Hili la Prof. Assad kumaliza kipindi chake limekaa kisiasa zaidi na siyo kisheria

Hili la Prof. Assad kumaliza kipindi chake limekaa kisiasa zaidi na siyo kisheria

Mbona huyu CAG mpya alipokuwa TRA mzee alimtoa kwa madai ya kuvurunda,akampeleka Njombe huko,akawa DAS?

Rais hakurupuki, ana timu inayokesha ikikagua kila hatua anayofanya, hivyo ukiona kamteua huyo, jua anafaa.Magufuli ana nia njema na nchi, ana uzalendo na uchungu wa nchi, ana shauku ya kuangamiza umaskini, hivyo aachiwe nafasi atimize majukumu yake.
Kama wewe shabiki wa mpira, angalia pattern jinsi huchezwa, kuna wakati wachezaji hurudisha mpira nyuma ili kupanga mashambulizi vizuri, haitokua haki wewe kama shabiki unazomea zomea tu, kuna muda unafaa ufike wa kuwaamini hao wachezaji na kocha wao, ukijua wana nia nzuri ya kushinda.
 
Hicho kifungu cha CAG ulichokiandika mbona hukuweka "reference" tukisome kwa ukamilifu wake?

Soma namba 7 hapo halafu fata "reference" iliyowekwa hapo uje uweke vifungu vyake.

Huu mchezo hautaki haraka.
Hivi mbona Assad anachukiwa sana na wana wa Lumumba wakiongozwa na Herode? Kati ya CAG walioibua madudu ya serikali Prof Assad ni namba 1, Je wana Lumumba hamtaki Prof Assad kufichua ufisadi ndani ya serikali?
 
Rais hakurupuki, ana timu inayokesha ikikagua kila hatua anayofanya, hivyo ukiona kamteua huyo, jua anafaa.Magufuli ana nia njema na nchi, ana uzalendo na uchungu wa nchi, ana shauku ya kuangamiza umaskini, hivyo aachiwe nafasi atimize majukumu yake.
Kama wewe shabiki wa mpira, angalia pattern jinsi huchezwa, kuna wakati wachezaji hurudisha mpira nyuma ili kupanga mashambulizi vizuri, haitokua haki wewe kama shabiki unazomea zomea tu, kuna muda unafaa ufike wa kuwaamini hao wachezaji na kocha wao, ukijua wana nia nzuri ya kushinda.
Mkuu huu uteuzi Wa Jana rais ama ameshauriwa vibaya au amekurupuka.mwanzoni niliamini hayo usemayo lakini kadiri muda unavyokwenda nimeridhika nilikosea kuamini hivo.
 
Kinasema kwa vyovyote atastaafu akifikisha miaka 60 maana yake Nini ? Raisi aweza mteua mtu awe CAG akiwa na miaka 58 Mfano.Huyo CAG akifikisha miaka 60 lazima aondoke bila kujali kuwa aliyemteaua kampa miaka mitano.
Kuna ma CAG kibao wa Tanzania Kuna mdau kaweka wako waliodumu miaka miwili wengine mitatu wakaondoka
Sasa mbona Assad ana miaka 58 vipi sasa...
 
Na sheria inayompa madaraka Rais inasemaje? Nchi zetu maskini zina shida moja....hizi sheria hazijaunganishwa in the sense that they create a balance. Zimeundwa as if CAG is very independent. Kumbe ni mteuliwa na Rais na kama anateuliwa, kwanini asiondolewe? Maana baada ya kumteua, hakwenda bungeni for approval.
Mkuu huu mtazamo Wa kila anayeteuliwa Na rais anaweza ondolewa wakati wowote Ni uwongo nimeona rais Leo naye kasema, sio kweli.vipi jaji Mkuu akiteuliwa aweza tenguliwa?
 
Hii kitu imekaa vibaya. Kwa kifupi ni kwamba JPM kamtumbua Assad kwa sababu anazozijua mwenyewe. CAG hajastaafu kwani bado hajagonga 60 years. Inaleta ukakasi sana kama JPM ana nia ya dhati kabisa ya kupambana na wizi wa fedha za Umma
Niliwahi kuandika humu kuwa Jiwe ndo mhujumu uchumibna fisadi # 1. Lakini anamjua Prof. Assad ni mtu wa dizaini gani; hawezi kuwa naye.
 
Iko hivi, tenure ni miaka 5. Iwapo CAG akiwa chini ya any kind of investigation (yeye Bunge lilimuita kujieleza/kujibu tuhuma), sasa huwezi jua recommendation ya huo muhimili ilikuwaje. Be matured, na mamlaka hailazimiki kuendelea na mtu kama inaona ana kiuka miiko ya kazi zake.
Ndo tuelezwe sasa hicho kilichosababisha asiteuliwe kwa awamu ya pili. Na je, kuhojiwa na Bunge ndo njia ya kisheria ya "investigation" dhidi yake?
 
