Hili la NBC Je Huu si Udini Jamani?

Utakuwa una CHUKI zako binafsi juu ya uislamu...tafsiri yako ndio inaleta udini
 
Crdb wametoa mkopo wa uwekezaji tena kwa riba. Nafikiri siyo kosa kuwakopesha wakristo ambao wao wako tayati kulipia riba. Je ni kosa kwa wakristo kukopa?
 
NA je CRDB kuwamwagia mapesa wakatoliki kujenga kitega uchumi pale Msasani huoni huo nao ni udini? Acheni uchochezi nyie! wakifanyiwa maprotestants ni sawa waislamu udini?! mna kazi kweli kweli !

Wakatoliki wamekopa na watalipa kwa riba kama wateja wengine wanaokopa bank. Suala ni kuwaelewesha watu juu ISLAMIC BANKING jinsi inavyofanya kazi. Msichukulie kila jambo ni udini acheni upuuzi huu..
 
Hayo ni mambo ya kibiashara, unajua katika unaangaia zaidi fursa.
 
Lakini wao jamaa wa NBC hawaoni athari ya hii promotion? Ahsante
Mh.EH, Maajabu kuwa mfumo wa benki yeyote huwa zinatamaa na kukubali fedha(pesa za aina yote) bila kujali halisi/asili yake...kwao ilimradi wanyakuwe kwa sabubu Benki hujiendesha kwa masilahi yake kabla faida mtjeja wake. Kuhusu njia ya kuwanasa waisilamu kwa njia ya matangazo, Lengo lao nikuwakusanya wateja kwa wingi na wao kufaidika ....

Mara nyingi Kwa waisilamu huwa hawajali ADV. yasiyoathiri itikadi au imani..KM.wao hutumia sarafu za (dola $,Poundi,euro nk) hata kama zina alama ya msalaba hiyo haijalishi au kupanda ndege zenye misalaba kama vile Swissair!! kwa hiyo NBC inatambua potensho ya wateja wakiislamu wanajua kula nao!! kwa upande wa wasio wasilamu mie sina comment impact gani itafuatia.... after all hizi ni common interest wote kuna manufaa.
 

uislamu ni dini iliyokamilika kuanzia banking .kuchinja.jinSi ya kuvaa nguo .marriage.dealing wid corruption.how to do wid ufisadi.science. and technology na yote unayOyajua.. xo usihamaki Sio udini ni mfumo uliokamilika.
 

kuna mwingine atakuja kulala mikia ukabila sasa..
 
Sipendi mijadala ya kidini hasa kwa kuwa napenda kuheshimu uhuru wa mtu binafsi kuabudu. Lakini sipendi vilevile kushirikishwa kwa namna yoyote ibada za watu wengine hasa zisizoniingia akilini.

Ni hivi, niliwahi kuwa na NBC personal account kwa muda mrefu sana, ni wakati m1 hivi jamaa yangu mmoja alinikuta najaza cheque deposit slip ananionesha ile chata ya "ISLAMIC BANKING", chini kushoto, najiuliza hivi ni lazima kuweka viashiria vya kidini kwenye kila kitu? Tangu siku hiyo nilifreeze account yangu kule.

Namshukuru MUNGU kwa kutuwezesha kuanzisha benki yetu ya MKOMBOZI COMMERCIAL BANK = the bank with integrity. Ndo niliko sasa na sitoki kamwe!
 
Mleta mada unaugua.Udin wako usiwafikirie nawenzako wapo hivyo.Kaa tafakar ndipo uandike.Umetoka kwenye mvinyo.Huna maana.
 
Tafadhali futa kauli yako pale msasani si wakatoliki ni KKKT, nyie watu mna tatizo gani na wakatoliki, mkristo akifanya lolote mnarukia ukatoliki tu

we acha ukatoliki unawasumbua sana
 
Usijibu kwa hamaki mheshimiwa. Unajua NBC wana watu wa media wanaofuatilia kurasa kama hizi , hivyo maoni ya wachangiaji yanaweza kuwafumbua macho. Ahsante

Sijakujibu kwa hamaki!

