Hili la Ngorongoro halijaisha, tumefunika kombe

Hili la Ngorongoro halijaisha, tumefunika kombe

Kwani kuna wamasai crater?? Hata siku moja hutakaa umkute masai crater., crater kule shimoni wanaishi wanyama tuu. Wamasai wanaishi juu. Na wamasai wanalinda wanyama na hawawaui. Wamasai sio majangili
Tunapoongea crater tunamaanisha eneo lote lililo chini ya NCA (mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro).

Hata mimi nimefika Ngorongoro na nimeingia kwenye crater na najuwa ninachoongea
 
Je wakileta Wazungu utakuwa nanmsimamo sawa?

..kuna ujenzi unaofanyika ktk mbuga na hifadhi zetu ambao ni kinyume malengo ya uhifadhi.

..mgogoro kuhusu suala hilo ulikuwepo tangu wakati wa utawala wa Rais Mwinyi. Wakati huo hata hatujaingia ktk mfumo wa vyama vingi.

..Mh.Patrick Qorro mbunge wa Karatu wakati huo aliwasilisha hoja binafsi kupinga hujuma dhidi ya uhifadhi zilizoanza kuibuka wakati huo.

..mimi nampinga yeyote anayehatarisha uhai wa mbuga na hifadhi zetu za wanyama.
 
Siasa ikiwekwa pembeni- watu na wanyama kwa style ya Ngorongoro hawawezi ku co exist na kuweza kuwa wote salama. Something will have to give.
  • Wanyama wakibanwa na mifugo eco system inakuwa challenged na uwindani haramu unaongezeka, magonjwa ya mifugo yanawaingilia wanyama pori, pia mioto ya asili ya pori inabdilika maana mifugo inaweza pia introduce mimea ya kwinginepo inapotoka kupitia kinyesi.
  • ⁠kwa upande wa binadamu, ni ngumu sana kupeleka huduma za kijamii kwa makundi yanayoishi kwa kuwa scattered tena kwenye maeneo yenye hatari. Hivyo it’s hard to have your cake and eat it too. Maendeleo ya service za jamii ili wayapate hiyo namna wanavyoishi inabidi ibadilike.
Utalii wa watu asili ni utalii mpya tuelekee huko ona aborigines etc.
 
Haya ni maoni yangu mimi, kwamba;

1. Wamasai hawana shida iwapo watashirikishwa kikamilifu ktk uhifadhi wa ikolojia ya Ngorongoro na huko kwingine....

2. Shida iko serikalini hususani kwa Rais Samia Suluhu Hassan mwenyewe na wenzake huko CCM. Kwa sababu sababu za kuwahamisha wamasai ni za kinafiki, uongo na ulaghai mtupu. Wamasai wameliona hili na wakasema, HAIWEZEKANI........!!

3. Sababu hizi za kinafiki toka serikalini zinajengwa ktk msingi kwamba "wamasai wamezidi sana Ngorongoro na hivyo kuathiri ikolojia ya eneo hilo muhimu kwa utalii hivyo waondoke ili kuruhusu wanyama na uoto wa asili kushamiri tena". Lakini ukweli ukiwa ni kuwa "fukuza wamasai kisha karibisha wanaoitwa wawekezaji waendeleze eneo hilo la Ngorongoro kwa kujenga mahotel nk". Hili wamasai wameliona na ndiyo maana ya upinzani huu mkali unaoendelea huko......

4. Kwa sababu hizI za kinafiki na ulaghai mtupu zinazotolewa na serikali, usitegemee kuwa kuna mmasai mwingine ataondoka/atahama tena eneo hilo kwenda popote unless otherwise itumike nguvu ya kumwaga damu za watu hapo.......!!