Assad hajang'olewa, bali miaka yake mitano ilifikia ukomo, na hakuwa re appointed ili kusubiria umri wa miaka 60.

Katika uteuzi huu mpya, JPM amefanya kama walivyomfanyia Tido pale TBC, mkataba ulipoisha tuu, akateuliwa. Kikawaida muda wa mkataba wenye reappointiment extention, ukifika, kama huna nia ya kumpa extension, anatakiwa kuwa notified in writing 28 days prior to due date.
Prof Assad has never been notified.

Huyo ndiye JPM.
P
Pascal uliwahi kusema kuwa una taaluma ya sheria. Je, hii phrase ya "....and shall be eligible for ...." unaielewaje kisheria?
 
Iko hivi, tenure ni miaka 5. Iwapo CAG akiwa chini ya any kind of investigation (yeye Bunge lilimuita kujieleza/kujibu tuhuma), sasa huwezi jua recommendation ya huo muhimili ilikuwaje. Be matured, na mamlaka hailazimiki kuendelea na mtu kama inaona ana kiuka miiko ya kazi zake.
Pia ni kwamba tunavyomfahamu Assad ni kishabiki zaidi kuliko ambavyo JPM alivyo na taarifa zake.
 
Angekuwa Hana Nia ya dhati hivi ingewezekana vipi akanunua madege karibu kumi ndani ya miaka minne..hujiulizi..wewe...hata kidogo..haya mapesa si yote angeyatia ndani..angeyalamba yote, wee vipi bana..
Ukisikia ufisadi, uhujumu uchumi, ubadhirifu au utakatishaji fedha umetetendeka basi fahamu lazima kuna biashara (dili) imefanyika au ilitakiwa ifanyike.

Kupitia biashara ya ununuzi wa "midege" inaweza kuwa, bali kuna kila dalili ya kufanyika ufisadi ukizigantia kuwa haijawahi kukaguliwa. Tunachokifahamu kupitia ripoti za CAG ni kwamba kuna pesa zimechotwa hazina kupelekwa Ikulu na Ikulu.
 
Shall be eligible unajua maana yake, shall hold office for fixed term of 5 years kwako inaeleweka vipi? Maana yake baada ya hiyo miaka 5, anaweza kuendelea tena mingine 5 unless awe amefikisha miaka 60, mteuaji akiona hiyo miaka 5 inatosha kavunja sheria ipi? Mimi namkubali sana Asad, lakini ukweli ni kwamba rais hajavunja katiba.
Wewe unahitaji ukumbushwe kitu. Kwanza kabisa wengi wameshatolea ufafanuzi wa matumizi/maana ya neno "shall" (siyo "may") kisheria kuwa ni "lazima" iwe au fanyike. Pili, kuna neno (kiunganishi) limetumika "and" (sio "or") ambalo wengi waliotoa ufafanuzi pamoja na wewe mnalisahau. Kwa kutumia neno "and" maana yake ni kwamba muhula wa kwanza wa miaka mitano unatakiwa "ujumlishwe" na muhula mungine wa ziada ndipo astaafu.
 
Niliwahi kuandika humu kuwa Jiwe ndo mhujumu uchumibna fisadi # 1. Lakini anamjua Prof. Assad ni mtu wa dizaini gani; hawezi kuwa naye.
Ile 1.5T ilileta nongwa kuu na nilijua it was just a matter of time.
 
Hivi mbona Assad anachukiwa sana na wana wa Lumumba wakiongozwa na Herode? Kati ya CAG walioibua madudu ya serikali Prof Assad ni namba 1, Je wana Lumumba hamtaki Prof Assad kufichua ufisadi ndani ya serikali?
Kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani.
 
Kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani.
Labda pia ni kwa sababu ndege wafananao huruka pamoja. Mamba na Kenge wakiongozana si rahisi kuwatofautisha. Hilo moja lakini la pili ni kwamba ni vigumu kuwakuta wakishambuliana. Sasa naomba nikuulize swali, hivi wewe tukuweke upande gani...wa mamba au kenge?
 
Mkuu huu mtazamo Wa kila anayeteuliwa Na rais anaweza ondolewa wakati wowote Ni uwongo nimeona rais Leo naye kasema, sio kweli.vipi jaji Mkuu akiteuliwa aweza tenguliwa?

Jaji anaweza kuwekwa benchi akakosa cha kufanya. Kama ni uongo, mbona tunashuhudia lila wakati mambo yanatokea?
 
Labda pia ni kwa sababu ndege wafananao huruka pamoja. Mamba na Kenge wakiongozana si rahisi kuwatofautisha. Hilo moja lakini la pili ni kwamba ni vigumu kuwakuta wakishambuliana. Sasa naomba nikuulize swali, hivi wewe tukuweke upande gani...wa mamba au kenge?
Siku zote nasimamia haki. Niweke kwa walio kwenye haki.
 
Back
Top Bottom