Nadhani mpaka sasa umeona kuwa wachangiaji wengi wanakubaliana na mimi kuwa thread hii lengo ni kuleta chokochoko za udini. Kitu ambacho ni chanzo cha mtafaruku nchi za wengine.

Tuna waanzisha fujo wengi mno nchini ambao tatizo kubwa walilonalo ni uchache wa elimu. Na kuwaelimisha hawa ni kazi ya ziada.

Sidhani kama tunahitaji wengine wapya!
 
Tafadhali futa kauli yako pale msasani si wakatoliki ni KKKT, nyie watu mna tatizo gani na wakatoliki, mkristo akifanya lolote mnarukia ukatoliki tu

Amekosea kusema katoliki. Namtakia radhi kwa niaba!

Alikuwa na maana ya kanisa la kikristo msasani.
 
mleta uzi unalako jambo na ndio naweza sema wewe ndio mdini manake unapoleta uzi kama huu kwenye jukwaa kama hili unataka ujumbe umfikie nani?kwanini usipeleke uhsauri wako huko waliko nbc?
 
Lugha unayotumia na jinsi unavyojibu hoja inaonekana kama kwamba hoja yangu ilielekezwa kwako au imani yako.Hebu soma hoja za KENEKAI hapo juu utaona kuna walakini katika yale yanayotendwa na NBC. Hebu nikukumbushe kwamba NBC ilianzishwa kwa fedha za WALIPA KODI wa DINI zote SASA NBC kuingiza NEMBO & Label/Chata za ISLAMIC BAKING katika Deposit Slips na Withdraw Slip bila taarifa kwa wateja wake ni hatari sana. Hebu tutumie LOGIC kidogo kwamba kesho unaenda pale CRDB , NMB au BANK nyingine yeyote ambapo wewe ni mteja halafu ukakuta Chata za kibuda, kikatholic, kilutheri au Imani yeyote bila kuwa umepewa taarifa mapema HIVI utakaa kimya. Naomba tujaribu kuwa Neutral tunapochangia mada hii.Ahsante
 
Huko unakoenda si sahihi.Naomba tuongee hapa hoja za kulijenga taifa letu na sio kulibomoa.Hayo mambo ya kuchinja yanaingiaje hapa. Kwanza naomba utambue kwamba WAISLAMU wa kweli nawaheshimu sana kwani ni waaminifu, wapole, wachapakazi, si watu wa vurugu, ni watu wanaotumia hekima sana katika kuufikisha Imani yao kwa waimani tofauti. Kwahiyo naomba utambue kwamba nilileta hoja hii si kuwashambulia watu BALI kuondoa yale yanayoweza kutufarakanisha kama watanzania. Ahsante.
uislamu ni dini iliyokamilika kuanzia banking .kuchinja.jinSi ya kuvaa nguo .marriage.dealing wid corruption.how to do wid ufisadi.science. and technology na yote unayOyajua.. xo usihamaki Sio udini ni mfumo uliokamilika.
 
acheni kuhangaika na vitu vidogo kuna ubaya gani kuwa na hiyo product. mbona tuna madhambi mengi tu lakini twaona ya wenzenu. mpoclean mpaka muwaone wenzenu wadhambi. safisheni njia zenu.
 

.........kwani Roma na Israel kuna hija !?
unajua maana ya hija ?
 

kwa hiyo kwa mtazamo wako hiyo promotion ina provoke ?
hebu lete lililo moyoni mwako unalolificha na siyo kuwayawaya bila hoja za msingi !
Wateja wanao weka pesa kwa taratibu na nidhamu ya dini ya Kiislaam (ibada) kuna tatizo gani kuwazawadia 'bakshish' ya kwenda kuhiji Makkah ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…