5. Kama tunataka kuthibitisha kuwa mradi huu wa kuhamisha wamasai umejengwa ktk msingi wa sababu za uongo, kinafiki na ulaghai huku ukiwa na dalili ya 100% kuwa, kuna mataifa ya nje hususani ya uarabuni yamewahonga viongozi wetu (akiwemo Rais) ili kulitoa eneo hilo kwa mwekezaji huyo mhongaji wa viongozi wetu kwa sharti la kuwaondoa wenyeji wote wa eneo hilo (wamasai), tujiulize tu nani anagharamia gharama za uhamishaji huo wa wamasai kwenda Msomera Tanga (zaidi 550km) toka Ngorongoro? Kama ni serikali, bunge liliridhia mpango huo? Bajeti kiasi gani ilipitishwa na bunge kugharamia project hiyo? Lini na wapi?

6. Kama tunataka wamasai wahame Ngorongoro kwa hiari yao; Mosi, serikali iache uongo, unafiki na ulaghai kwa jamii hii. Pili, jamii yote ya kimasai wanaoishi ishirikishwe kwa uwazi kwa kutoa elimu ya kwanini ni muhimu wapungue Ngorongoro. Tatu, pendekezo lako kuwa wachaguliwe wamasai baadhi tu hususani Malaighwani, ni hapana. Hii ndicho kilicholeta shida hata mzozo kufikia hatua hii ya kuelekea umwagaji damu. Kwenye hili kila mmasai anayeishi Ngorongoro mume, mke,kijana na wazee washiriki ktk kufanya maamuzi. Kwa kuwashirikisha hawa wanaoitwa "baadhi ya wawakilishi tu", hapana kwa sababu kwa hii serikali ya kifisadi inaweza kuwahonga hao wachache ili mradi wakubaliane na matakwa ya serikali na kuipa uhalali wa kuwafanya chochote wamasai wote halafu ikitoka hapo watambe kuwa wamasai wamekubalI lakini mwisho wa siku mgogoro unarudi palepale na pengine kuwa mbaya zaidi.....

7. Zoezi hili lifanyike kwa wamasai wenyewe wote kuulizwa wanataka wasogezwe wapi. Kwa maoni yangu, Msomera Tanga ni ardhi nyingine kabisa huko yenye mazingira tofauti na waliyozoea wao. Kama lengo ni kuwatoa tu kwenye hifadhi ya Ngorongoro, ni kwanini basi wasitafutiwe maeneo ndani ya mikoa hii hii ya Arusha au Manyara ambayo ndiyo mazingora yao ya siku zote? Mbona kuna maeneo makubwa tu ktk mikoa hii hata kama baadhi wataingia mikoa ya karibu ya Dodoma na Singida......?

8. Na wakiondoka, kamwe ardhi yao asipewe mtu mwingine hususani mwaarabu kama alivyofanya Hayati Rais Ally Hassan Mwinyi kule Loliondo kwa kuwafukuza wamasai na kuwapa Waarabu. Ni kweli ardhi ibaki kuwa hifadhi kwa ajili ya uoto wa asili na wanyama tu na kwa ajili ya shughuli za utalii kwelikweli......!
 
..kuna ujenzi unaofanyika ktk mbuga na hifadhi zetu ambao ni kinyume malengo ya uhifadhi.

..mgogoro kuhusu suala hilo ulikuwepo tangu wakati wa utawala wa Rais Mwinyi. Wakati huo hata hatujaingia ktk mfumo wa vyama vingi.

..Mh.Patrick Qorro mbunge wa Karatu wakati huo aliwasilisha hoja binafsi kupinga hujuma dhidi ya uhifadhi zilizoanza kuibuka wakati huo.

..mimi nampinga yeyote anayehatarisha uhai wa mbuga na hifadhi zetu za wanyama.
Je umewahi kufanya tafiti ni wanyama kiasi gani wamepungua baada ya hayo mahoteli kujengwa mbugani?

Pili umewahi kutafiti ni revenue kiasi gani imeongezeka baada ya mahoteli hayo kujengwa??
 
Je umewahi kufanya tafiti ni wanyama kiasi gani wamepungua baada ya hayo mahoteli kujengwa mbugani?

Pili umewahi kutafiti ni revenue kiasi gani imeongezeka baada ya mahoteli hayo kujengwa??

