Hili la Prof. Assad kumaliza kipindi chake limekaa kisiasa zaidi na siyo kisheria

Mbona huyu CAG mpya alipokuwa TRA mzee alimtoa kwa madai ya kuvurunda,akampeleka Njombe huko,akawa DAS?

Rais hakurupuki, ana timu inayokesha ikikagua kila hatua anayofanya, hivyo ukiona kamteua huyo, jua anafaa.Magufuli ana nia njema na nchi, ana uzalendo na uchungu wa nchi, ana shauku ya kuangamiza umaskini, hivyo aachiwe nafasi atimize majukumu yake.
Kama wewe shabiki wa mpira, angalia pattern jinsi huchezwa, kuna wakati wachezaji hurudisha mpira nyuma ili kupanga mashambulizi vizuri, haitokua haki wewe kama shabiki unazomea zomea tu, kuna muda unafaa ufike wa kuwaamini hao wachezaji na kocha wao, ukijua wana nia nzuri ya kushinda.
 
Hicho kifungu cha CAG ulichokiandika mbona hukuweka "reference" tukisome kwa ukamilifu wake?

Soma namba 7 hapo halafu fata "reference" iliyowekwa hapo uje uweke vifungu vyake.

Huu mchezo hautaki haraka.
Hivi mbona Assad anachukiwa sana na wana wa Lumumba wakiongozwa na Herode? Kati ya CAG walioibua madudu ya serikali Prof Assad ni namba 1, Je wana Lumumba hamtaki Prof Assad kufichua ufisadi ndani ya serikali?
 
Mkuu huu uteuzi Wa Jana rais ama ameshauriwa vibaya au amekurupuka.mwanzoni niliamini hayo usemayo lakini kadiri muda unavyokwenda nimeridhika nilikosea kuamini hivo.
 
Sasa mbona Assad ana miaka 58 vipi sasa...
 
Mkuu huu mtazamo Wa kila anayeteuliwa Na rais anaweza ondolewa wakati wowote Ni uwongo nimeona rais Leo naye kasema, sio kweli.vipi jaji Mkuu akiteuliwa aweza tenguliwa?
 
Hii kitu imekaa vibaya. Kwa kifupi ni kwamba JPM kamtumbua Assad kwa sababu anazozijua mwenyewe. CAG hajastaafu kwani bado hajagonga 60 years. Inaleta ukakasi sana kama JPM ana nia ya dhati kabisa ya kupambana na wizi wa fedha za Umma
Niliwahi kuandika humu kuwa Jiwe ndo mhujumu uchumibna fisadi # 1. Lakini anamjua Prof. Assad ni mtu wa dizaini gani; hawezi kuwa naye.
 
Ndo tuelezwe sasa hicho kilichosababisha asiteuliwe kwa awamu ya pili. Na je, kuhojiwa na Bunge ndo njia ya kisheria ya "investigation" dhidi yake?
 
Pascal uliwahi kusema kuwa una taaluma ya sheria. Je, hii phrase ya "....and shall be eligible for ...." unaielewaje kisheria?
 
Pia ni kwamba tunavyomfahamu Assad ni kishabiki zaidi kuliko ambavyo JPM alivyo na taarifa zake.
 
Angekuwa Hana Nia ya dhati hivi ingewezekana vipi akanunua madege karibu kumi ndani ya miaka minne..hujiulizi..wewe...hata kidogo..haya mapesa si yote angeyatia ndani..angeyalamba yote, wee vipi bana..
Ukisikia ufisadi, uhujumu uchumi, ubadhirifu au utakatishaji fedha umetetendeka basi fahamu lazima kuna biashara (dili) imefanyika au ilitakiwa ifanyike.

Kupitia biashara ya ununuzi wa "midege" inaweza kuwa, bali kuna kila dalili ya kufanyika ufisadi ukizigantia kuwa haijawahi kukaguliwa. Tunachokifahamu kupitia ripoti za CAG ni kwamba kuna pesa zimechotwa hazina kupelekwa Ikulu na Ikulu.
 
Wewe unahitaji ukumbushwe kitu. Kwanza kabisa wengi wameshatolea ufafanuzi wa matumizi/maana ya neno "shall" (siyo "may") kisheria kuwa ni "lazima" iwe au fanyike. Pili, kuna neno (kiunganishi) limetumika "and" (sio "or") ambalo wengi waliotoa ufafanuzi pamoja na wewe mnalisahau. Kwa kutumia neno "and" maana yake ni kwamba muhula wa kwanza wa miaka mitano unatakiwa "ujumlishwe" na muhula mungine wa ziada ndipo astaafu.
 
Niliwahi kuandika humu kuwa Jiwe ndo mhujumu uchumibna fisadi # 1. Lakini anamjua Prof. Assad ni mtu wa dizaini gani; hawezi kuwa naye.
Ile 1.5T ilileta nongwa kuu na nilijua it was just a matter of time.
 
Hivi mbona Assad anachukiwa sana na wana wa Lumumba wakiongozwa na Herode? Kati ya CAG walioibua madudu ya serikali Prof Assad ni namba 1, Je wana Lumumba hamtaki Prof Assad kufichua ufisadi ndani ya serikali?
Kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani.
 
Kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani.
Labda pia ni kwa sababu ndege wafananao huruka pamoja. Mamba na Kenge wakiongozana si rahisi kuwatofautisha. Hilo moja lakini la pili ni kwamba ni vigumu kuwakuta wakishambuliana. Sasa naomba nikuulize swali, hivi wewe tukuweke upande gani...wa mamba au kenge?
 
Mkuu huu mtazamo Wa kila anayeteuliwa Na rais anaweza ondolewa wakati wowote Ni uwongo nimeona rais Leo naye kasema, sio kweli.vipi jaji Mkuu akiteuliwa aweza tenguliwa?

Jaji anaweza kuwekwa benchi akakosa cha kufanya. Kama ni uongo, mbona tunashuhudia lila wakati mambo yanatokea?
 
Siku zote nasimamia haki. Niweke kwa walio kwenye haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…