugalu fedha zake za Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu.

Nimejaribu kupekenyua sijajua hasa ni ipi inayozungumzia lakini niliyoiona labda ni ile tuzo ya Julai mwaka jana.

Sasa wadau ninachojiuliza, taarifa hiyo ambayo nilianza kuona imefichuliwa na Ricardo Momo wa Wasafi FM, hivi ina ukweli na kama kweli kwa nini mpunga huo haujatolewa hadi leo?

Inamaana wadhamini wa tuzo hiyo hawajatoa mkwanja au ni makusudi tu, hivi lipoje hili wadau?

mugalu-2-1024x682.jpg
 
Asubuhi ya leo nimeamka na taarifa niliyoikuta mitandaoni kuwa Bodi ya Ligi inayosimamia Ligi Kuu kwamba haijamlipa mshambuliaji wa Simba, Chriss Mugalu fedha zake za Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu...
Unaweza ukatuwekea source ya taarifa yako hii!?
 
Unaweza ukatuwekea source ya taarifa yako hii!?
Nimeandika hapo mzee baba, ngoja ninukuu nilichoandika: "Sasa wadau ninachojiuliza, taarifa hiyo ambayo nilianza kuona imefichuliwa na Ricardo Momo wa Wasafi FM, hivi ina ukweli na kama kweli kwa nini mpunga huo haujatolewa hadi leo?"
 
Ni ya toka msimu uliopita au mwezi gani huo?
 
Nimeandika hapo mzee baba, ngoja ninukuu nilichoandika: "Sasa wadau ninachojiuliza, taarifa hiyo ambayo nilianza kuona imefichuliwa na Ricardo Momo wa Wasafi FM, hivi ina ukweli na kama kweli kwa nini mpunga huo haujatolewa hadi leo?"
Kwahiyo weka link hapa. Tofauti na source wewe ni mbea mithili ya mbulukenge.
 
Aliyempa uchezaji bora huyo atakuwa na tatizo la Afya ya akili

Na ndiyo maana mpaka leo bado wana mzungusha. Inawezekana ni baada ya akili zao kukaa sawa, wakabakia tu kujishangaa na kujilaumu.
 
Nchi ya hovyo sana hii, hivi huyu nae amewahi kuwa mchezaji bora wa mwezi?😀, dah....
 
Itasikitisha sana endapo hizi taarifa zitakua na ukweli...
 
Back
Top Bottom