..hilo ni jambo ambalo halihitaji utafiti kwamba mahoteli hawapaswi kujengwa ktk maeneo ambayo yamehifadhiwa na ni mapito ya wanyama.

..kuna maeneo mbadala yanayofaa kujenga mahoteli na hivyo kuongeza mapato yetu ya utalii.

..jambo lingine ni maamuzi ya Rais Samia kuchimba madini ktk mbuga ya Serengeti. Maamuzi hayo yanaonyesha kuwa Samia ni kiongozi asiye na nia ya dhati ya kulinda mbuga zetu.
 
..hilo ni jambo ambalo halihitaji utafiti kwamba mahoteli hawapaswi kujengwa ktk maeneo ambayo yamehifadhiwa na ni mapito ya wanyama.

..kuna maeneo mbadala yanayofaa kujenga mahoteli na hivyo kuongeza mapato yetu ya utalii.

..jambo lingine ni maamuzi ya Rais Samia kuchimba madini ktk mbuga ya Serengeti. Maamuzi hayo yanaonyesha kuwa Samia ni kiongozi asiye na nia ya dhati ya kulinda mbuga zetu.
Ukipata muda tafuta idadi ya Mohoteli na Campsites zilizopo Maasai Mara ambayo ni extension ya Serengeti iliyopo upande wa Kenya, halafu linganisha na idadi ya hoteli zilizoko Tanzania (Serengeti). Huku ukizingatia kuwa 3/4 ya pori ni Serengeti wakati 1/4 ndiyo Maasai Mara.

Baada ya hapo urudi hapa na majibu
 
Ukipata muda tafuta idadi ya Mohoteli na Campsites zilizopo Maasai Mara ambayo ni extension ya Serengeti iliyopo upande wa Kenya, halafu linganisha na idadi ya hoteli zilizoko Tanzania (Serengeti). Huku ukizingatia kuwa 3/4 ya pori ni Serengeti wakati 1/4 ndiyo Maasai Mara.

Baada ya hapo urudi hapa na majibu

..hatupaswi kuiga UHARIBIFU uliofanyika Maasai Mara kwa kujenga mahoteli mengi ktk hifadhi bila mpango.
 
Namalizia kwa kuuliza swali hili! Baada ya Rais Samia kuepusha shari kwa kupooza tuu kwa mtindo wa funika kombe, je, Watanzania tujifunze kuukubali ukweli wa tatizo, tutafute ufumbuzi wa kudumu wa tatizo husika, au tuendelee na huu mtindo wetu wa sasa wa kufunika kombe mwanaharamu apite?
Jibu ni rahisi.
Hakuna tatizo linalo fumbuliwa kwa "kufunika kombe."
Lakini baada ya kusema hivyo, ni vema pia niseme kuwa mfumbuzi wa tatizo wa uhakika hawezi kuwa mtu/kiongozi huyo huyo anaye funika kombe.

Umeeleza vyema sana kuhusu mkasa ule wa vikongwe. Katika maelezo yako umejaribu kufananisha; lakini mimi nasema hakuna mfanano wa karibu vile.
Hili swala la Ngorongoro, pamoja na kuwa na ukweli kuhusu mazingira ya eneo hilo; lakini pia swala hilo linaingiliwa na maslahi ya kufaidika baadhi ya watu/viongozi kutokana na uwekezaji katika eneo lenyewe, baada ya wamasai kupisha..

Mwalimu Nyerere hakuwa na maslahi katika swala la vikongwe kuuawa, mbali ya wananchi wake kupoteza uhai. Hii leo kwa Ngorongoro, Rais Samia, ambaye anapoza tu moto, kwa kulazimishwa; anahusika na analijua swala hilo katika hatua zote tokea mwanzo na katoa/kashiriki katika maamuzi ya kuwaondoa wamasai katika eneo hilo.

Kwa hiyo, niseme tu mwisho, kwamba, hapa Rais Samia hawezi kuwa mtatuzi wa kweli wa swala hili. Itabidi tuombe sana apatikane kiongozi mwenye dhati ya kweli ya kulitatua tatizo hilo kwa maslahi ya nchi nzima.
 
