Uchaguzi 2020 Hili la Sheikh Ponda liacheni. Hatua ya Ponda ni kwa maslahi ya Waislam na Watanzania

Sasa mtu kama Sheikh Kipozeo naye ni wa kumtilia maanani yeye kazi yake kuzungumzia makalio ya Wanawake tu
Huyu Sheikh huwa anazingua sana..

October 28th kura zote za ndio ni kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Hudhuria mikutano yake ndugu, SIKILIZA
Kama ahadi zake sio za kutetea haki zinazovunjwa
Rudi kampigie kura JPM
Ndugu mimi nafuatilia Sana kampeni hizi
Sijasikia magufuli. Majaliwa wala Samia akiongelea kero za waislam
Kuanzia mashekh wetu mpaka mashule yanayoungua kila kukicha hakuna uchunguzi
Wakati wa mwinyi waislamu serikalini walikua 20%--25%
Wakati wa mkapa 28%--30%
Wakati wa Jakaya 30%--36%
Wakati huu chini ya 18%
Je waislamu tumepoteza uwezo kwa kiasi hicho?
Jipime mwenyewe
 
Mwenyezi Mungu ambariki Sheikh Ponda ampe umri mrefu wenye baraka hapa duniani na mwisho wa maisha yake akaione pepo!
Mwenyezi Mungu na awaadhibu masheikh njaa waliopokea vipande vya fedha kutoka kwa madhalimu ccm waipondee haki na wapenda haki
 
Niko na wewe kaka wenda nilikosea kuituma hii ilikuwa inaenda kwa mtete mmoja wa JPM
 
Kwenu Masheikh na wahadhiri wetu
Nawasalimien Assalam Aleikum.

Jana mmefanya press conference, mmezungumza na kutoa kauli yenu kuhusu hatua ya Sheikh Ponda kusimama na kuwataka Waislamu na wananchi wamchague mheshimiwa Lissu katika uchaguzi huu...


Binafsi huwa nachukia sana mtu anaeingiza mambo ya dini kwenye utawala wa umma/serikali ama kuhusianisha siasa na dini. Serikali yetu hainaga dini ila wenye dini ni sisi wananchi, sasa habari za mashehe kuanza kuongelea siasa zinatokaga wapi?

Kazi yao ni kuhubiri neno la Mungu ili watu tumjue na kumtumikia Mungu, habari ya sijui serikali ya ccm imewafunga mashehe inatoka wapi, kama mtu unakiuka maadili ya nchi na kutaka kusababisha amani ya nchi kutoweka kwanini usichukuliwe hatua. Nakupa mfano tu maana naona umeegemea upande wa dini moja tu (uislam).

Hebu itokee hapa mhubiri yeyote wa kikristo iwe Gwajima, mwamposa, mwakasege au yeyote yule unae mjua wewe ambae ni mkristo alafu aanze kuhubiri maada ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wa nchi, trust me nao watawafata mashehe huko huko segerea.

Serikali haiwezi kuvumilia watu ambao wanaweza kuivuruga aman ya nchi kwa kupandikiza sumu miongoni mwa waumini wao. sisi hapa tanzania hatupo kama Saudia arabia, ama Iran ama wapi huko kwingineko ambako Serikali inaongoza kwa misingi ya kidini, tanzania hatuko hivo kila mtu aabudu dini anayoijua yeye na wala hairuhusu kuibeza dini ya mwenzio, mtu dini yake anaijua yeye mwenyewe wewe uikosoe dini ya mtu unakuhusu nini.

Tumwabudu Allah wetu mmoja,tutende mema ila usikiuke misingi ya amani ya nchi yako
 
Binafsi huwa nachukia sana mtu anaeingiza mambo ya dini kwenye utawala wa umma/serikali ama kuhusianisha siasa na dini, Serikali yetu hainaga dini ila wenye dini ni sisi wananchi, sasa habari za mashehe kuanza kuongelea siasa zinatokaga wapi ?..
Hizi Habari zote zinakuja baada ya sheikh Ponda kujitokeza hadharani Lakini wakati mashekh wanafiki wa BAKWATA waliyokuwa wanampigia kampeni yule katili mlikua hamna shida kuchanganya dini na siasa. Sisi waislamu tunasema kuna mashekh wetu wapo jela bila kufikishwa mahakamani na wanateswa Sana mpaka wengine wamehasiwa kwa kuminywa korodani.

Hatusemi waachiwe wala hatutaki kuishi na magaidi ila tunaomba serikali iwapeleke mahakamani na kama wanakosa wahukumiwe na kama la waachiwe. Hicho ni kilio chettu kwa miaka. Tundu lissu ni mwana siasa pekee amesema atalishughulikia swala Hilo.

Waislamu wote wa kweli kura zetu kwa Lissu.

Waislamu wanafiki kura zao kwa kiongozi katili.
 
Endorsements imefanywa tayari na sheikh ponda....
Wale masheikh ni walaji wa kitimoto,wazinzi,wachawi(sheikh sharrif majibu),na wanafiki hata kama wangezungukunga nchi nzima kupinga kauli ya sheikh ponda bado Sisi watanzania tunajua ukweli uko wapi
 
Mnataka haki ee? Hamtoipata haki hiyo! Taifa hili la Mungu haliko tayari kuchomwa moto kwa ajili ya hiyo haki yenu mnayoitaka.
Ngoja muingie kwenye 18 ndio mtajiona mlivyo wajinga
 
Je unaweza kuuthibitishia Ummah hayo maneno yako
Japo speech moja tu lissu akisema?
KUHUSU HAYO?
Nadhani ungetaguliza uthibitisho wako kwanza kwa Alhady the way ulimvomsema hapa awali then na mimi nitathibitisha ikiwemo uhuru wa faragha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…