Hili la Simba SC na Stand Utd kuvaa jezi zinazofanana,nashauri TFF ihamishiwe TAMISEMI

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
899
Reaction score
1,231
Huuo mpira wa bongo sio poa ni vyema TFF ihamishiwe TAMISEMI rais ateue mwenyewe maana kila anayeteuliwa madudu kuliko ya mwanzo

Anaandika shaffih Dauda;

Goodmorning!Nimefuatilia kwenye vyanzo vyangu vyote kutaka kufahamu kwanini Simba SC na Stand UTD walivaa jezi zinazofanana,kwenye pre match meeting iliyohudhuliwa na viongozi wa vilabu vyote pamoja na kamisaa (Jovin Bagenda) na mwamuzi wa mchezo huo (Kinungani Selemani )

Kanuni zinasemaje? (i) Kamishna atahakikisha timu zinatumia sare kwa mujibu wa rangi za
nyumbani na ugenini kama zilivyoandikishwa na klabu zenyewe kwa TFF. (j) Timu zitaheshimu uchaguzi wao wa rangi za sare zao kwa michezo ya nyumbani na ugenini, na endapo itatokea timu ya nyumbani kukosa uzingativu wa kuwasilisha rangi sahihi kwa sare zake kwa mechi za
nyumbani katika kikao kitangulizi cha mchezo (pre match meeting) timu ngeni itakuwa na haki ya kwanza ya kuchagua rangi ya sare katika mchezo husika.

Baada ya utafiti wangu nimejiridhisha ya kwamba Simba hawakuwa tayari kuvaa jezi za ugenini kutokana na maagizo ya 'KAMATI' ikabidi kamishna wa mchezo akubali kwasababu jezi za Stand zilikuwa ni za rangi ya machungwa na Simba rangi nyekundu kwaiyo zisingewasumbua waamuzi.
 

Attachments

  • Screenshot_20171002-161642.png
    77.1 KB · Views: 43
Je, ni sahihi kuvaa jezi za nyumbani katika mechi za ugenini
 
Matopeni waligoma kuvaa jezi nyeupe ambayo ni rasmi jezi yao kwenye away games
 
Msichokijua ni kwamba aliyepewa jukumu la kupeleka jezi zile KWA BABU alikosea na kubeba nyekundu fasta, kuja kustuka kuwa wapo away wanatakiwa kuvaa nyeupe game inakaribia na hawawezi kufika kwa babu kupeleka jezi, sasa masharti wameshakosea kwahiyo wakaamua kujitoa ufahamu na kugoma kuvaa jezi za away kwani walikuwa washaambiwa mkiingia na nyeupe mmeliwa kichwa.
 
Je, ni sahihi kuvaa jezi za nyumbani katika mechi za ugenini
Wanasema ni zamu yao sasa. Matop wawili wa TFF ni wanachama hai wa Simba. Msomali na Makamu wake.
Kelele za Malinzi hazikuwa kutaka usawa bali kubebwa wao. Kibaya zaidi upendeleo wa Malinzi kwa Yanga ilikuwa ni imaginary kuliko uhalisia.
Sasa wanao Karia na Wambura na Kamati karibia zote
 
Je, ni sahihi kuvaa jezi za nyumbani katika mechi za ugenini
Ni sahihi kama mgeni na mwenyeji wanatofautiana rangi za jezi zao za nyumbani eg yanga na simba wanaweza kuvaa jezi zao za nyumbani kila wakikutana, Ila walichofanya simba dhidi ya stand ni upuuzi
 

Msimu uliopita Stand United walivaa hizo hizo jezi za orange walivyocheza na Simba hapa Dar na hakukuwa na tatizo. Leo mnalaumu Simba wakati sio jambo geni katika mpira wetu
 

Msimu uliopita Stand United walivaa hizo hizo jezi za orange walivyocheza na Simba hapa Dar na hakukuwa na tatizo. Leo mnalaumu Simba wakati sio jambo geni katika mpira wetu
Kwahiyo wanalipiza kisasi?

Ni unproffesion kwa club ambayo inataka kubadili mfumo wa kizamani kwenda kisasa kufanya jambo la hovyo kisa tu iliwahi tokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…