..hatupaswi kuiga UHARIBIFU uliofanyika Maasai Mara kwa kujenga mahoteli mengi ktk hifadhi bila mpango.
Siyo uharibifu bali ni ushindani wa kibiashara. Na hao wenye mahoteli Masai Mara ndiyo wanawalipa local NGOs na Wanaharakati uchwara kama akina Maria Sarungi ili wapinge hatua zozote za Tanzania kuongeza mahoteli.

Kwa sasa watalii wanapokuja kwenye peak season especially kushuhudia World biggest wildebeest migration, wanalala hoteli za Kenya na kuja Mto Mara kushuhudia na kupiga picha kisha wanarudi Kenya.

Tanzania haipati a right share of tourism revenue due to this landscape
 
Issue kubwa hapo Ngorongoro ni ukuaji wa population ya watu kutoka 8,000 hadi kufikia zaidi ya 100,000. Pamoja na idadi ya mifugo kuongezeka hivyo kupelekea binadamu kutafuta eneo zaidi ndani ya hifadhi kwaajili ya makazi na malisho ya mifugo yao, kitu ambacho kwa hakika ni changamoto kwenye uhifadhi wa mbuga hiyo ya Ngorongoro.

Project ya kuwaondoa wakazi wa Ngorongoro nadhani imekuwa too rapid, Serikali haijaweza kutake time kufanya research juu ya amdhara yanayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa zoezi hili, pia kushindwa kuwaandaa wananchi wake juu ya zoezi hili huku wakiendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa zoezi hili kwa maisha endelevu ya Hifadhi yetu.

Kuna madhara makubwa yanayojitokeza kwa kutizama kwa haraka tu
Ikiwa ni pamoja Na kupoteza utulivu katika hifadhi, pia kuwaondoa wananchi jamii ya wamaasai ni kupoteza kivutio cha kipekee ndani ya maisha ya Ngorongoro ambapo ni hifadhi pekee kama sitokosea ambayo inamjumuiko wa wanyama pori pamoja na binadamu kwa pamoja.

Cha muhimu kabisa serikali ingeanza kutoa elimu juu ya wananchi wa Ngorongoro kuhusu udhibiti wa idadi ya mifugo yao kulinganisha na eneo la makazi.

Pili, juu ya ongezeko la idadi ya watu na eleo linaloruhusu watu kuishi bila kuathiri ecology, dunia ya sasa elimu katika kila jambo ni muhimu kuliko kutumia nguvu bila maelewano ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza baada ya mchakato kufanyika.
Shida nyingine ni kuwaondoa masai na kumuuzia mwarabu ajenge hotels kama ni kulinda mazingira basi wakitolewa maasai wabaki wanyama tu
 
Waarabu pia watoke
Sasa Inatakiwa tuchague moja kati ya haya mawili
1. Wamasai waondoke Ibaki hifadhi ya Wanyama
2. Wanyama waondoke wabaki Wamasai

Ila kiuhalisia Wamasai ndio wameingia eneo la hifadhi (wao ndo wamevamia hifadhi)

Ila hatuwezi kuwa na wamasai wengi kwenye crater na tukawa na wanyama pia
 
Siyo uharibifu bali ni ushindani wa kibiashara. Na hao wenye mahoteli Masai Mara ndiyo wanawalipa local NGOs na Wanaharakati uchwara kama akina Maria Sarungi ili wapinge hatua zozote za Tanzania kuongeza mahoteli.

Kwa sasa watalii wanapokuja kwenye peak season especially kushuhudia World biggest wildebeest migration, wanalala hoteli za Kenya na kuja Mto Mara kushuhudia na kupiga picha kisha wanarudi Kenya.

Tanzania haipati a right share of tourism revenue due to this landscape

..mahoteli yajengwe mengi, lakini sio kwa kuhujumu na kuharibu ikolojia na uhifadhi wa mbuga zetu.

