Hili la Okrah na Dejan, Juma Ulifanyie Kazi


Sasa Ukiongea hivi utaonekana ni mpinzani. Lakini umeongea Ukweli Tupu.

The man lacks management skills and Confidence. Nadhani pia hana Self - realization.... yaani anaona kama kilichotokea ni bingo badala ya kuonesha skills zake na power Kama kiongozi .

Kitendo kilichotokea JUZI kimedhihirisha hilo.

Inawezekana yeye Mwenyewe anaona labda ni dodo; Hivyo anaweka usela badala ya ku Act Kama manager na Ku exercise power yake. Kama kiongozi upumbavu haupaswi kutokea.
 
Kabisa mkuu......kwa akili ya kawaida inaonekana discipline Ni zero..... cause ikifika hatua ya kupigana wanaume .....ujue Ni shida Sana

Na hapo hata wapatanishwe vpi....lzma kutakuwa na bifu la chini chini
 
Ufupi sio ulemavu

Nakubali but Ufupi unakuja na changamoto zake.

Hata gentleman lazima uwe na kimo... ukimuona mtu kama Boko , Dejan etc etc they are always calm and polite. They are good people.

Njoo kwa hizo short guys Sako , Okrah etc etc wanataka waonekana wao na hii ndio sifa zao. However, exceptional is there, kama vile Phiri ... unaona kabisa ni mtu Mzuri and always he smiles and very humble guy ... so Sio wote lakini majority ni CHANGAMOTO.

Do not take my words personal .... it is just part of it !
 
Kocha mwenyewe kingereza cha kuungaunga anaanzaje kuwafokea au kuwakalipia wachezaji wanaozungumza kingereza tu? Raia wengi wa nchi za afrika wanatudharau watanzani kutokana na kutokujua kingereza.
 

Ulichoandika hapa ni pumba tupu.
 


Je walipigana?

Maana Dejan na Okrah wamepigana.

Wamerushiana ngumu. How do you define that.... labda wewe ufafanue zaid
 
Si bado mnashangilia goli la Sakho lile la CAF? Au mmeshamkinai.
 
Si bado mnashangilia goli la Sakho lile la CAF? Au mmeshamkinai.

Watatolewa Na Timu ya Angola . Amini nikuambiacho.

Yanga atamfunga Alhilal Na ataenda Makundi.

Simba ina wiki 2 kutoka kwenye michuano iwe jua iwe mvua wanatoka.

Hakuna kikosi chenye ushirikiano pale. Kuna wimbi la wahuni lenye akili ya individual success.
 
Nyuzi zote zinazowahusu MAKOLO huwezi kuwaona wakichangia,yanapita na kuchungulia kama yanaaga maiti,mengi yamejazana kwenye nyuzi zinazohusu Wananchi!
Mkuu hicho KISWA-NGLISH kilichomwagwa hapo wanahaha...RAGE woyeeeeee.
 
Though Tokea mwanzo kwenye uzi wako umeandika takataka na vimaneno vya kuokoteza vya kiingereza cha hovyo kuwakoga mamburula wenzio.

Ila hapa kwenye ku-attack vimo vya watu ndio umekosa hoja kabisa. Generalization is illogical, kuna watu wafupi wengi ni humble kuliko hata warefu and vice versa is true. USA kuna marais wengi tu wafupi mfano James Madison, Jimmy Carter, Benjamin Harrison etc

Haya mambo ya wachezaji kuzinguana ni kitu cha kawaida kwenye mpira kwa sababu ni part ya ubinadamu.

Juzi tu ilisambaa clip Richalson anataka kumkwida Vinicius Jr akina Neymar na Alves wakamzuia. Je hao nao sio professional?

Je kipindi Lacazete alivyomkwida mchezaji mwenzie wa Arsenal. Naye sio professional?

Kingine Okrah huwezi kumuweka kwenye kundi la wachezaji wabinafsi. Ni mchezaji ambaye anatoa pasi sana kwa wenzie. Hata goli la pili la Phiri dhidi ya big bullets angekuwa mchoyo asingetoa pasi kwa sababu hata yeye alikuwa kwenye nafasi nzuri tu ya kufunga.
 
If wishes were horses beggars would ride. You may continue to enjoy your wishful thinking.
 

Don’t take my word personal . Nimesema kuna exceptional. Hoja zako zote hazihalalishi misbehaving iliyofanywa na wachezaji wa simba.
 
Mimi sio mfupi nipo above 6ft nazijua taabu za watu wafupi
 
Uzi umeanza vzr ila mwisho umeleta sintofahamu
 
Hata hili litapita mzee, tulishuhudia Mane na Salah inamaana Kloop nae amefeli kwenye mgt?
 
Kocha mwenyewe kingereza cha kuungaunga anaanzaje kuwafokea au kuwakalipia wachezaji wanaozungumza kingereza tu? Raia wengi wa nchi za afrika wanatudharau watanzani kutokana na kutokujua kingereza.
We ni Muongo kuna makocha hawajui kiingereza na wanaheshimika....Mfano kocha Nabi kila mahojiano yake anaongea kifaransa na bado heshima ipo pale pale .....sema mnaona wazungu ndio kila kitu...kumbe hata waafrika wanaweza....
 
Tatizo umeleta upumbavu wa ushabiki mwishoni ila mwanzo umeanza vizuri Simba na Yanga zimeshawatoa akili unaandika hoja nzuri baadae unajidhihirisha umeandika kiushabiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…