..kwa mfano, sasa hivi Mama Samia ameamua kuchimba madini ktk mbuga ya Serengeti. Je, tuwalaumu Wakenya kwa maamuzi hayo ya Mama Samia? Je, anatumika?
 
Kwani walioweka utawaratibu wa mchanganyiko mwanzo walikosea nini? Haya na sehemu zingine zilizopewa Waarabu nako kuna nini? Hii si biashara ya kujali biashara kuliko ubinadamu?
 
Ili Tanzania tupate maendeleo ya kweli ambayo ni endelevu, ni lazima tujifunze kuukubali ukweli halisi jinsi ulivyo na kukitokea tatizo, tukabiliane nao kwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo na sio kufunika kombe mwanaharamu apite.

Ngorongoro kuna tatizo, Serikali ilitaka kulitatua kibabe, Wamasai wakagoma, alichofanya Rais Samia Suluhu Hassan ni kufunika kombe tu, lakini tatizo bado lipo na linahitaji ufumbuzi wa kudumu ili tuendelee kuwa na Ngorongoro yenye maendeleo endelevu.

Kufuatia hali ya Ngorongoro ilivyokuwa tete, jambo la kwanza ni pongezi kwa Rais Samia kunusuru Ngorongoro kwa kuepusha shari kwa mtindo wa funika kombe mwanaharamu apite, kwa kupooza tu, lakini ukweli unabaki palepale, Ngorongoro kuna tatizo, tutafute suluhisho la kudumu kwa kuwatendea haki wananchi wa Ngorongoro kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni.

Rais Samia ameupooza mtanziko wa Ngorongoro kupitia tamko la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi wakati akizungumza na wananchi wa kata 11 zilizopo tarafa ya Ngorongoro, akiwasilisha maagizo ya Rais aliyewatuma kuwasilikiza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku tano wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.

Waziri Lukuvi alisema Rais ameagiza uchaguzi katika tarafa hiyo kwa kutumia mipaka ya zamani, ufanyike kama utakavyofanyika maeneo mengine nchini. Baada ya Rais Samia kuepusha shari Ngorongoro, Serikali iwawajibishe wale waliotufikisha hapo kwa kutotimiza majukumu yao kikamilifu.

Mwaka 1976, kulitokea mauaji ya vikongwe mikoa ya Mwanza na Shinyanga, Serikali kupitia Makamu wa Rais, enzi hizo, Rashidi Kawawa, Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa Usalama, Peter Siyovelwa, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (DGIS), Emelio Mzena, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Samweli Pundugu na kamati za ulinzi za mikoa ya Mwanza na Shinyanga, walijiuzulu.

Katika mahojiano ya Mwanza, watuhumiwa wawili, Masaga Makhula Mazengenuka na Isaack Ng’wana Nkhobhoko wakapoteza maisha mikononi mwa polisi. Mwalimu Nyerere alisafisha wote kutokea juu kwa kuwastaafisha kwa manufaa ya umma, Kawawa akashushwa cheo, wakuu wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga wakafutwa kazi, maofisa wasimamizi, RPC, RSO, OCD na DSO, wote wakapandishwa kizimbani isipokuwa mshitakiwa mmoja tu, RSO wa Mwanza, aliyeponea tundu la sindano kutokana na kutetewa na wakili mahiri, Murtaza Lakha, lakini wengine wote walikula mvua za kutosha.

Hakuna tofauti ya kilichotokea Mwanza lakini mwaka 1976 na kinachofanyika Ngorongoro, kitendo cha Rais Samia kuingilia kati ni cha kupongezwa, lakini waliotufikisha hapo, wanapaswa kuwajibishwa na pili hatua za Rais Samia kuituliza hiyo hali ni funika kombe, tatizo la Ngorongoro bado lipo, litafutiwe ufumbuzi wa kudumu

Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) lilianzishwa mwaka 1959 kwa Wamasai kutoka mbuga ya Serengeti kuhamishiwa Ngorongoro kama eneo la kipekee la matumizi ya mseto ambapo uhifadhi, utalii na maisha ya jadi ya jamii ya Wamasai vingeweza kuishi pamoja.

Idadi ya Wamasai ambayo ilikuja mwanzo kutoka Serengeti ilikuwa takriban 8,000 katika miaka ya 1959, sasa eneo hilo lina watu zaidi ya 100,000. Ongezeko hili la watu limeleta mzigo mkubwa kwenye rasilimali za eneo hilo, hali iliyosababisha uharibifu wa mazingira, ulishaji wa mifugo kupita kiasi na migogoro kati ya uhifadhi wa wanyamapori na shughuli za binadamu na wingi wa watu kutishia ekolojia ya eneo hilo. Japo mpango huu umelenga kuboresha hali ya maisha ya Wamasai ili wapate maisha bora na ya kisasa, unawahatarisha pia watu hao kupoteza uasili wao.

Malengo ya Serikali kuwahamisha Ngorongoro ni jambo jema lakini utekelezaji wake umekumbana na changamoto ikiwemo kuwalazimisha waliogoma kuhama, kutaka kuwahamisha kikuku kwa kutaka kutumia nguvu kwa kuvifuta vijiji na kuzuia vyakula huku akiwakatia huduma muhimu ili kuwashinikiza kuchagua kuhama au kufa njaa kwa Serikali kuvifuta vijiji vyao kinyume cha Katiba, sheria, taratibu na kanuni.

Alichokifanya Rais Samia ni kutuliza mtanziko wa tatizo kwa kulipooza, lakini tatizo bado lipo. Mapendekezo yangu ni; mosi, katika utekelezaji wa mpango huo, Katiba, sheria, taratibu na kanuni za uhamishaji zifuatwe.

Pili, ushirikishwaji wa wahusika kwa kuwatumia viongozi wa Wamasai wenyewe kwa kuanza na malaigwanani wao. Tatu, kufanya tathmini mpya ya kuwatambua Wamasai kama wakazi wa asili na kufanya upembuzi yakinifu nini kina faida zaidi kati ya binadamu na wanyamapori.

Binadamu wakiwa na faida zaidi kiutalii, wanyama ndio wapishe na Tanzania tuanzishe utalii wa wakazi asilia (indigenous people tourism) kama ilivyo kwa wahindi wekundu (red indians) huko Marekani, Aborigines huko Australia na Maori huko News Zealand.

Nne, jamii zote za asili za Tanzania, wakiwemo Wahadzabe, Wamang’ati, Watindiga, Wabarbaig, Wabalungi na jamii asili za makabila mbalimbali zitambuliwe zilindwe na zitunzwe kama kivutio cha utalii.

Tano, kitu muhimu kwenye taifa lolote, haiwezekani mnyama akathaminiwa kuliko binadamu, lakini huyu binadamu akizidi kuzaliana na kutishia ekolojia, lazima adhibitiwe, Marekani walitumia dawa ya kudhibiti uzazi ya Depo Provera, sisi tusifike huko.

Namalizia kwa kuuliza swali hili! Baada ya Rais Samia kuepusha shari kwa kupooza tuu kwa mtindo wa funika kombe, je, Watanzania tujifunze kuukubali ukweli wa tatizo, tutafute ufumbuzi wa kudumu wa tatizo husika, au tuendelee na huu mtindo wetu wa sasa wa kufunika kombe mwanaharamu apite?

Ukweli unabaki pale pale kuwa Ngorongoro kuna tatizo, je, tufunike kombe au tutafute suluhisho la kweli la kudumu kwa kuwatendea haki wana Ngorongoro kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni?

Mungu Ibariki Tanzania.

©Mwananchi
Wazo lako ni zuri, tatizo viongozi tulionao sio, ukiwaambia waongee na viongozi wa wamaasai wao watatanguliza bahasha kuwalainisha hao viongozi bila kujua huenda wakauchochea zaidi mgogoro, mmaasai siyo mzaramo. Wasuruhishi toka ulaya wataweza kufanikisha kwani hawatakua na maslahi upande wowote na wanaaminika zaidi kuliko hawa aina ya akina Nape na Makonda.
 
Back
Top Bottom